Kundi la vijana ni silaha kubwa ya mageuzi vizazi vijavyo hapa nchini Tanzania

Kijana ushe2

Senior Member
Apr 6, 2017
176
122
Ndugu wanajamvi leo nataka nigusie kuhusu wimbi letu la vijana wa hili taifa la Tanzania:

Moja, vijana tupambane katika kutafuta riziki ya kila siku vijana tujikubali na tuweze kuuachia ubongo uweze kutafsiri vyema namna ya kupambana na maisha ya kawaida ya kila sikh na so kutegemea mtu ama viongozi.

Pili, kwenye kazi tufanye kwa weledi bila ubaguzi na majivuni vijana kama vijana tunapaswa tufanye kazi bila hurka ya kwamba mm nimepata wengine sio bora hapana wewe umepata kwa kuwa ni zamu yako itumie vyema maaana ikienda hiyo nafasi hautafanikiwa na utafanya wengine wasiaminiwe kwasababu yako binafsi.

Tatu, vijana wa viongozi ndio haohao wanaoaminiwa na serikali na so viongozi kwa sababu ni kiongozi, hii ipo kote duniani lakini luna sehemu kwa nchi yetu kijana akiwa karibu na serikali ndio atapata haya kama uwezo wake ni mdogo mno inaumiza na inasikitisha sana.

Nne, vijana tujikite zaidi katika biashara na kilimo kwa ustadi na hali ya juu huku tukipenda kusaidizane kulingana na mazingira.

Mwalimu wa wanafunzi wenye adabu!
 
Ila wasiwe type ya sabaya, bashite,hapi.
Uongozi ni hekima na hekima ni malezi bora
 
ccm walishachelewa kuwatengeneza hata wkiwapata hawawezi kuwa wazuri kwa taifa
 
^Haiwezekani kamwe katu kuleta mabadiliko wala mageuzi wala maendeleo yoyote yenye maana na hilimivu (sustainable development) kwenye taifa ambamo asilimia kubwa ya vijana wake ambao ndio kundi kubwa na lenye nguvu zaidi wamewekeza utashi, fikra, juhudi, nguvu zao katika starehe, ngono, pombe na ulafi wa pesa^ ~ Che Guevara
 
Hii ni fursa muhimu sana ambayo imewekwa mikononi mwa vijana ili kuweza kuthibisha ya kwamba wakiaminiwa kushika nafasi nyeti za uongozi wa nchi hii, nao pia wanaweza kufanya mambo makubwa kinyume na yale ya mazoea ya viongozi wazee waliopita.

Ni vyema wakatenda na kuleta maendeleo na mabadiliko chanya na endelevu ya kiuchumi na kijamii, yaani "paradigm shift" yenye uwezo wa kuthibika na kuonekana.

Hatutegemei wakageuka kuwa dodoki la kusafisha mapungufu yaliyopo serikalini, bali wawe chachu ya fikra pevu na mpya katika kutetea ukweli na kwa kuuishi ili nchi hii ipate kuendelea. Watoke nje ya kasha ili kuifanya nchi yetu kuwa sehemu bora ya kuishi kwa makundi yote ya watu pasipo kujali milengo yao ya kidini, kisiasa na kiutamaduni.
 
Back
Top Bottom