Kungekuwa na upinzani imara huu ulikuwa wakati sahihi kuiondoa CCM madarakani

beny jr

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
822
1,133
Natumaini nyoote mu wazima wa afya wataalamu wa siasa na propaganda zake ni mara yangu ya kwanza kuandika huu uzi kwenye jukwaa hili pendwa.zamani nilikua nachukia siasa lakini baada ya kwenda shule kidogo na kuona athari za maamuzi ya kisiasa yananigusa moja kwa moja mimi ambae sikua kwenye mlengo wowote kisiasa zaidi ya kuvutiwa na popural readers wa nyuma kama JK NYERERE,JK KIKWETE ambaye huyu nilianza kumjua baada ya skendo ya waziri mkuu wake mh LOWASA

Katika kufuatilia kwangu siasa kuna wanasiasa niliwapenda nikatamani kuwa kama wao mmoja ni hayati KINGUNGE NGOMBALE MWILU, DR MTIKILA na mwingine aliyekuja karibuni ambaye aliitwa jina bora kabisa la SHUJAA WA AFRIKA na ye si mwingine ni JOHN.POMBE MAGUFULI ambao wote hawa ni marehemu mwenyezi mungu azilaze roho za watu hawa pepon amina.

Lengo la kuandika huu uzi ni baada ya kuangalia nakufuatilia yanayoendelea nchini nimeona kuna mwanya kama kungekua na upinzani au mpinzani ambaye angejipambanua vizuri kisiasa 2025 ninaiona kabisa CCM kuitwa chama cha upinzani bila hata kumwaga damu kama watu wengine wanavyodhani kuwa kuiondoa CCM kwenye box la Kura ni ngumu hoja zangu ni kama zifuatazo kwanini upinzani unaweza kuondoa ccm madarakani kirahisi

SUALA LA KATIBA MPYA
Hili suala chini ya utawala wa mh Samia Suluhu hasa amefeli kabisa kucheza nalo kisiasa naona kama wanatumia nguvu kubwa kujibu hoja za wanaodai hii katiba kuliko kujibu kisiasa kitendo cha kumpa. Mh Mbowe kesi ya ugaidi katika kipindi ambacho anapigania katiba na haki ya kukusanyika ni ishara ya ushindi kwa upinzani na hoja yao kupata mashiko ndani na nje ya nchi kwakua sasa hivi mpaka vyombo vya Magharibi vinaripoti hii issue na sababu zikitajwa ni kudai katiba mpya ndizo zilizopelekea kupewa tuhuma hizi nzito na kwa utafiti wangu wengi wanaamini katiba iliyopo inainufaisha CCM hivyo CCM kukataa hii hoja ni kielelezo kuwa ccm hawewezi kushindana kwenye ulingo huru wa kidemocrasia na wananchi wanajua hili


SUALA LA CORONA
hii hoja ya corona ni mwiba mkali kwa ccm hii inakuja baada ya mgawanyiko mkubwa uliopo ndani ya chama hiki tawala kuanzia wabunge na viongozi wa huku chini wengi wanaamini maamuzi aliyoyafanya Hayati magufuli yalikua maamuzi sahihi juu ya mapambano ya hili gonjwa la corona kuliko kuwaletea chanjo ni hili linachangiwa na kauli tata kuanzia Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya Waziri Mkuu anasema idadi ya wagonjwa ni wachache sana Rais anasema idadi ni kubwa na waziri wa afya anacheza ngoma ya Rais akitokea mwanasiasa anasimama na maamuzi ya magufulification kwenye agenda yake ya 2025 ccm kwisha habari yake.


KIVULI CHA JPM KINAITESA SANA CCM
Huyu mwamba alijizolea watu sana kwa falsafa yake ya utawala anawafuasi wengi mnoo ndani ya chama na nje ya chama alikishika ipasavyo chama kitendo cha kutaka. Kuzima haya majaribio naona naona ndio chama kinapoteza ushawishi kwa watanzania akija politician 2025 akasema ntafuata sera za JPM nadhani mchana kweupe CCM inaanguka
 
Upinzani ni pamoja na wewe na mimi lkn tupo hapa kwa fake ID maana tu waoga ku sacrifice!
 
Back
Top Bottom