Kunani nyuma ya pazia juisi ya miwa kukosa bahati ya kufanyiwa usindikaji?

TEAM 666

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
4,330
8,421
Habari moja kwa moja kwenye kwenye bandiko letu

Muwa nalo ni-jamii ya Tunda ambalo for my research naona limekosa kabisaa kufanyiwa brand pakeges Kama ilivyo kwa ukwajuu,Embe ndizi..nk

Juice per juice fresh ya miwa bongee moja la ideas wenye mitajii kamatia fursaa hii

Watu wanapendelea zaidi bidhaa ya asili kuliko haya masoda yao yenye madhara kwa afyaa

1.-Homemade-Sugarcane-Juice.jpg

Hapa pia kunaitajika brand hizi Juice naona zinauzwa Sana local level. Narudia tena,kusema mwenye mtaji afanyee ivestment hapa kweye juice ya miwaa hatojutiiaaa.

Faida zake za kiafya zinatosha kabisaa kuliteka soko

WEB-PRODUCT-_-UKWAJU-JUICE.jpg

Azam product amefanya bonge la Ideas kwenye hii Brand watanzania wengi tunapenda juice fresh Kama hizi.

Embe-300x300.jpg

Embe pia limepata bahati yakufanyiwa pakeges yakiwango Sana.
 
Faida za juice ya miwa


1.Juice ya miwa ni chanzo cha sukari ya mwili (glucose) hivyo hutupatia nguvu na kurudisha maji yaliyopotea. Bora unywe juice ya miwa kuliko energy drink.

2. Licha ya kuwa juice ya miwa ina ladha tamu na ina sukari nyingi ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari, ina sukari asilia ambayo ina kiwango kidogo cha glycemic index ambayo ndio huongeza kiwango cha sukari mwilini.

3. Juice ya miwa ina viwango vya juu vya Calcium, Magnesium, Potassium, Iron, na Manganese ndani yake. Magonjwa kama saratani (cancer) hayawezi kukaa katika mazingira yenye viwango vya juu vya madini haya, tafiti zinaonesha inasaidia sana kupambana na Saratani.

4. Juice ya miwa pia huongeza kiwango cha Protein mwilini, inaboresha afya ya figo na pia husaidia kuondoa maumivu kama ya kuungua vile wakati wa haja ndogo ambayo mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa na UTI.

5. Juice ya miwa pia inafanya kazi kubwa ya kuondoa sumu mwilini, ina vyanzo ndani yake ambavyo husaidiana na ini katika kuondoa sumu mwilini, kuboresha kinga ya mwili, kulinda ini dhidi ya maambukizi.

6. Juice ya miwa pia inatumika kama kiungo muhimu katika kumeng'enya chakula, ndani yake kuna potassium ambayo husaidia kuweka mfuko wa umeng'enyaji chakula katika hali nzuri kuzuia maambukizi tumboni na kulainisha haja.

7. Tafiti zinonesha Juice ya Miwa inaepusha kuoza/kuharibika kwa meno na harufu mbaya katika kinywa.

8. Upungufu wa virutubisho katika mwili wako unaweza kuonekana kupitia makucha, Kama una makucha yanayokatika ovyo, vidoti vyeupe, basi ni muda wa kuweka Juice ya miwa katika mlo wako.

9. Pia Juice ya miwa inasaidia katika kupambana na homa za hapa na pale hasa kwa watoto ambazo hupelekea kupunguza kiwango cha Protein Mwilini hivyo unywaji wa Juice ya miwa hutatua tatizo hili.

10. Likija ni swala la afya ya ngozi basi lazima utaongelea alpha hydroxy acids ambayo huwa na faida nyingi baadhi ikiwa kupunguza kuzeeka kwa ngozi na kuacha ngozi ikiwa na maji muda wote. Juice ya miwa ni moja ya chanzo chake.
 
Idea hii labda kama muqekezaji ana pesa za kuchezea, Soko la juice ni kuna matunda Giants ndio yamekubalika na soko miaka na miaka
*Embe
*Passion
*Pineaple
*Orange

Hizo ndio juice Giants miaka yote

Muwa nalo ni-jamii ya Tunda
Muwa sio tunda
Watu wanapendelea zaidi bidhaa ya asili kuliko haya masoda yao yenye madhara kwa afyaa
_Hii ni kujiongopea hakuna soko linalopenda bidhaa za asili
1)Ingekuwa hivi Brand za Coca-Cola na Pepsi zisingekuwa Giant Duniani.
2)Makjuice na Zanana wangekuwa mamillionaire/Billionaire.
Hii Azam Ukwaju isha Floop ipo ICU


Zikija juice za miwa zitakuwa trend kama Azam ukwaju zitapotea vibaya sana.
 
Watu wanapendelea zaidi bidhaa ya asili kuliko haya masoda yao yenye madhara kwa afyaa
Policosanol present in sugarcane can cause insomnia, upset stomach, dizziness, headaches and weight loss (if consumed excessively). It can also cause blood thinning and can affect cholesterol levels in the blood.
 
Soda zina madhara gani kwa afya, na ni kutokana na utafiti gani?
madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.Tafiti mbalimbali za wanasayansi zinaeleza kuwa soda ina asidi aina ya ‘phosphoric’ yenye uwezo wa kuvuruga madini ya ‘calcium’ yaliyoko mwilini na kusababisha mifupa na meno kudhoofika.

Aidha, asidi aina ya ‘phosphoric’ huvuruga asidi aina ya ‘hydrochloric’ iliyo tumboni mwa binadamu na hivyo kuharibu mfumo wa kusaga chakula.

Viwanda vya soda ndio watumiaji wakubwa wa sukari na wanasayansi wanasema sukari hupandisha kiwango cha ‘insulin’ ambayo husababisha kasi ya mzunguko wa damu, ugonjwa wa moyo, kupanda kwa ‘Cholesterol, kisukari, kuzeeka mapema, ongezeko la uzito na maradhi mengine.

Aidha inadaiwa kuwa viwanda vya soda pia hutumia dawa ya kulevya aina ya kafeini. Wataalamu wanasema vinywaji vyenye kafeini, husababisha kupanda kwa mapigo ya moyo, kasi ya mzunguko wa damu na matatizo ya kiza.
 
Madhara ya sukari ni yapi mwilini?
Sukari nyingi ni inayoanzia kiasi gani?
Miwa si ndio malighafi ya kutengenezea sukari ambayo umedai sio nzuri kiafya?
Sukari yamiwa ni original haina kemikali yoyote ilee
 
Viwanda vya soda ndio watumiaji wakubwa wa sukari na wanasayansi wanasema sukari hupandisha kiwango cha ‘insulin’ ambayo husababisha kasi ya mzunguko wa damu, ugonjwa wa moyo, kupanda kwa ‘Cholesterol, kisukari, kuzeeka mapema, ongezeko la uzito na maradhi mengine.
Na miwa ndio inatumika kutengeneza sukari
 
Back
Top Bottom