Kung'atuka kwa Nyerere, alionesha kwa VITENDO, kuwa ipo siku CCM nayo ing'atuke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kung'atuka kwa Nyerere, alionesha kwa VITENDO, kuwa ipo siku CCM nayo ing'atuke

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, Jun 11, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kama ambavyo wengi hawakutarajia Mwl. Nyerere aliomba kung'atuka ikiwa ni mpango wake wa kuonesha kuwa nchi inaweza ikaendelea bila yeye Nyerere kuwepo madarakani, aliomba afanye hivyo wakati bado ananguvu ili aweze kutoa mchango wake ktk kipindi ambacho nchi itaendelea bila ya yeye kuwepo madarakani. Nadhani alisaidia sana kwa siasa za ndani ya chama kuachiana madaraka bila ugomvi na hati hati za chama kufa.

  Suala hili lilimjengea sifa na heshima kubwa duniani, lakni kama binadamu wenye akili tunazifunza mambo mengi kwa somo hilo la Nyerere. Kwanza ni makosa makubwa kutaka kuonesha kuwa bila CCM nchi haiwezi kuendelea, pili utaratibu wa kupisha ungali bado una nguvu ili utoe mchango wako ktk kuruhusu mabadiliko, tatu nchi ni moja vyama ni vingi kwa nini utawala milele? sio busara kufanya hivyo hata kama mazingira yatakuruhusu kama yalivyokuwa yanamruhusu Nyerere ( uwezo mkubwa wa Mwalimu wa kufikiria zaidi ya leo na kesho unajionesha hapo).

  Nyerere alitaka tujifunze kupishana ktk uongozi ndani ya chama hata na vyama kwa vyama ili mradi manufaa ni kwa taifa la tz. Utakumbuka aliwahi kusema CCM sio baba wala mama, anaweza kuondoka na kujiunga na chama kingine chenye maono na mwelekeo wa kuwakomboa watanzania. Wakati wa mwisho mwisho wa uhai wake Nyerere aliikosoa sana CCM, wapo waliompuuza na kusema mzee apumzike zake butiama, eti amechoka huyo na mengine mengi.

  Kama Nyerere alionesha kuwa unaweza kuacha madaraka kwa mtanzania mwingine, nahisi kama kungekuwepo vyama vya siasa vingi wakati huo angewaomba wenzake wakipishe chama kimojawapo kwa maana ya kukabidhi serikali kwa chama kingine. Kwa nyerere huenda hili lingewezekana, ndo maana aliikosoa CCM hadharani, alipinga sera za kulipa madeni ili upate sifa za kukopeshwa, alipinga ubinafishaji wa mali ya UMMA,alipinga viongozi wa africa kutumika kama wakala wa nchi tajiri, alipinga ubeberu na ukoloni mamboleo.

  Wito wangu kwa CCM, kama nyerere alipima na kuona enzi hizo ni bora kujenga utamaduni wa kuachiana madaraka kwa maana ya kumpa fursa mtanzania mwingine kuongoza serikali na nchi, ni wakati CCM ili kumuenzi baba wa taifa kutoa fursa kwa mtu mwingine wa chama kingine kuongoza serikali, nyumba ni moja kama watz tunadhani CCM wanajenga vibaya, wape CDM au chama kingine (ili mradi watu ndo wamepitisha) nafasi ya kujenga nyumba hiyo hiyo kwa ustadi mkubwa zaidi, hii ndo namna pekee kwa muungwana yeyote kuweza kutetea hoja yake. Kama CCM mtang'ng'ania, TZ haiwezi kupima kwa kina uchapakazi wenu, lazima kubadilisha ili kupata vigezo na kipimo kilicho sahihi sana.

  CCM KUNG'ATUKA SIO KOSA ni kipimo cha ukomavu ktk fikira, nyerere alikitumia na nyinyi kitumieni kulinda maslahi ya nchi.
   
Loading...