kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Aliyekuwa Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel Moshe Ya'alon amefichua kuwa magaidi wa kundi la ukufurishaji la Daesh waliwahi mara moja kuwashambulia kimakosa askari wa utawala huo katika eneo la miinuko ya Golan kusini mwa Syria lakini waliomba radhi haraka.
Ya'alon ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya 10 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni na kukiri kwamba akthari ya mashambulio ya makombora yaliyofyatuliwa kuelekea 'Israel' hayakufanywa na wanamgambo wa Daesh bali yalitokea maeneo yanayodhbitiwa na jeshi la Syria.
Kabla ya hapo magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh (ISIS) walikuwa wameshatangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa hawatopigana vita na Israel.
Ijumaa iliyopita, jeshi la utawala haramu wa Israel lilitangaza kuwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) zililengwa na makombora matatu yaliyotokea ndani ya ardhi ya Syria katika miinuko ya Golan lakini hayakusababisha maafa.
Aidha jana Jumapili jeshi la Israel lilishambulia ngome ya jeshi la Syria ya Nab'ul fawaz, kaskazini magharibi mwa Rif Qunait'arah na kuwaua askari watatu na kuwajeruhi wengine wawili.
Tangu mwezi Machi mwaka 2010, wakati ulipoanza mgogoro wa Syria hadi sasa, utawala wa Kizayuni umekuwa ukiwasaidia na kuwaunga mkono magaidi wanaopambana na serikali halali ya nchi hiyo.
Hivi karibuni, kanali Tomer Koller, daktari wa kikosi cha 210 cha jeshi la Israel alitangaza kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi wanaojeruhiwa vitani nchini Syria wanapelekwa 'Israel' kutibiwa kupitia eneo la miinuko ya Golan.../
Source;Parstoday.sw