Kunani Simba Sc Vs IPP Media? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunani Simba Sc Vs IPP Media?

Discussion in 'Sports' started by Kakalende, Nov 26, 2007.

 1. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2007
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Inaelekea kuna bifu kati ya vyombo vya habari vya IPP Media na Klabu ya Simba, wamesusa kutangaza habari za Simba kwa zaidi ya miezi mitatu sasa; kuanzia redio-one, ITV na hata magazeti! Hata wakati ligi ya Vodacom inaendelea kiasi kwamba hata matokeo ya mechi kati yao na Yanga haikutangazwa.

  Ingekuwa inawahusu Yanga tungefikiria labda ni muendelezo wa ugomvi wao na Manji lakini hili laSimba kuna namna! Wadau leteni data za ndani kama zipo.
   
 2. M

  Middle JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2007
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hata mie nikishaliona ilo,kuna bifu hapo
   
 3. A

  Agao Kichore Member

  #3
  Nov 27, 2007
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nashukuru Kakalende kwa kulivumbua hili. Ni majuzi tu ndo nilianza kushtukia vyombo vya habari za kufanya habari za Simba kuwa siri. Ningependa nikueleze kuwa si ITV au Radio One na magazeti ambata tu bali vyombo vingi tu vya habali wamezifanya taarifa za msimbazi kuwa kichele. Jumapili ya tarehe ile baada ya Jumamosi ya Man U kufungwa na Bolton, Simba walicheza mechi na Zanzibar Heroes. Sikupata fulsa ya kufika kiwanjani lakini nilitegemea kupata chochote toka kwenye media. Ndugu yangu sikuamini maana kama hiyo mechi haikuwepo. Si IPP wala Clouds waliyoweza kugusia mechi hiyo iliyopigwa Taifa. Na hata kesho yake katika magazeti ni gazeti moja tu ndo liliweza kutoa kipande kidogo kuhusu mechi hiyo.
  Taarifa za Msimbazi wakati wa mgogoro na walipokuwa wakidundwa kwenye ligi zilikuwa kibao lakini imagine hata kikosi kilichotangazwa na Simba hazikutajwa na Clouds. Hawa jamaa wanatangaza mpaka mechi za mchangani lakini mechi ya Simba inasababisha moto kitega uchumi na vyombo vingine vya habari.
  Je, who is backing this non-sense? Is this what Ben concluded that Waandishi wa Bongo ni waandishi 'UCHWARA'?

   
 4. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2007
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Simba kuwasilisha usajili leo

  2007-11-26 09:06:38
  By Somoe Ng\'itu

  Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa leo unatarajia kuwasilisha majina ya wachezaji wake katika Shirikisho la soka nchini (TFF) ambao itawatumia kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mapema mwakani.

  Makamu mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba, Geofrey Nyange `Kaburu` alisema jana kuwa wamefikia maamuzi ya kuwasilisha usajili huo kufuatia kukamilika kwa zoezi hilo.

  Kaburu alisema kuwa sababu za wao kuchelewa kupeleka usajili wao ilikuwa ni kutaka kuhakikisha kuwa wanasajili wachezaji kulingana na mahitaji na si kuangalia majina makubwa pekee.

  `Suala la usajili ni nyeti na sasa tumekamilisha tunaomba ushirikiano wa wanachama na wapenzi ili kufikia malengo,` alisema Kaburu.

  Alisema kuwa licha ya kutopata ratiba ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati wanatarajia kucheza mechi za kirafiki mbalimbali ili kukipa majaribio kikosi hicho kipya.

  Baadhi ya wachezaji wapya walioripotiwa kusajiliwa na Simba ni pamoja na Edwin Mukenya, Juma Nyoso, Michael Katende na Vicent Barnabas.

  Simba iko chini ya kocha Jamhuri Kihwelo huku uongozi na kamati hiyo ya usajili ikisema kuwa inaanza taratibu za kutafuta makocha wa nje ya nchi ili kuongeza nguvu katika benchi la ufundi.

  * SOURCE: Nipashe
   
 5. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2007
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani au Nipashe la Mwananchi Com na sio IPP?
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2007
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Siku hizi wanaitangaza Simba kidogo kidogo kupitia 'Ze Comedy' lakini kutotangaza matokeo ya mechi haina maana.

  Isijekuwa ni visa binafsi vya watangazaji wao ambao wengi tunawafahamu ni 'manazi' wa Yanga.
   
 7. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hili bifu halijaisha!

  Kumbe ni ITV ambao wamesusa kuitangaza Simba, na kwa kiasi fulani RadioOne. Hatujui iwapo ni sera rasmi ya vyombo hivyo vya habari au ni unazi wa baadhi ya watangazaji ambao tunawajua ni Yanga damu.

  Magazeti yao yanaiandika lakini wanaposoma magazeti kwenye taarifa ya asubuhi wanajitahidi kutozitaja habari zinazoihusu Simba.

  Baadhi ya watu humu JF wataniambia lete ushahidi! nasema mwenye macho haabiwi tazama.
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Makubwa haya...
   
 9. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  kuna kajiukweli kuhusu hili. ANGALIA WANAPOSOMA MAGAZETI ILE ASUBUHI, kukiwa na habari inayohusu SSC INAKUWA SKIPPED! ............!LABDA huwa hazionekani na muda unakuwa umekwaisha(MBONA KWA HABARI ZA SIMBA TUU KULIKONI!)
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani hamjuwi kuwa Mengi ni Yanga?
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hata ushindi mkubwa walioupata Simba jana wakiwakilisha Taifa hawakutangaza kwenye taarifa ya jana usiku na leo asubuhi msoma magazeti alikuwa akiikwepa habari hiyo!

   
 12. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  BASI KWA U-BIASENESS WAKE NDIYO SABABU DINI FULANI ILIANZA KAMPENI YA KUSUSIA VINYWAJI VYAKE(COCACOLA)NA WAKAAHIDI KUTENGENEZA "coca cola" za dini yao..............
  SIMBA S.C NAO WATATAKA KUSUSIA MEDIA ZA IPP? JAMANI SWALI HILO LATAKA JIBU
   
 13. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #13
  Feb 29, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tangia amalize adhabu ya kufungiwa na "fwati" amekuwa kimya sana; enzi zake Simba wa Yuda angewapasha maneno yao hawa "aitivii"

  [​IMG]
   
 14. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Inaelekea lile bifu limeisha!

  Leo katika taarifa yao ya habari aitivii wametangaza kipondo cha 4-0 walichsulubiwa Simba huko Aba na Enyimba ya huko.

  Shukrani za dhati watangazaji wa aitivii kwa kuitikia wito wa wadau.
   
 15. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  poeni sana Simba SC, jitieni moyo, mjipange vizuri mnaweza kushinda tu. Kwani wao wanaweza wananini? nasi tushindwe tuna nini? ila acheni kuwaponda YANGA.
   
Loading...