Kundi la Mwigulu linajipanga Uchaguzi mwaka 2025. Mwigulu anatumia nafasi hii Kushusha Umaarufu wa Rais Samia

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
3,280
2,000
Anachofanya Mwigulu si kwa bahati mbaya. Anajua vizuri sana na anatumia mbinu ya kumchonganisha Samia na wananchi huku akijipanga kuja gombea Uchaguzi wa mwaka 2025/2030. Hafanyi kwa bahati mbaya.

Hizi tozo mpya anajua anachofanya. Anamshusha Rais Samia huku yeye akijiwekea mazingira ya kupata pesa uchaguzi ujao. Ameanza kujipanga kwa muda mrefu sana. Na hajaacha.

Rais Samia kuwa makini na Mwigulu Nchemba.
 
EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,884
2,000
Mkuu unajua process za kutunga sheria??

Hadi mswada unafikishwa Bungeni unajua unapitia hatua zipi??

Mwigulu peke yake hawezi kumkwamisha hasa kwa hili la tozo.

CCM wametengeneza tatizo halafu wakajificha kusikilizia "reaction" walipoona moto hao hao wanalitatua then wanajibebea credits
 
ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
14,802
2,000
Masikini akipata

IMG-20210718-WA0139.jpg
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
12,824
2,000
Huyu mtu sio mtu wa mama SSH kumwamini hata kdg na ni mtu wa kujikomba sana kwa maslahi yake binafsi.
Kama bado ana ndoto za Uraisi hafai kabisa ashukuru Mungu kuwa ni mbunge wa huko singida angekuwa anatoka ktk Mikoa inayojitambua hata Udiwani asingepata! Historia yake alipokuwa mambo ya ndani imejaa makandokando mengi sana.
 
Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
3,540
2,000
Nimegundua kuwa magufuli haikuwa muongo wakati ule anasema "watanzania wengi ni wanyonge", ingawa wengi wa vijana wa Ufipa walilikataa ila kupitia hizi tozo unadhani wengi wao wameitambua nafasi yao kwenye Taifa kama hili .
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,314
2,000
Hivi nani kaloga middle class wa kitanzania?mbona kama vichwa vyao vimejaa funza?maana ufikiri wao ni bora umsikilinze mndendeule wa hapa Lingusenguse,huu mswada umepita ngazi zote hadi kupitishwa including ofisi ya Rais,huwezi sasa baada ya kuona ume backfire unamtwisha mzigo wote huu our Finance Minister hii sio sahihi kabisa,hapa ni Bunge na President kuonyesha the way forward sio kujifanya eti now atauangalia upya hii ni rubbish,lini tutaanza ku take responsibility ya maamuzi yetu?na kutuletea hapa upuuzi huu kuwa Mr.Mwigulu anajipanga kwa mbio za Urais hii nayo ni fake news,toka lini mtoa mada umeshageuka kuwa Sangoma?
 
beijing_07

Senior Member
Jul 19, 2021
114
250
kuna siku watanzania wakapoamua kujitoa ufaham juu ya hawa wanasiasa ndio tutaelewana vzuri
 
Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,386
2,000
Anachofanya Mwigulu si kwa bahati mbaya. Anajua vizuri sana. Na anatumia mbinu ya kumchonganisha Samia na wananchi huku akijipanga kuja gombea Uchaguzi wa mwaka 2025/2030. Hafanyi kwa bahati mbaya.

Hizi tozo mpya anajua anachofanya. Anamshusha Rais Samia huku yeye akijiwekea mazingira ya kupata pesa uchaguzi ujao. Ameanza kujipanga kwa muda mrefu sana. Na hajaacha.

Rais Samia kuwa makini na Mwigulu Nchemba.
Upo Sahihi SUKUMA GANG utadhani haipo kumbe imetulia KIMKAKATI KuleTwitter kuna Kundi linajiita MPP na lina Nembo hii kazi yao Kumchafua MAMA
Screenshot_20210704-161108_Twitter.jpg

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
2,027
2,000
Mkuu unajua process za kutunga sheria??

Hadi mswada unafikishwa Bungeni unajua unapitia hatua zipi??

Mwigulu peke yake hawezi kumkwamisha hasa kwa hili la tozo.

CCM wametengeneza tatizo halafu wakajificha kusikilizia "reaction" walipoona moto hao hao wanalitatua then wanajibebea credits
Hii ni mbinu kongwe au ni mbinu mpya?
 
Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
3,280
2,000
Hivi nani kaloga middle class wa kitanzania?mbona kama vichwa vyao vimejaa funza?maana ufikiri wao ni bora umsikilinze mndendeule wa hapa Lingusenguse,huu mswada umepita ngazi zote hadi kupitishwa including ofisi ya Rais,huwezi sasa baada ya kuona ume backfire unamtwisha mzigo wote huu our Finance Minister hii sio sahihi kabisa,hapa ni Bunge na President kuonyesha the way forward sio kujifanya eti now atauangalia upya hii ni rubbish,lini tutaanza ku take responsibility ya maamuzi yetu?na kutuletea hapa upuuzi huu kuwa Mr.Mwigulu anajipanga kwa mbio za Urais hii nayo ni fake news,toka lini mtoa mada umeshageuka kuwa Sangoma?
Tulia dada usipanic hivyo... Haya mambo hayataki hasira. Kwa hiyo unataka kusema kosa ni la Rais?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom