Kungeanzishwa shule zinazofundisha Elimu ya Sekondari kwa lugha ya Kiswahili

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Habari za leo wakuu,

Natumai mu wazima wa afya tele. Lakini pia poleni na mihangaiko ya kulisaka tonge.

Sasa ni hivi, leo wakati naperuzi makabrasha yangu kichwani nimejikuta napata wazo hili, kwamba kungejitokeza watu waanzishe shule za Sekondari zitakazo fundisha elimu ya Sekondari kwa lugha ya Kiswahili.

Nadhani hii ingekuwa nzuri sana wakuu kuwasaidia wale ambao hawafaulu kujiunga na kidato cha kwanza kwa lugha ya Kiingereza badala yake wao wajiunge kidato cha kwanza kwa lugha ya Kiswahili.

Lakini pia kuanzishwe na vyuo vitakavyo fundisha elimu ya chuo kwa lugha ya Kiswahili.

Naombeni michango yenu wakuu ninyi mnalionaje hili.
 
Sioni umuhim wa kuanzishwa kwake. Wakati shule za serikal zipo. Simplh tu wabadilishe mtaala
 
Habari za leo wakuu,

Natumai mu wazima wa afya tele. Lakini pia poleni na mihangaiko ya kulisaka tonge.

Sasa ni hivi, leo wakati naperuzi makabrasha yangu kichwani nimejikuta napata wazo hili, kwamba kungejitokeza watu waanzishe shule za Sekondari zitakazo fundisha elimu ya Sekondari kwa lugha ya Kiswahili.

Nadhani hii ingekuwa nzuri sana wakuu kuwasaidia wale ambao hawafaulu kujiunga na kidato cha kwanza kwa lugha ya Kiingereza badala yake wao wajiunge kidato cha kwanza kwa lugha ya Kiswahili.

Lakini pia kuanzishwe na vyuo vitakavyo fundisha elimu ya chuo kwa lugha ya Kiswahili.

Naombeni michango yenu wakuu ninyi mnalionaje hili.
Yaani tuko hapa kuzungumzia Kingereza kama tatizo Tanzania

Naona ndugu yangu wewe ni hujui lolote kabisa..

Tanzania kwenye lugha,tena zote Kingereza na Kiswahili watoto hawana shida navyo,ndio masomo wanayofaulu zaidi ya mengine..

Shida ya Tanzania ni elimu ya Sayansi na Hisabati,watoto wanafeli zaidi ya masomo mengine yote put together..

Na wanaomudu kuyasoma ni wachache sana kwa idadi...

Masomo yaliyojaza watoto ni ya lugha na historia,ila sio Sayansi na Hisabati...

Njoo hapa na solution ya Sayansi na Hisabati kwanza halafu baadae ndio uje na huu ujinga ulioandika hapa...
 
Sasa mbona unanifokea chief.
 
Hayo maelezo uliyo yatoa ndio nimeyalenga chief. Watoto hawaelewi sayansi kwasababu ya lugha. Nadhani umenipata. Shule ya msingi sayansi na hisabati ni nyepesi kwasababu tunatumia kiswahili kama lugha ya kufundishia.
 
Nani kakwambia watoto wanafaulu zaidi Sayansi na Hisabati shule ya msingi zaidi ya masomo mengine?

Kingereza hakina mjadala,ni LAZIMA watoto wetu wasome,hutaki peleka wanao kwenye hivyo viswahili unavyotaka then tuje tuone nani ataenda kuomba ajira kwa nani!

Unachosema ni wishful thinking maana hakuna mzazi atataka mwanae asisome Kingereza,hakuna wewe included!

Mtanzania hashindani na Mtanzania mwenzake tu,anashindana na Walimwengu wote,halafu ulimwengu unashindana nao kwa Kiswahili?

Who told you that?
 
Back
Top Bottom