Kundi la mafia tishio kwa usalama wa watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kundi la mafia tishio kwa usalama wa watoto

Discussion in 'International Forum' started by sulphadoxine, Jul 21, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MUDA uliotolewa na mtekaji nyara raia wa Uganda aliyemteka mtoto, Ibrahim Lawrence(7), akitaka kulipwa Sh3.5 milioni, unamalizika leo huku matumaini ya wazazi kumpata mtoto huyo yakiwa yametoweka.Wananchi wanatupia lawama polisi kuwa wameshindwa kutumia teknolojia ya kisasa kumnasa mtekaji nyara huyo, ikiwamo kufuatilia mawasiliano yake na wazazi ambayo yangeonyesha mahali alipo.

  Tukio hilo ambalo linafananishwa na sinema za Hollywood, ni la pili kutokea mkoani Kilimanjaro kipindi cha mwaka mmoja na yote yakihusisha genge la raia wa Uganda linaloteka nyara watoto.Aprili 18, mwaka jana, mtoto Faraji Haruna (8) naye alitekwa nyara mjini Moshi akitoka shule na kupelekwa Uganda, alirejeshwa nchini baada ya wazazi wake kulipa dola 400 za Marekani.

  Lakini, safari hii tukio la utekaji nyara linamhusisha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere Uganda, Paul Lubega, aliyeomba kufundisha kwa muda shule ya Samaria ya Moshi aliyokuwa anasoma mtoto huyo.Mtoto huyo alitekwa nyara Julai 15, saa 9:30 alasiri na mwalimu huyo ambaye amekwishawapigia simu wazazi wa mtoto huyo, akiwataka wampe kiasi hicho cha fedha ifikapo leo asubuhi vinginevyo atamuua na kuwarejeshea maiti.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma, alisema jitihada za polisi kumtafuta mtoto huyo zinaendelea usiku na mchana na kuomba ushirikiano wa raia wema.

  Kwa mujibu wa Mwakyoma, baada ya kutoweka kwa mtoto huyo, wazazi walipokea simu kutoka namba +254739665740 ambayo ni ya nchini Kenya, ikiwahoji kama wanamfahamu mtoto Ibrahim.“Siku iliyofuata wazazi walipokea simu nyingine kutoka +25675361094 ambayo ni ya Uganda ikihisiwa ni kutoka kwa mshukiwa huyo akitoa masharti ya kulipwa Sh3.5 milioni ili amrejeshe mtoto,” alisema Mwakyoma.

  Kamanda Mwakyoma alitoa tahadhari kwa wazazi na walimu kuwa makini na kutowakabidhi watoto kwa mtu au watu wasiowafahamu, huku akisisitiza watoto wakabidhiwe kwa wazazi wao.

  Babu wa mtoto huyo, Moses Laurence, alisema raia huyo wa Uganda alimpigia tena simu juzi usiku akiulizia kama wazazi hao wamekwishapata fedha hizo akisisitiza asipozipata leo basi watapokea maiti.Uchunguzi wa Mwananchi ambao umethibitishwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Kilimanjaro, unaonyesha mshukiwa huyo aliingia nchini kihalali Julai 6, mwaka huu na kuomba kufundisha Kiswahili shuleni hapo.

   
 2. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  mh hatari namna hii!
   
 3. S

  Simcaesor Senior Member

  #3
  Sep 10, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani hii inaonesha jinsi gani tusivyokuwa makini pia ni namna gani polisi wasivyojua kazi yao...
   
Loading...