Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,252
Serikali yetu imekuwa ikihubiri katika huduma bora za afya katika hospitali zake na haswa Uwepo wa huduma bure wa makundi maalumu ya wazee kuanzia miaka sitini (60) na kuendelea, na watoto umri chini ya miaka mitano.
Ila ukweli ni kwamba hali halisi huko mahospitalini ni tofauti sana na kauli mbiu ya serikali yetu, kutokana na kwamba zile huduma za bure za wazee baadhi ya hospitali za serikali ni lazima kulipia kwa madai kuwa huduma hizo ni kwa Hospital za wilaya tu.
Jana nikiwa mjini Moshi nilimsindikiza rafiki yangu Hospital ya Mkoa ya Mawenzi ambapo alikuwa anampeleka babake kwa ajili ya matibabu,tukiwa pale tuliomba kuonyeswa kwa dirisha la wazee lakini tulijibiwa kuwa tuchukue namba hapo mapokezi na Kuwa watu wote na umri wowote ule wanachukua namba hapo mapokezi kwa ajili ya kuwahi /kuweka foleni.
Baada ya kuchukua namba na baada ya Kukaa kwa Muda wa Kama lisaa limoja na zaidi namba yake ilifika akaitwa kufika pale alipoitwa ambapo bado ni eneo la mapokezi rafiki yangu alipewa control namba ya kwenda kulipia faili na alipohoji kuwa mbona tunaambiwa Hospital za serikali wazee ni bure?
Alijibiwa kuwa hiyo huduma za. Bure kwa wazee ni kwa ajili ya hospitali za wilaya lakini Hospital za mkoa kila. Kitu ni kulipia hadi kufungua faili la. Kumuona daktari ambapo ni sh. Elf kumi.
Basi bila hiana rafiki yangu akatoa hela ya faili ikafuatiwa na hela ya vipimo na mlolongo mwingine kama kawaida hadi mwisho wa vipimo na kote alikuwa akilipia kama ilivotakiwa na tukasahau habari yenye kauli mbiu kuwa wazee ni bure.
Tukiwa pale hospitalini tuliona ni jinsi gani wazee wakilalamika gharama kubwa za matibabu ambazo wengi wao wanashindwa kuzimudu kutokana na. Hali halisi ya maisha na aina ya magonjwa yanawayowasumbua.
Ushauri wangu kwa serikali kwa kupitia wizara ya afya ni kuwa pale inapooamua kufanya jambo basi wahakikishe linatimia na iwe ni kweli kulingana na kauli mbiu yao na sio Hospital za Chini ndio huduma bure na. Zile Za juu kama Hospital za rufaa nk. Ambapo ndiko kwenye madaktari bingwa na hususani magonjwa sugu ya wazee na ambapo idadi kuwa ya wazee huelekea huko kuwa ni za malipo.