Uchaguzi 2020 Kundi la WhatsApp lachukua sura mpya baada ya Tundu Lissu kutangazwa Mgombea Urais CHADEMA

Graduates hawana ajira,hali ngumu,democracy,human rights,watumishi wa umma hakuna nyongeza kwa miaka mitano,uhuru wa mahakama,
Niendelee ?
MJIFUNZE SIO KILA GRADUATES AAJIRIWE HIZO MYUMBA ZENU ZINGEKUWA OFISI ZA SERIKALI NDIO MAANA MNAMDA MCHAFU KUDANGANYA WATU MPATE POSHO KWENYE UCHAGUZI KWIKWIKWIO
PAMBANENI NA HALI ZENU
WALIOWAPA MDOMO NDIO WAAWAPA CHAKULA
 
Nipo kwenye group la graduates mwaka fulani wa nyuma, ambao tulinufaika na Loan board kipindi cha Kikwete, na ajira ya Kwanza(first appointment) tukiwa na Kikwete. Tunakumbushana mengi tu hasa Neema za kipindi hicho cha nyuma.

Wadau wengi wa kundini walitia Nia kupitia chama tawala(sikuona chama pinzani aliyepost kundini ingawa walikuwepo, nawafahamu) picha za kijani zilijaa kwenye devices zetu, hadi watu wakafikia hatua kushauri tuwachangie fedha za kuchukulia fomu, ingawa hoja hiyo ilipotea hewani na wengine waliishia kuleft. Wakati huo watu wenye itikadi tofauti na chama cha kijani walionekana kuwa wachache sana.
Hivi sasa napata picha kuwa kumbe wale walioleft hawakuwa na 'Political tolerance' tuliobaki active kwenye agenda za kisiasa nadhani ni mimi na wenzangu Kama wanne hivi Kati ya wanagroup zaidi ya 300.

Aisee watu ni waoga ati! Lile group limebadili gia angani tangu kutangazwa kwa TL kuwa Mgombea Urais CHADEMA. Wanakijani wanahesabika Kama wakivyohesabika wa rangi nyingine hapo awali. Picha ya Tz yetu kwa sasa nimeipata kupitia grupu langu la wasap. Grupu lina wasomi na maafisa wengi tu walioendelea na masomo hadi PhD. Tulikuwa tunaogopana lakini tangu 3/8/2020 woga umeisha.

Utawala huu umeniadhibu mambo kadhaa makubwa ambayo sitokuja kusahau maishani. Nadhani tupo wengi nyuma ya haya na mengine.

1.Baba yangu kastaafu tangu October 2017, yapata miaka miwili na nusu hajapata mafao yake hadi leo. Amehangaika, akapatwa na stroke ingawa alikuwa na historia ya BP ila nadhani hili limechangia. Ameparalaizi kwa sasa.

2. Mimi na mdogo wangu tulipata ajira ya ualimu wa sekondari 2009 na 2011. Serikali ikatupeleka kufundisha shule za msingi mwaka 2018. Si vibaya kufundisha msingi lakini iliniuma kuona wenye degree tunapelekwa msingi na wenye diploma wanabaki secondary Schools. Bila kujali seniority kazini(umri kazini) yaani miaka yangu 9 kazini unanipeleka kwenye kazi ambayo sikuisomea na Wala kuifikiria halafu unamwacha dogo wa diploma mwenye miaka 5 kazini. No!! Huu siyo utumishi wa umma.

3. Uhakiki wa vyeti feki ulinifurahisha Sana, niligundua walimu wengi wana vyeti zaidi ya kimoja, yaani waliunga unga elimu(wali resit) na wengine walisomea majina tofauti ili warudie darasa. Cha kushangaza hao hao waliachwa wafundishe sekondari sisi wenye division one(na umahiri katika masomo) tukapelekwa shule za msingi, kisa tunamchalenji hedimasta. Kuna shule ambazo wanafunzi waliandamana kupinga uhamisho onevu wa competent teachers mwaka 2018, waliopelekwa msingi.

Niliacha kazi ya serikali nikaenda private school, na baadae kwenye biashara za mazao hadi leo hii. Naiona Tanzania yenye HAKI na Usawa mbeleni kama Uongozi utageuka upande wa pili, Binafsi natamani hivyo na dalili naoina.
Time will tell!!
Ulipoandika ni kundi la graduates, nikaelewa una digrii fulani, lakini niliposoma unavyoandika na kupangilia maneno, sioni usomi wako. Bado unadai ulistahili ukafundishe sekondari badara ya msingi, kwa elimu ipi?
Tulikimbilie kutanja digrii na diploma tu, tuangalie na uelewa wetu. Elimu siyo vyeti ni ufahamu wetu.
 
Lazia. Utangoja sana utawala huu ubadilike na hiyo haki unayoitaka haitakuwepo. Utakuwa frustrated. Nakuhakikishia hilo halitakaa litokee. Fanya kazi jenga maisha yako. Usitegemee CHADEMA ibadili mambo, haiwezi. Tundu hawezi kuwa raisi. Hilo halitotokea. Haitasimama bendera tofauti na ya kijani kwenye uraisi mpaka unazeeka.
 
Wewe kama bibi na babu yako wamelipwa haina tafsiri kwamba "wote" wamelipwa, hii habari ya watu kitokulipwa mafao yao ni dhahiri kabisa, nina mzee wangu alistaafu tangu August,2018 mpaka leo bado hajapewa haki yake!

Ukweli ni kwamba mzee Magu ana roho ya kikatili, achilia mbali wazee hao (ambao hawajalipwa), najaribu kumtazama namna anavyodhulumu haki za watumishi wa umma kwa sasa!

Kwa miaka 5 ameikanyaga sheria ya utumishi wa umma, kwani kutowaongezea basic salary maana yake hakuna nyongeza yoyote kwenye mchango wa mfuko wa hifadhi ya jamii (kwa miaka yote ya uongozi wake)

Wakati huo huo Kuna sheria ipo "pending" ya kulazimisha wastaafu kuchukua 25% ya mafao yao kwa kisingizio cha "kuwatunzia" wastaafu pesa zao wakati wao (viongozi Magu akiwemo) kwa miaka yote wamekuwa wakijikwapkulia pesa zao zote kila baada ya miaka mitano utadhani wao hawazeeki (high level of selfishness)

Huyu mzee ni katili mnoooooo!
Yaani hawa watu wanaobeza hivi sijui Wana roho gani. Just imagine baba kastaafu hiyo October 2017, huu ni mwaka wa pili na kidogo, ameparalaizi upande mmoja mkono na mguu. Kwasasa anahudhuria clinic ya BP na mazoezi (physiotherapy) kwa mwezi mara moja, na bado hajapata mafao yake.
Mkuu wa nchi anagawa hela yu kwenye ziara zake huku mzee wangu aliyetumikia umma kwa mda wote huo hajalipwa hata shilingi Mia.
 
Usiwasemee watu. Kaka yangu alistaafu tangu August 2016 bahati mbaya akafariki February 2017. Tulifuatilia mafao for 3 years yamelipwa June 2020. Usitutie hasira watu tulioathirika na hii system kenge wewe!!!!
Watu wanatetea ujinga humu, hawajui mateso wanayopitia wastaafu. Huruma Sana.
 
Ulipoandika ni kundi la graduates, nikaelewa una digrii fulani, lakini niliposoma unavyoandika na kupangilia maneno, sioni usomi wako. Bado unadai ulistahili ukafundishe sekondari badara ya msingi, kwa elimu ipi?
Tulikimbilie kutanja digrii na diploma tu, tuangalie na uelewa wetu. Elimu siyo vyeti ni ufahamu wetu.

Badara#Badala
Tulikimbilie#Tusikimbilie
Kutanja#kutaja

Hata kiswahili hukijui, mfyuuuu!
 
Yaani Lissu wakijipanga kumalizana nae ni swala jepesi sana anadai Magufuli katoa rushwa na ushahidi anao na CDM wanashangilia.

Hivi Magufuli kaanza kutoa hela barabarani jana au kuchangisha watu kwa sababu ya shule, amekuwa akifanya ivyo karibu katika kipindi chote cha miaka mitano na bado muda wake kama raisi aujakoma.

Sasa utaitaje rushwa alichofanya Kibiti kitu ambacho amekuwa akikifanya kilasiku anaposimama kuongea na wananchi tena Lissu anajitapa huo ndio ushahidi wake.

This guy is a joke hoja zake ni nyepesi mno, anavyoongea utadhani yeye na raisi wa nchi wana mamlaka sawa sawa wakati ata form za kugombea uraisi azijatolewa bado.

Hivi kuna kesi gani kubwa ambayo Lissu amewahi kushinda? Anyone.
 
Mpewe loan
Mpewe na AJIRA
Si mtaomba mpewe na wake kabisa
Graduates hawana ajira,hali ngumu,democracy,human rights,watumishi wa umma hakuna nyongeza kwa miaka mitano,uhuru wa mahakama,
Niendelee ?
 
Usijibishane nao wala usijifananishe Naoo haya n maandiko
Yaani Lissu wakijipanga kumalizana nae ni swala jepesi sana anadai Magufuli katoa rushwa na ushahidi anao na CDM wanashangilia.

Hivi Magufuli kaanza kutoa hela barabarani jana au kuchangisha watu kwa sababu ya shule, amekuwa akifanya ivyo karibu katika kipindi chote cha miaka mitano na bado muda wake kama raisi aujakoma.

Sasa utaitaje rushwa alichofanya Kibiti kitu ambacho amekuwa akikifanya kilasiku anaposimama kuongea na wananchi tena Lissu anajitapa huo ndio ushahidi wake.

This guy is a joke hoja zake ni nyepesi mno. Hivi kuna kesi gani kubwa ambayo Lissu amewahi kushinda? Anyone.
 
Huu ndio muda ambao ccm watashangaa maana hawataamini kura watakazopewa na wananchi...wengi wana hasira kuanzia familia za waliotumbuliwa kwa uonevu
Mbona waliyotumbuliwa wengi tu wamegombea udiwani na ubunge kupitia ccm?
 
Back
Top Bottom