Kundi la Masha lageuza zengwe la ID kwa kundi la Membe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kundi la Masha lageuza zengwe la ID kwa kundi la Membe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by omarilyas, Feb 4, 2009.

 1. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa nimezipata kuwa lile zengwe la kuingilia taratibu za tenda ya kuendesha mradi wa vitambulisho nchini limekuwa zaidi ya ulaji wa Masha. Hivi sasa sakata hilo limegeuzwa kama vita kati ya "akina Masha" Vs "akina Membe"

  Sakata hilo sasa limeelekea bungeni ambako sumu imepenyezwa katika kambi ya upinzani ikidaiwa kuwa ni barua iliyopelekwa kwa Mheshimiwa Pinda kutoka kwa wazalendo serikalini. taarifa niliyonayo ni kuwa kilichofanyika ni kuchukuwa some facts na kuzitwist pamoja na zengwe's na kutengeneza skendo ambalo wanaamini litamwingiza matatani Membe ambaye wameapa kuwa hatafika 2010 kisiasa kama njia ya kumzuia "asimrithi" JK ama 2010 au 2015.

  Hii ni hatari kwani ni wazi sasa MRADI huu muhimu kwa Taifa letu umegeuka kutoka ligi ya nani apate ulaji/ufisadi na kuingia katika siasa za Urais kati ya makundi hasimu ndani ya CCM.

  Ni wazi kuwa wanajua kwamba Pinda katu hataingia mkenge kwani anajua huu mradi kwa undani wake ikiwemo mapambano ya ulaji yaliyokuwepo hivyo wameona ujanja ni kuwapa wazee wa mabomu kuingia bungeni ambako wanadhani ni uwanja muafaka wa mapambano yao yenye maslahi binafsi.

  Sio tu hili linaweza kuderail utekelezaji wa mradi huu na hivyo kuongezeka gharama lakini pia unatumika kuwachanganya zaidi watanzania ili kutoweza kulinda umakini wa kupambana na UFISADI iliothibitika...

  Nawaachia wajuvi waongeze taarifa...

  Tanzanianjema
   
 2. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #2
  Feb 4, 2009
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Membe ni 'nyoka' (shushushu) na ni vigumu sana kumwangusha. Although yeye anausika indirectly kwenye ishu ya ID card lakini sidhani kama wanaweza kumwangusha kisiasa.
   
 3. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ilishaelezwa hapa tangu awali kuwa membe was behind id project na vita kati yake na edo na hata mzee jose jimmy
   
 4. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nyoka hupigwa kichwani
   
 5. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii tabia ya kutupia kila kosa au vitimbi vya mawaziri kuwa ni "wanaandamwa kwa ajili ya vita ya urais" ni kujitukanisha sisi wenyewe kama wananchi tulio huru, na wenye akili timamu.

  Manunuzi ya umma, yana sheria, kanuni na taratibu zake. Sasa kama mtu anapindisha au kukiuka, au kudharau hizo sheria na kanuni, wajibu wetu ni kumbana awajibike kwa kukiuka sheria kwa makusudi au kwa kutojua. Kuwajibika kuko kwa aina nyingi,... na kunaendana na uzito wa kosa.

  Sasa kama mbaya wako au mshindani wako, anacheza ndani ya mipaka ya sheria na kanuni, asianze mtu kulialia eti ni vita binafsi vya urais au kuchafuana. Cha msingi kwetu kama wananchi ni kujua the facts of the matter. Halafu aliyelikoroga alinywe tu bila ya kutizama hizo excuses za kutaka kukwepa responsibility.

  Kama Membe ameharibu, awajibike kwa kuharibu, na kama Masha ameharibu nae awajibike kwa kuharibu. Hii tabia ya watu kuharibu halafu tunakimbilia cheap explanations za "ni vita vya urais" wakati pesa tunayokatwa kwenye PAYE inateketezwa haikubaliki.
   
  Last edited: Feb 5, 2009
 6. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na mkuu SOBER,sioni mantiki ya kuanza kumuingiza Membe kwenye hili.ikumbukwe kwamba mchakato wa ID ulishika kasi sana mara baada ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani na Mh.Membe akiwa Naibu waziri wa mambo ya ndani.Lakini wapo watu na makampuni yaliyokwishaanza kupenyeza rupia toka wakati wa serikali ya awamu ya tatu na waliendelea kuingiza vichwa vyao wakati serikali mpya ilipoingia madarakani lakini hiyo haitoshi kumuingiza Mh.Membe katika kashfa hii kwasababu haijanukuliwa kokote kwamba ali-influence au ameinfluence kwa namna yoyote mchakato wa zabuni. ninavyofahamu mimi ni kwamba evaluation ya technical proposal imekwishafanyika na kampuni ya SAGEM imeondoshwa katika mchakato huo wa awali hivyo kimsingi wametaarifiwa kwamba hawatakuwemo katika mchakato wa pili ambao unahusisha kufunguliwa financial proposal na hatimaye kujumlisha score za technical evaluation na score za financial proposal ili kumpata mshindi atakayepata tenda hiyo kubwa zaidi pengine baada ya Twin towers kumhusisha contractor mmoja.

  Kimsingi ninavyoelewa mimi SAGEM walipeleka malalamiko yao baada ya kutambua kwamba hawawo katika hatua ya pili na hivyo wakapeleka malalamiko yao kwa Mh.Waziri mwenye dhamana ili haki itendeke bila kufahamu kwamba malalamiko yoyote kuhusiana na zabuni yalipaswa kuelekezwa kwa Procurement Appeal Board ambao wangewasaidia. Mh.waziri kwa kutofahamu taratibu na sheria za manunuzi naye akakurupuka kutaka kupata maelezo kwanini SAGEM wameondolewa.

  Inewezakana kabisa mheshimiwa waziri hana maslahi yoyote katika zabuni hiyo lakini namna alivyoingilia mchakato lazima ilete maswali mengi.Mimi binafsi nafikiri Mh.Waziri hakupata ushauri kabla ya kuingilia mchakato huo na ninafikiri anapaswa kusamehewa.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,648
  Trophy Points: 280
  Nimeshasema hapa ukumbini kwamba serikali ya Kikwete ni vurugu tupu!!! Yaani kila kukicha kunakuwa na utata wa aina moja au nyingine. Haya makundi ndani ya serikali yangewezesha kabisa kuishinda kirahisi CCM katika uchaguzi ujao, lakini wapinzani wenyewe wana matatizo makubwa hawaaminiani, wameweka mbele maslahi binafsi badala ya yale ya Taifa pamoja na kupewa ushauri wa bure na Watanzania walio wengi kuhusu umuhimu mkubwa wa kuunda chama kimoja chenye nguvu lakini ushauri huo wameamua kuudharau. Nchi yeyu bado ina safari ndefu sana katika kupata viongozi ambao ni makini na priority yao ya kwanza ni maendeleo ya Tanzania na Watanzania badala yao wenyewe.

  Mungi ibariki Tanzania.
   
  Last edited: Feb 5, 2009
 8. K

  Koba JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...serikali imejaa walafi tuu,nilifikiri baada ya lowassa na baadhi ya mawaziri kujiuzuru ingekuwa ni lesson kubwa sana na wangeogopa kufanya ufisadi wa aina yeyote ule,kama huu sio uwendawazimu ni nini?na kwanini Waziri anakuwa na uwezo wa kuingilia vitu vyenye policy & legal procedural kama hivi? ndio yale yale ya nidhamu ya kuogopana eti mkubwa,na wananchi tulivyoharibika akili tumebaki kushangilia ubabe na kuona hili ni tatizo la kugombea uraisi kuliko ufisadi na kutowajibika kwa viongozi,sitashangaa kuona magazeti yakiandika habari hii kiushabiki na kuichukulia kama kampeni ya siasa badala ya uhujumu!
   
 9. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Sasa umeamini eeh..?

   
Loading...