Kundi gani linafurahia utawala wa Rais Magufuli mpaka sasa?

Chillo97

JF-Expert Member
Jun 18, 2016
630
933
Wana bodi,

Mimi kwa sasa niko mtaani na biashara zangu ndogo ndogo. Biashara hii inanikutanisha na watu wa aina zote wafanyabiashara wa kati wadogo wadogo wakulima na wafanya kazi wa serikali na mashirika binafisi.

Kwa upande wangu na biashara zangu ndogo ndogo kwa sasa mauzo ya siku yameshuka zaidi ya 30% kulinganisha na kipindi kilichopita hali ni ngumu zaidi.

Wateja wangu wakubwa na wadogo wote wanalia njaa wafanyakazi wa serikali wanadai hali ni ngumu hakuna vikao hata semina za kuwafanya wapate chochote cha ziada. Posho zimepungua hali ni mbaya maofisi.

Kwa wafanyabiashara wengine hawa wa jumla na wenye makampuni miradi mingi ya watu binafsi imesimama na kusababisha ukata kwa wafanya biashara hawa.

Kwa kuwa hawa watu wenye pesa ndio waliokuwa hata wanasababisha ulaji kwa masikini sasa na sisi wa hali ya chini njaa umetanda hakuna kazi za vibarua kwa kuwa miradi imesima.

Je, mtaani kwako hali ikoje?
 
Ukipewa kazi kubwa usiifanye kwa kukamia utaumiza wengi na kukosesha watu amani. Mambo hufanywa step kwa step ndipo misingi itajengeka vema lakini kubwa Ni unaweza kubana watu saana na mpakamwisho lisionekane lamno ulilowabania hapo ndio tujus uongoz Ni spiritual plus art sio hamasa na ubabe
 
Hahahahahaaaaaa! Magufuli hayupo hivyo. Anafanya mambo mengi kwa pamoja na yote yapo katika ubora ule ule.
 
Ukipewa kazi kubwa usiifanye kwa kukamia utaumiza wengi na kukosesha watu amani. Mambo hufanywa step kwa step ndipo misingi itajengeka vema lakini kubwa Ni unaweza kubana watu saana na mpakamwisho lisionekane lamno ulilowabania hapo ndio tujus uongoz Ni spiritual plus art sio hamasa na ubabe
We jamaa unaonekana una akili sana aisee.
 
Mimi na watanzania wote wanaonizunguka tunafuraha sana na utawala wa Rais Magufuli na tunamsapoti kila hatua anayochukua.

Sijui wewe mweenzangu unaishi na watanzania wa wapi hao?
 
Huu utawala umesaidia wale waliokuwa wanapinga short cut, waliozoea ujanjaujanja hili ni kaa la moto tena lipo mfuko wa nyuma kabisa, 10% na tenda bila vifaa zimeyeyuka, kuuziana mbuzi kwenye gunia kunamalizikia, shopping za dubai zilizikwa tangu december, kazi za vi memo kwisha habar yake. Kwa hali hii mtaani lazima pawe pagumu kweli.
 
Kikwete anafanyiwa assessment baada ya kuongoza miaka kumi! Magufuli anafanyiwa assessment kabla ya miezi kumi.

Tatizo la Magufuli alianza kwa speed na matambo mengi ndio maana kila anachofanya sasa hivi anapimwa nacho.
Kwa kuwa ameingia kwa kujinasibu kwamba ataondoa majipu huku akisahau kwamba mfumo wa hayo majipu ndio uliomweka madarakani.
 
Kama mvua inanyesha vizuri wanaoisifia ni wale wanaonyeshewa na mvua hiyo.Wengine hawaoni hata dalili ya mvua ambayo ni mawingi.AJIRA KWANZA.
 
Back
Top Bottom