Kundi la Samia litafanikiwa Kati ya Katiba na Tume huru kipi kianze

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
Na Yhabiti Kombo


Mm kwa mtazamo wangu kwa sasa kumekuwa na makundi manne!

Na kila kundi linafanikiwa kwa namna yake!

Lkn ktk mafanikio hayo!

Kuna kundi litafanikiwa na kunufaika zaidi,nalo ni kundi la :

SAMIA SULUHU.

Makundi hayo ni :

1)CDM

2)SAMIA SULUHU

3)ACT

4)NCCR

Ktk makundi haya ukiyapima kila kundi lina hoja za msingi!

Na ktk kufanikisha dhamira za makundi haya ni muhimu makundi haya matatu yakaunganisha nguvu au yakaridhiana baadhi ya mambo,ili yaweze kukabiliana na kundi moja la SAMIA SULUHU.

Nayo ni :

1)CDM
2)ACT
3)NCCR

Kwakuwa makundi haya ambayo yana uhitaji unaofanana lkn tofauti yao ni,
1)kutoaminiana
2)kushutumiana
3)kuogopana
4)kufanyiana khiyana
5)na kipi kianze kati ya tume huru na katiba mpya.

Basi ni muhimu kukaa chini na kutafakari juu ya kuyaendea haya ili mafanikio yapatikane.

Vinginevyo mahitaji ya makundi haya hayatafanikiwa kwa sababu kundi la :

SAMIA SULUHU

ndio kundi linalotusikiliza mahitaji yetu na ndio kundi linaloamua litaanza na nini,na mbaya zaidi tayari limeshaweka tahadhari zake kuwa kwanza nendeni mkaelewane kisha mje na mambo mliyoridhiana ndio yafanyiwe kazi!

Ikumbukwe kwa sasa hakuna chama kilichowekeza vya kutosha kuweza kutumia nguvu ya umma!

Hivyo utashi na maamuzi ya SAMIA SULUHU ndio yanategemewa kufanyika!

Kwa kuwa maneno ya SAMIA SULUHU yameonyesha anayataka makundi mengine yaridhiane ktk mambo mbalimbali ndio na yeye aweze kuchukua hatua,na kwa kuwa haya makundi matatu bado hayajafikia kukubaliana na kushikamana!

Basi tutegemee SAMIA SULUHU ataupiga mwingi zaidi ya hapa kwa sababu akirudi kwa wananchi ataonyesha kuwa makundi hayo makubwa matatu yalishindwa yenyewe kujipanga na kuonyesha uhitaji wa pamoja juu ya mahitaji ya wananchi!

Tutegemee ushindi wa SAMIA SULUHU utapatikana kutoka kwa CDM,NCCR na ACT.

umuhimu wa kuunganisha nguvu na kuridhiana ni vema likawa hitaji la vyama vyote na si hitaji la vyama kadhaa tu!

Kuutamani au kuung'ang'ania ukubwa usio na dola ni ukubwa wa mbuyu ulio na tundu katikati!

Vyama vyote vinatakiwa kutamani kushika dola kwa kuanzia na uwakilishi wa serikali za mitaa,udiwani na ubunge!

Hii ndio dhana ya kufanikiwa ktk haya mapambano!

Na mafanikio hayo yataletwa na vyama hivi kushirikiana!

Mashirikiano ya vyama hivi yatachagizwa na wananchinpamoja na wagombea wenye dhamira ya kushinda ktk chaguzi zijazo!

Naamini ktk kutofautiana mitazamo lkn naamini kukubaliana ktk mashirikiano inawezekana!!
 
Matatizo ya upinzani ni hayo uliyoyasema

1)kutoaminiana
2)kushutumiana
3)kuogopana
4)kufanyiana khiyana
Nalog off Z
 
Back
Top Bottom