Kundi la kijeshi lafanya mapinduzi nchini uturuki

Ubavu

JF-Expert Member
Jun 19, 2012
2,791
3,236
Kundi moja la kijeshi nchini Uturuki linasema limechukua udhibiti wa nchi, huku madaraja jijini Istanbul yakifungwa na ndege za kijeshi zikionekana kupaa katika anga ya Ankara.
Mapema waziri mkuu Binalo Yildirim alitangaza kuwepo kwa “hatua zisizo halali” zilizochukuliwa na “kundi” la kijeshi, na kusisitiza kuwa hakuna mapinduzi ya kijeshi. Alisema serikali bado inadhibiti nchi.
Yanayojiri kuhusu mapinduzi Uturuki
Magari yamezuiwa kuvuka katika madaraja yanayovuka mto Bosphorus jijini Istanbul.
Kumekuwa na taarifa za milio ya risasi katika mji mkuu Ankara, na pia milio ya risasi karibu na ikulu ya rais.
Kumeripotiwa pia mlipuko karibu na makao makuu ya mkuu wa jeshi.
Kituo cha CNN Idhaa ya Uturuki kimeripoti kuwa Rais Recep Tayyip Erdogan yuko "salama” lakini hakikufafanua zaidi.
Baadaye, Bw Erdogan ameambia kituo cha habari cha CNN Turk, kwenye mahojiano ya webcam, kwamba kitendo cha leo kimechochewa na kuwepo kwa "mfumo sambamba". Amesema jaribio la mapinduzi litakabiliwa kwa "hatua ifaayo" na kuwataka raia wa Uturuki wajitokeze barabarani.
Mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na YouTube ilizimwa muda mfupi baada ya taarifa za mapinduzi ya serikali kutokea.

Source BBC swahili
1468623865224.jpg
 
Back
Top Bottom