Kungekuwa na makampuni mengine ya umeme Tanesco ingezidisha ufanisi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270
Enzi za Tanesco kuwa monopoly msambazaji wa umeme zimepitwa na wakati. Huu ulikuwa mfumo wa Ujamaa, enzi za collectiveness. Hakukuwa na ushindani wa kibiashara.

Makampuni mengine yakaribishwe na kupewa zabuni ya kusambaza umeme. Wananchi wapewe uhuru wa kuhama kwa supplier mwenye huduma nzuri na bei bafuni.

Makampu hayo yapate mgao kutoka kwenye gridi ya taifa na walipe kodi kwa serikali.

Matatizo ya umeme kukatika yatakwisha. Hakuna atakaetaka kupoteza wateja.
 
Wazo la hekima/akili sana hili... Ni sawa na mke mvivu, ukimuolea mke wa pili lazima aongeze ufanisi na kujituma zaidi.
Kule kite ambako mashirika ya umma yalitoa huduma kwa wananch enzi za Ujamaa ukiondoa China wameshaachana na mfumo huo.

China ukiwa kiongozi na ukaihujumu kampuni ya umma Dhabi ni kufungwa maisha au kunyongwa.
 
Kule kite ambako mashirika ya umma yalitoa huduma kwa wananch enzi za Ujamaa ukiondoa China wameshaachana na mfumo huo.

China ukiwa kiongozi na ukaihujumu kampuni ya umma Dhabi ni kufungwa maisha au kunyongwa.
Ndio maana china makusanyo yao ya mapato wanavuka hata "BUDGET" ya matumizi ya serikali yao, hela zinatosheleza na kubakia na ndio maana wanamkopesha mpaka marekani kwenye budget yao.

China ni kosa, ila kwetu huku kuihujumu nchi ni "SIFA".
 
Back
Top Bottom