Kundi la Wanafiki laibuka kutaka Ole Sabaya aonewe huruma

Mahakama ikishatoa hukumu, mtu pekee anayeweza kutoa msamaha ni Rais mbali ya rufaa.
 
Baada ya jambazi Lengai Ole Sabaya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, limejitokeza kundi la WANAFIKI wanaotaka Sabaya aonewe huruma.

Lakini ni watu haohao walikaa kimya Sabaya alipovunja miguu vijana wa Chadema kule Hai. Ni watu haohao waliokaa kimya Sabaya alipomkata sikio mtoto wa diwani wa Narumu. Ni watu haohao waliokaa kimya Sabaya alipovamia hoteli ya Weruweru na kutaka aoneshwe chumba alicholala Nandy. Leo wanataka Sabaya aonewe huruma. Unafiki ni mbaya sana.

Sabaya alipovamia nyumba ya Nicodemus Mbowe akiwa na genge lake, akatembeza kipigo nyumba nzima, baba akavunjwa mguu, mtoto akakatwa sikio, na mama akatenguliwa nyonga hawa wanafiki walikua wapi? NIcodemus alilalamika lakini hakuna anayemsikiliza. Aliripoti polisi lakini kesi yake ikatupwa. Ukabaki kumlilia Mungu.

Mtu yuleyule aliyesababisha ulemavu kwa familia nzima (baba kavunjwa mguu, mtoto kakatwa sikio, mama katenguliwa nyonga) anahukumiwa kifungo, halafu wanajitokeza watu kumuonea huruma. Lakini watu hao hawakumuonea huruma Nicodemus wakati ukifanyiwa unyama huo. Hiki ni kiwango kikubwa sana cha unafiki.

Mtu anasimama hadharani na meno 32 yaliyooza, anaropoka eti usifurahie matatizo ya Sabaya. Huyo Sabaya alipopiga watu, alipotesa watu, alipoharibu biashara za watu mbona mlikaa kimya? Ina maana mlifurahia sio?

Mlifurahia Nandy kuvamiwa hotelini? Mlifurahia mzee Eliot Lyimo kuporwa 25M? Mlifurahia dada zetu kudhalilishwa kingono na genge la Sabaya? Mlifurahia Cuthbert Swai kufunga biashara zake na kukimbilia Kenya sababu ya Sabaya. Mlifurahia hoteli za kitalii Arusha kujiendesha kwa hasara sababu ya Sabaya kulala bure? Leo mnasema tusifurahie Sabaya kufungwa? Acheni unafiki muende mbinguni.

Eti Mungu hapendi kufurahia matatizo ya mwenzako. Kwahiyo Mungu alipenda watu waonewe, wapigwe, wavunjwe miguu, wakatwe masikio bila hatia? Ni "mungu" gani huyo ambaye anaonekana tu Sabaya akipata matatizo na sio wengine wakipata matatizo? Mungu ninayemuabudu mimi ni Mungu wa haki (Jehovah) ambaye husimama katika haki wakati wote.

Mnajifanya kumuonea huruma Sabaya, je wale waliofanyiwa unyama sio binadamu? Au kwa sababu huyu alikua DC ndio anatakiwa aonewe huruma kuliko wengine? Mnamaanisha raia kufanyiwa unyama si kitu, ila DC kufungwa ndio inawauma? Wajinga nyie.

Ndugu Swai (Katibu wa Chadema Machame) alitumiwa ujumbe na Sabaya akimwambia aache kuitisha vikao vya Chadema kwenye kata yake kwa sababu eti vikao hivyo ni vya kumtukana JPM. Swai akamjibu vikao vitaendelea kwa sababu vipo kwa mujibu wa sheria na hawamtukani JPM bali wanapanga mipango yao ya kichama.

Sabaya akaona jamaa kamdharau. Kilichofuatia ni kutekwa. Kwa siku 3 hakujulikana alipo. Alikuja kuokotwa huko Nduruma Arusha akiwa amepoteza fahamu. Akakimbizwa hospitali Mt.Meru ambapo alitibiwa kwa siku 3 ndipo fahamu zikarudi.

Katika maelezo yake anasema alitekwa na kundi la vijana watano waliokua na gari aina ya Toyota Landcruzer yenye namba za umoja wa mataifa (UN). Alifungwa kitambaa cheusi na kupelekwa mahali asipopajua. Alipofika alifunguliwa kitambaa na akamuona Sabaya mbele yake amevaa miwani nyeusi. Sabaya akamdhihaki na kumwambia "ulisema unaye Mungu, sasa leo utamuita aje kukusaidia"

Kilichofuatia ni kipigo kikali cha marungu, mateke, vitako vya bunduki na kuwekewa short ya umeme. Alilia sana akiomba Sabaya amsamehe lakini mateso yaliendelea hadi akapoteza fahamu. Hakujua kilichoendelea hadi alipookotwa huko mto Nduruma na kukimbizwa hospitali.

Alipotoka alifungua jalada la uchunguzi kituo cha polisi Bomang'ombe na kueleza waziwazi kuwa alivamiwa na Sabaya na genge lake. Lakini hakuna aliyejali. OCD gani anathubutu kumuita DC na kumhoji? Kesi ikapotezewa.

Swai akaita waandishi wa habari na kueleza kisa kamili lakini hakuna aliyejali. Halafu leo watu wanapanua pua zenye makamasi kupayaka eti usifurahie mateso ya Sabaya. Mlikua wapi wakati hao wengine wakiteseka?

Mimi ni mhanga wa Sabaya, niliyeponea chupuchupu kuingia mikononi mwake mara mbili. Mara ya kwanza alipomwambia binamu yangu (ambaye ni rafiki yake) anipigie simu bila kuniambia yupo na Sabaya, ili nikienda anikamate. Ndugu yangu huyo akagoma kufanya hivyo. Sabaya akamgeuzia kibao kwa kumpiga na kumuweka rumande kituo cha polisi Bomang''ombe. Urafiki wao ukafa. Hata baada ya kutoka polisi hakurudishiwa simu zake hadi leo.

Mara ya pili ni alipovamia kwenye eneo moja tulilokua mimi na Don J Mbowe akitutafuta na baada ya kutukosa akapiga fisasi hewani, bila kujali eneo hilo ni sehemu ya starehe na anaharibu biashara ya watu. Alilazimisha aonwshwe tulipo akiamini tumejifucha. Akaambiwa wameshaondoka lakini hakuamini. Yeye na genge lake wakatusaka kuanzia jikoni, counter hadi chooni. Hatukuwepo. Akalazimisha baadhi ya magari yafunguliwe, hakutupata. Kwa hasira akapiga risasi kadhaa hewani na kuondoka.

Nilieleza matukio yote hapa. Hawa wanafiki wanaotaka tumuonee huruma Sabaya leo, hawakujaribu hata kumuonya, instead leo wanataka tumuonee huruma. Idiots.!

Jeff wa Speshoz alinyanyaswa kwenye kiwanda chake cha uzalishaji wa pombe kali pale Hai. Akawekwa hadi mahabusu bila hatia, kisa Sabaya alitaka kiwanda hicho kimpe "mamilioni ya pesa" kwa ajili ya Mwenge. Hivi nyie mmewahi kumpa Jeff pole ya kinafiki kwa yaliyompata, au yeye hatakiwi kuonewa huruma? Anayetakiwa kuonewa huruma ni Sabaya tu.

Kuna wanawake wanaodai kulazimishwa ngono kwa nguvu na wengine kulawitiwa na genge la Sabaya. Wengine ni wake za watu. Sabaya akikukuta na "pisi kali" unapigwa halafu mpenzi wako anachukuliwa na kwenda kufanyiwa vitendo vya kinyama. Sasa jiulize kabla hujapayuka kuwa Sabaya aonewe huruma, jiulize ingekua mkeo, mwanao au mama yako amelawitiwa na genge la Sabaya ungekua na nguvu za kusema aonewe huruma? Hivi mnajua maumivu wanayopitia watu kabla hamjaomba huruma zao?

Mnaotaka Sabaya aonewe huruma, mnafanya makosa yafuatayo;

1. Mnataka kujenga matabaka, kwamba wanaotakiwa kuonewa huruma ni viongozi tu na sio raia. Ujinga.

2. Mnataka kuwapa kinga viongozi kwamba wanaweza kuwafanya raia chochote, na ikitokea wameshtakiwa basi nchi iwaonee huruma. Upuuzi.

3. Mnataka ionekane kama Sabaya alionewa au alisingiziwa makosa yake, wakati ushahidi wa wazi upo hadi wa CCTV. Wehu.!

4. Mnataka kumuondoa Sabaya kwenye lawama ionekane alikua anatekeleza maagizo ya mwendazake. Upumbavu.!

5. Moyoni mnajua Sabaya alikosea lakini mnamtetea kwa sababu tu alikua mwanaCCM mwenzenu, au DC mwenzenu, au alumni mwenzenu chuoni. Upoyoyo.

Action points kwa viongozi mliopo madarakani sasa;

1. Tenda haki kwa wote. Usitumie madaraka yako kuumiza watu, kutesa watu au kuonea watu bila hatia. Ipo siku utalipa, kama si hapa basi mbinguni.

2. Usikubali kutumika na "mamlaka za juu" kunyanyasa watu bila hatia. Mamalaka za juu zina kinga, lakini wewe huna kinga. Za kuambiwa changanya na zako.

3. Siasa si uadui ni utofauti tu wa mawazo. Usimchukie mtu kwa sababu ya siasa. Vyama visiwe msingi wa kunyanyasana bila sababu. Waliotuletea hivi vyama hawafanyiani unyama kama tunaofanyiana sisi. Wanatushangaa.

4. Unaweza kuwa na wapambe wengi ukiwa na madaraka, lakini mambo yakikugeuka utajikuta peke yako. Sabaya alikua na wapambe hadi wa kumbebea glass akiwa club. Mmoja kabeba glass ya Henessy, mwingine glass ya red wine. Anachukua moja anakunywa anamrudishia mpambe abebe. Aliishi kama peponi. Lakini leo yupo peke yake Kisongo, akisubiri kupangiwa kazi ngumu na nyapara kuanzia kesho.

5. Usinyanyase watu kwa sababu kuna "godfather" anakulinda. Ni dhambi kubwa kuishi kwa kumtegemea mtu. Mtegemee Mungu pekee. Ishi na watu vizuri sponsor hufariki.

6. Ukiona mwenzako amekosea muonye ajirekebishe. Usipomuonya it means na wewe umeshiriki katika makosa yake. Marafiki wa Sabaya mnaotaka aonewe huruma leo, je wakati ananyanyasa watu mlitumia urafiki wenu kumuonya? Au mlimsifia kinafiki huku mkijua anaumiza watu, halafu leo mnataka aonewe huruma.

7. Ishi na watu vizuri, siku ukipata tatizo watakukimbilia kukufariji. Lakini usinyanyase watu halafu ukipata tatizo uanze kutafuta huruma. Wahenga walisema mwenda tezi na omo marejeo ngamani.!

8. Kilichotokea kwa Sabaya sio jambo jipya. Mfalme Herode (aliyemkata kichwa Yohana mbatizaji) alipokufa nchi yote ya Israel ilipaza sauti za shangwe na kumtukuza Mungu. Kwahiyo ukitaka watu wasifurahie matatizo yako ishi nao vizuri. Siku ukiomboleza wataomboleza na wewe, siku ukifurahi watafurahi na wewe. Lakini unanyanayasa watu, unateka watu, unavunja watu miguu, halafu unataka watu haohao waomboleze na wewe ukiwa kwenye dhiki? Never.!

9. Kila unachokifanya kifanyie kwanza tathmini, usijifanyie tu. Pima faida na hasara zake kwanza. Socrates aliwahi kusema maisha yasiyo na tathmini ni maisha yasiyofaa kuishi "unexamined life is not worth living"

10. Unaweza kutumia cheo chako kunyanyasa watu, ukawapakazia kesi za ugaidi na kesi nyinginezo. Pengine kwa sababu una kinga ya kutoshtakiwa ukadhani hakuna wa kukufanya kitu. Lakini amin, amin nakuambia MUNGU YUPO KAZINI. Machozi ya watu yakizidi, yeye atafanya.!

Malisa GJ
Tunasubiria hukumu ya mkuu wa magaidi. Halafu watakatifu wa watakatifu tuone watakavyoipokea
 
Wanaweza kumfunga lakini hakuna ushahidi. Huwezi ukamkamata gaidi kisha ukamnunulia chakula gaidi na kukaa naye meza moja kula huku akiwa hana pingu.

Tunasubiria hukumu ya mkuu wa magaidi. Halafu watakatifu wa watakatifu tuone watakavyoipokea
 
The more i read story za huyu sabaya naanza kuelewa kwa nini watu wengi wamefurahia sana kufungwa kwake , na nimeona clip moja lema akimuonya kwenye simu aache kuumiza watu kwa kujipendekeza, seems kadhulumu sana, kaua biashara za watu,kaumiza upinzani na inawezekana kaua watu huyu achunguzwe zaidi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Anatakiwa alawitiwe huyu mshenzi mpk nnya iwe inadondoka yenyewe tu.Jinga Sana lile lofa.
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Sabaya ni scapegoat
Amesema mahakamani kuwa alisapotiwa na waziri wa fedha wa kipindi (ambaye nadhani ni Mpango),na viongozi wa juu ambao nashawishika kuamini na huyu rais ni mmojawao.
Kumfunga ni kumnyamazisha
Najua jamaa ni katili na anastahili kuwa huko lakini tuijadili chain nzima ya juu iliyomtuma.Wengine hawajafa,wapo kwenye ofisi kubwa.
Ccm hawanaga utamaduni wa kuwawajibisha waovu isipokuwa wanapotaka kuficha kitu.
Hakika hii sio ccm ya Nyerere amini nawaambia.
Gharika na moto agano limekataa sijui ni nini kingefaa. Wema watataokokaje? Hebu kila aliyepata cheo huko ajiohoji kama alichokipata ni halali.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa calibre ya jiwe naamini ni kweli alimtuma
But kutumiwa kufanya uovu hakukufanyi kuwa innocent
Nimeandika kuwa anastahili kuwa huko lakini sio peke yake,Mpango,SSH hawahusiki kwenye kumtuma huyu?
Naona ni kama kumsilence
And am afraid atatolewa soon
Afrika Nafasi ya usaidizi katika dola haikupi nafasi ya kumpinga bosi wako hata tu kwa kujiuzulu. Hatuwezi kuwahukumu kwa nafasi hizo na hii inathibitishwa na baada ya bosi kuondoka.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
New look
IMG-20211018-WA0000.jpg
 
Yaa nikweli kabisa,tumeshafunga ukurasa wake sasa,hukumu tayari.
Ni mda wa kusubiri kesi ya Ugaidi,tuone mwisho wake. Baada ya hukumu ya Ugaidi tutarudi hapa tena kuwatafuta wanaounga mkono na wanaopinga.
 
Huyu anayemtetea SABAYA atakuwa makonda au Hapi, haiwezekani huyo mpumbavu aliyejiona mungu wa dunia hii,sabaya hakutenda haki,miaka 30 haikutosha,huyu alipaswa kuuwa na akipunguziwa adhabu afungwe maisha.
 
Mwendazake aliteua majambazi kuwa viongozi katika utawala wake halafu kuna baadhi ya watu bado wanaamini kwamba jamaa alikua shujaa wa Afrika.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom