Kundi la kigaidi la Islamic state lateka bandari muhimu Msumbiji

Hakuna kitu kigum kusafirisha kama silaha za kivita pia kuzitumia sio rahisi kwa mtu ambaye hana mafunzo!!
Pia sio pesa kidogo! risasi zenyewe tu sio pesa kidogo!
Ni kweli.
Lakini mimi naweza kumiliki AK-47 kwa urahisi kabisa na nikaishi nayo Nyumbani kwangu bila wasiwasi endapo tu sitakuwa na matumizi nayo!

Unajua zinapatikana wapi na zinafikaje mikononi mwa watu? Hii sio kazi yangu Polisi na maafisa wengine wa usalama wanayajua haya yote.

Sasa kama mtu wa kawaida kama mimi naweza kupata AK-47 hao masalafi wenye mapesa kwa kutumia rasilimali zao zote, wenye misimamo inayoungwa mkono na makundi mbalimbali ya kigaidi ya kiislamu watakosa more advanced weapons?

Kusafirisha is not an issue, issue ni utazipataje kwisha mchezo.
 
Jamani NGO's ziangaliwe sana. Ni Majasusi yanagawa hela za kufugia kukunkwa watu wetu. Niko na imani hiyo.
Tatizo la Muafrika ni chuki miongoni mwetu. Sijui kwa nini.
Lakini inahitajika hili, tuletewe sijui demokrasia sawa, vyama vingi sawa lkn inapofika swala la utaifa tuweke vitu chini tuamue kama nchi.
Hatafaa kumuona mzee wetu wa kimasai, kihaya, kichaga ,msukuma au yeyote anataabishwa eti kwa sababu si kanda yetu NEVER EVER. Better die fighting.

Kiongozi anaweza kuwa mbovu sawa katuibia sawa, anatukana sawa ila msimamo uwe Utaifa wetu.

Wazungu waoneni ,wanayo ajenda ya siri na mali zetu, ikiwa karne ya 19 walikosa malighafi wakaamua kuja Afrika je karne ya 21 wametoa wapi? WANAZITAKA HATA LEO
 
Na uwarabuni je , uwe unawaza Kwa kutumia kichwa mda mwengine, hao wanajiita sio kama waislam wamejipachika jina lengo kualibu uislam hata Mimi naweza nikajiita mfuasi wa Kristo lakini nikafanya mambo tofauti na aliyokua anayofanya au anayokataza Kristo sasa ukisema msumbiji wamefamiwa na hao wanaojiita IS sababu wengi wakristo vipi kuhusu huko uwarabuni ?
Yani kama umeshindwa kunisoma kwa utaratibu na kuelewa mengine utayaweza kweli?

Nani kasema kuwa IS wamevamia Msumbiji kwa kuwa hilo taifa lina Wakristo wengi?

Haya wakishachafua hiyo imani yako what's next?

Huu ni mpango wa marekan wanatumia neno uisilam lengo kuchafua dini hii na kwakua ujinga huu ulianzia uarabuni Kwa kupora mafuta ndio akatumia Imani za watu ili afike malengo yake na kuchafua uislam
Wanaichafua imani ya kiislamu "Marekani" haya unaweza kutueleza kwanini wanaichafua na matokeo chanya watakayoyapata au wanayoyapata kutokana na huo uchafuzi?

Na kwanini wameanza kuichafua miaka mingi sana yani toka bibi wa bibi wa bibi yako hajazaliwa ina maana hawafanikiwi tu?
 
Tuna safari ndefu sana kuwa na watu wenye mawazo kama yako!
Kwa tarifa yako hapo tukitia mguu tunakula vikwazo visivyo julikana!
Hiyo haiwezi kuwa sababu!
Tanzania ina watu wenye akili sana hawaendi kichwa kichwa, na hao watu wanasubiri tu wapate sababu ya kuja!

Kuna uzi wa masalafi humu.
Wako Somalia hapo tumepaogopa sisi tuko Afghanistan huko na DRC na manchi ya mbalimbali!
 
Mkuu ndio maana nimesema ww akili yako ni ndogo,
Ulianza na ninatakiwa kupimwa akili nikakuuliza nani amekudanganya kuna kipimo cha akili umekwea mnazi, sasa umekuja kwenye akili ndogo!

Unaweza kutueleza akili ndogo ikoje?

yaani unani unaomba udhibitisho wa yakwamba kama waasi hao wana silaa?
Silaa = Silaha.
Alafu kuna tofauti ya udhibitisho na uthibitisho hapo palifaa kutumika neno uthibitisho.

Yes nataka uthibitisho kwa sababu umesema hao waasi wa Msumbiji wanamiliki silaha za mabilioni ya fedha, thibitisha hili.

Kwahiyo hivyo vita wanavyo pigana na serikali kiasi cha kuishinda nguvu wanatumia madera ya kudangia ya dada yako kupigana hivyo vita au?
Hufahamu hata suti na hoods zinatumika kudangia? Kumtumia dada yangu hapa ni dharau na upumbavu dada yangu mimi anaweza kuwa bibi yako au zaidi ya bibi yako kwa umri wako! (Naufahamu)

Majeshi ya DRC kwa kushirikiana na Monusco hadi leo wanapambana na waasi wanaopatikana kwenye misitu ya Congo ambao wana silaha za kawaida kabisa ambazo zinapatikana kwa wingi mno maeneo hayo una hii habari?

Mwisho umepata wapi ujasiri au nguvu ya kusema Jeshi la Msumbiji limeshindwa nguvu na hao waasi wa kiislamu?
Tanzania ilipambana na wahalifu wa Kibiti kwa muda gani?

Hivi jeshi la serikali unaweza kulishinda bila ya silaa nzito na kali au una dhani kuishinda serikali ni lelemama. Hivi utamilikije wapiganaji bila kuwalipa, kuwalisha na kuwatibu?.
Kulishinda nguvu jeshi ni kitu cha kawaida sana lakini swali ni kwa muda gani utaweza kuulinda ushindi wako?

Jeshi la Polisi Tanzania lilizidiwa nguvu na wahalifu wa Kibiti je hao waasi walikaa na huo ushindi kwa muda gani?
Je walikuwa na silaha nzito ambazo Polisi hawana?
 
na Syria au Libya nako majority ni christians??

Kumbuka Msumbiji population yake kubwa ni Wakristo, inamifumo Kristo n.k na hili jambo limetokea na litaendelea kutokea kwa sababu ambayo si uwingi wa Wakristo msumbiji

Ulisoma vizuri maoni yangu au ndio usalafi umeanza?

jiulizeee kwa nn hizii vuruguu daima zinatokea maeneo yenye resources muhimuuui??
Jaribu kufikiriaa nje ya upofu wa udini utaelewaaa
Huwa nacheka sana napoona vitu kama hivi.
Unaweza kuniambia Msumbiji ina rasilimali gani muhimu na bora sana ambayo haiko Tanzania?

Unaweza kuniambia kwanini Uganda wana Oil na hakuna hayo mambo?
Unaweza kuniambia kwanini Angola wana Oil na hakuna hayo mambo?
Unaweza kuniambia kwanini Tanzania ina Tanzanite na hakuna hayo mambo?

Au hivi si muhimu ila muhimu ni gesi ya Msumbiji ambayo Tanzania pia inayo?
 
Silaa ndio nini mkuu?
Mkuu ndio maana nimesema ww akili yako ni ndogo, yaani unani unaomba udhibitisho wa yakwamba kama waasi hao wana silaa?
Kwahiyo hivyo vita wanavyo pigana na serikali kiasi cha kuishinda nguvu wanatumia madera ya kudangia ya dada yako kupigana hivyo vita au?

Hivi jeshi la serikali unaweza kulishinda bila ya silaa nzito na kali au una dhani kuishinda serikali ni lelemama. Hivi utamilikije wapiganaji bila kuwalipa, kuwalisha na kuwatibu?.
 
Ni wale wale, na wangechekewa basi leo hali ingekuwa kama ya Msumbiji. Serikali inapo wadhibiti siasa kali kama wale Mashehe wa Uamsho wengi wanashindwa kuelewa kuwa vile ndiyo chanzo cha hii hatari na madhara yake ndio haya. Wale jamaa wana pesa na wanaweza mshawishi mtu yeyote kujiunga nao.

Tatizo la Msumbiji wao kwa wao hawaelewani, wana Ukabila, wana Waasi wa Renamo. Hawazungumzi lugha moja. Wanaishi kiujima ujima, hawana mahusiano mazuri na majirani zao. Ni wabinafsi na wanajiona sana na wanajifanya ni Wareno. Wanawadharau raia wa nchi nyingine hasa Waafrika wenzao. Nk.

Wacha wajifunze kuheshimu majirani.

Kama hao Magaidi watapenyeza huku TZ tunaomba Serikali itangaze kujitolea kupigana nao, huku mtaani tuko mgambo wengi sana sana, na tuna hamu ya kuwashikisha Adabu hao vibaraka.

Tuta watwanga hata kwa marungu. Kama Bunduki tutazinunua wenyewe.
Ivi ukiambiwa haya saini uende uanja wa mapambano utaenda au unasema tuu!
 
Ivi ukiambiwa haya saini uende uanja wa mapambano utaenda au unasema tuu!
Kwanini nisiende...!
Tana natamani sana kwenda katika uwanja wa vita, ilimradi niletewe silaha nitakazo agiza.

Tambua mapigano ya silaha yana watu wake na sio kila mtu anaweza kumudu.

Mi niko tayari hata sasa, we niletee silaha nitakazo kuagiza tu.
Na mahitaji mengine ya Kivita.
 
Heshima yenu wakuu

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kikundi cha wapiganaji huko Mozambique ktk mkoa wa CABO DELGADO wamefanikiwa kuiteka wilaya kubwa ya MSIMBOA DA PRAIA!

wameua mamia ya wakazi kwa kuchunja na baadhi ya wanajeshi hvyo mji huo mpka sasa hauna Raia yoyote na sasa washaichukua bandari ya wilaya hiyo!hli si nzuri ukizingatia wilaya hiyo ni KM chache mpka Mtwara !!wakimbizi wengi kutoka hiyo wilaya washakimbilia mtwara pia!!

Na hapo kwenye issue ya wakimbizi kukimbilia kwetu ni hatari nyingine pia, ubaya wa magaidi huwezi kuwatambua maana wanavaa kiraia tu.
 
Hawa jamaa serikali ya Msumbiji imewalea sana tangu mwanzo..na haya ndio matokeo yake!
Ni kweli kabisa, nakumbuka pale kibiti tungezembea basi na sisi tungekua katika wakati mbaya sana, maana polisi walikua wanaelekea kuzidiwa. Ndipo vijana wetu shupavu wa Jwtz walipoingia pale, ulifanyika msako wa nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda, kichaka kwa kichaka, kila kilichofunikwa kilifunuliwa, yatosha kusema ya kwamba walichokipata wale WAPUMBAVU hawatakisahau maishani mwao, ndipo baada yakuona chakufia nini! Baadhi yao waliofanikiwa wakatoroka.

Kwakuliona hilo JWTZ wakaamua kujenga na kikosi kabisa ktk pori la Rufiji.
 
Mkuu haya uliyoandika hapa yana ukweli?...🙄🙄🙄...
Yes sasa hivi kuna articles kibao ziko wazi kuzungumzia hiyo nchi,na walivyofanya. Watu baadaye walikuja kuuana mpaka leo kuna anti balaka na anti seleka . Anti Balaka ni wakristu, Anti Seleka ni waislam ni mgambo lakin msemaji wa Kundi na viongozi wachache ndio walikua waislam tena nadhani wengine ni majina walijipachika. The world is so complex. Africa ina vibaraka wengi na wasaliti
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom