Kundi hatari la vijana wajinga linazidi kuongezeka

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Wadau Nawasalimu,

Najua wapo watakaonilaumu lakini wenye Upeo Mkubwa wa Kuona mbali wataniunga Mkono.NCHI yetu inazalisha VIJANA wengi sana MASHULENI na VYUONI lakini wengi wao wanabaki MITAANI wanazururura hawana cha kufanya Wachache wao tena WATOTO wa VIONGOZI ndio Wanapata AJIRA.

Hatari ninayoiona ni hii ya hili KUNDI lisilo na AJIRA.Kundi hili VIJANA wake HAWAJIELEWI na wengi wao wamejiingiza kwenye MAMBO ya HOVYO yasiyo na Tija kwa TAIFA.

VIJANA hawa Wamekuwa Wazururaji Wezi wala Madawa Wabakaji Walevi na Wacheza Kamari Vitendo hivi mimi Naviita ni vya KIJINGA na Wanaovitenda ni WAJINGA.Kadiri Miaka inavyosonga mbele Kundi hili la WAJINGA linazidi kuongezewa.

Wasiwasi wangu ni Kwamba Kundi hili likiwa KUBWA kuna Siku litaamua Kumuunga Mkono Mgombea URAIS MJINGA na kwa WINGI wao Wakampigia KURA na AKASHINDA na NCHI yetu ikaongozwa na MJINGA aliyewekwa Madarakani na WAJINGA
 
Asante kwa taarifa lakini kwa uhakika bokisi la Kura Afrika haliwezi kukamilisha huu wasiwasi wako.

Chunguza mfano tu nchi jirani tu hapo karibu, majina yanayoongoza serikali ya mtaa ubin ni ule ule kuanzia babu hadi kitukuu.

Hao wajinga unaowataja watusubiri kwanza.
 
Kwa sasa tuwekeze kwenye elimu ya ujuzi kwa watoto wetu. Hakikisha kama una ofisi, basi watoto wako wanajifunza ujuzi.

Haya masuala ya kusubiria ajira mbuzi na zenye urasimu mwingi, za serikali; ni kuwaumiza tu watoto.
 
Mzee, kura na ushindi kwa huku kwetu ni mistari pacha, hakutani popote pale!

Baki kwenye ujinga wa vijana, kura haijawahi kumuweka mtu nafasini hapa Tz

..mwisho wa siku " wajinga " watajazana kila mahali.

..Na ndio watakaokuwa wasuka mipango ya kuchezea sanduku la kura na kumsimika mjinga mwenzao madarakani.

..dalili zake tumeziona ktk kundi la MATAGA / WASIOJULIKANA na uchafuzi wa 2020.
 
Who care?

Hakuna anaye tengeneza fursa na kuwa inua vijana

Asilimia ya vijana wanaoajriwa katika sekta binafsi na serikali haizidi 7% ya vijana

Wazungu : " Kaburini Ni Sehemu tajiri sana , coz ndoto za watu zimefukiwa "
 
Hapana,
Kumuweka kiongozi madarakani haitawezekana as kwa nchi kama hii hatuna correlation ya ballot box na kumuweka mtu madarakani.

Nachojua ni kuongezeka kwa watu wa hovyo, uhalifu wa kila aina mitaani kutokana na vijana ambao hawana kitu wanafanya cha kueleweka!
 
Kwan hao wenye akili wanaoongoza nchi wamewasaidiaje hao wajinga... Itapendeza wakiweka mjinga mwenzao
 
Kila Mitaa na Kitongoji Vijana kibao hawana cha kufanya, ata vibarua au connection ata za kubeba mizigo sehemu hakuna. Kila mtu amebaki kimya tu. Mungu aepushie mbali lakini kuwa kijana sasa ni hatari, ni kupigwa na maisha tu.
 
Mkuu timiza hata mwezi na hii ID yako, Jifunze kuandika na kupanga aya, Baada ya hapo uje kuwananga hao watoto wa Masikini humu.
 
Mjinga akiwa mmoja wakishakuwa wengi ni chama Cha siasa kabisa.... Na usidharau nguvu ya wajinga kwa pamoja.
#Niliyoambiwa utotoni nayashuhudia😔😔
 
Watu wako beausy kujadili kubishana
Usajili simba yanga,reyvn sjui kuondk
Wasaf.....show ya mondi nje,kajala konde.....mimba ya nandy sjui
Machawa wanaonekana role model kila mtoto anataka awe mkata mauno

Ova
 
Kwa sasa tuwekeze kwenye elimu ya ujuzi kwa watoto wetu. Hakikisha kama una ofisi, basi watoto wako wanajifunza ujuzi.

Haya masuala ya kusubiria ajira mbuzi na zenye urasimu mwingi, za serikali; ni kuwaumiza tu watoto.
Hii pointi muhimu sana. Hata kama una genge bora watoto wajifunze kurudisha chenji kama wadosi.
 
Back
Top Bottom