Kunani jimbo la mtwara mjini..??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunani jimbo la mtwara mjini..???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Sep 18, 2010.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kiifupi na Kihistoria mji wa Mtwara ni mji wa mwambao ambao upo kusini mwa Tanzania yetu ambao kipindi cha ukoloni ulikaliwa na waarabu toka mashariki ya kati, ni mji ambao unajulikana kihistoria zaidi kwa kuwa na ngome kubwa ya Waarabu pale Mikindani(Museums) . Hauna tofauti na ule mji wa bagamoyo kihistoria ila tofauti t uni kwamba yale majengo ya mikindani ambayo yalistahili kuwa makumbusho na ni vivutio kwetu si wenyewe na wageni, yamekwisha mno kiasi cha kwamba hayana tena thamani na mengi yameshabomoka kwani hayajawahi kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile kwa kipindi kirefu sana. Mji huu ambao kwa sasa unaitwa Mtwara-Mikindani, hapo mwanzo ulikuwa unaongozwa na kutawaliwa na waarabu ambao baadae walijichanganya na wenyeji na kuzaliana, ni mji ambao wakazi wake wengi ni waislam. Nimeanza hivyo kwakuwa huenda watu walio wengi wanausikia tu huu mji labda kwa umaarufu wake kwa kuwa na zao la korosho, na wengine hawaujui kama huu mkoa upo upande gani wa Tanzania(kusini ukiambatana na mipaka ya msumbiji na Malawi).
  Sasa ni hivi, kwa muda mrefu sana,tangu mimi nimezaliwa huu mji unapiga hatua polepole sana na kwakweli mwendo huu wa kobe sijui kama tutafika kule ambako watanzinia wengi watashawishika hata kuja mara moja kuuangalia. Uongozi na usimamizi mbovu wa viongozi ambao wapo kwenye mji huu kwa kweli unakatisha tamaa sana, na hapa ndipo mada yangu inapoanzia. Sina lengo la kuzungumzia udini katika inshu nzima ya uongozi katika jimbo hili la mtwara mjini la hasha ila itanilazimu niongelee swala hili kwani ndio ukweli uliopo na ndio vitu vinavyofanyika pale.
  Tangu kipindi kile cha miaka ya sabini ambapo kulikuwa na mfumo wa chama kimoja hadi hii leo wabunge waliongoza jimbo hili ni Waislamu, kumbukumbu zangu zinaniambia kwamba kipindi kile nilivyozallliwa kulikuwa na Mbunge toka CCM anaitwa Mzee Mkanyama, huyu bwana hata sielewi sasa hivi yupo wapi,baada ya hapo wabunge waliofuatia ninaowakumbuka ni Mpeme, Sinani na sasa ni Murji aliyepitshwa na CCM. Mchakato mzima wa kuwapata hawa mabwana kiukweli ni udini ulishamiri katika pande hizi. Ikumbukwe kwamba tangu mwaka 1995 pale Rais Mstaafu BENJAMIN WILLIAM MKAPA kutawazwa kuwa raisi, nlidhani ndicho kitakuwa kipindi kizuri kwa watu wa mtwara kuneemeka kupitia mbunge wake Mpeme kuleta maendeleo jimboni.
  Mchakaato wa kumpata huyu bwana ambae kiukweli elimu yake bila shaka ni chini ya darasa la saba, ulijaa udini sana, nasema hivi kwasababu mkapa alimpendekeza mtu mmoja Mr Kambona achaguliwe kupitia CCM,huyu bwana hakupewa hii nafasi na wazee wa kiislamu kwa ile sababu tu eti huyu bwana ni ‘’kafri’’ kwani ameishi sana Italia ambako akiwatumikia wakristu(alikuwa barozi wa Tanzania nchini Italy),kwahiyo hafai kuongoza mtwara eti tu kuna waislamu wengi, vp inaingia akilini kweli? Ndo hivyo wazee wakaamua na kusema kwamba hatuwezi kuongozwa na kafri. Taabu ilikuwa kwa wale wagombea wenzake waliopita kwenye kura za maoni!,walitishiwa kuuawa na Mpeme kwa mtu yeyote atakayepata ubunge mbali na yeye. Aliwafanyia vibweka wagombea wenzake mpaka akapata ubunge . cha ajabu miaka yote mitano hakuwahi kuzunguza lolote pale bungeni zaidi ya kulala tu. Mwaka wa 2000 uchaguzi mkuu,wale wazee wa kiislamu wakamchagua tena huyu bwana awe mgombea,akapata ubunge na hakuongea lolote bungeni hadi alipomaliza utukufu wake.
  Mwaka 2005 kwa mshangao wazee wa pale mjini wakamtipisha mtu mwenye uraia wa msumbiji ambae tena elimu yake nadhani kama sio chini la darasa la saba basi ni si zaidi ya form four,huyu ni Mr Sinani agombee kwa tiketi ya CCM kama mbunge, akapata ubunge, hakuongea lolote bungeni hadi miaka mitano ikapita. Funika kombe mwanaharamu apite, huyu bwana akagombea tena na akabwaga vibaya na mgombea mwenzake (mfanyabiashara maarufu wa kihindi na sio mwenye asili ya kihindi,hapana, ni mhindi) na hapa ndipo ninapoanza kusema haya.
  Katika kipindi cha kura za maoni, palikuwa na wagombea makini ambao sio maarufu sana kwa jamiikulinganisha na huyu Baniani, lakini ni watu makini na wenye ushawishi mkubwa sana, hawa ni Mr JOEL NNANAUKA na Mr. KASUGULU. Nitamuongelea kiundani huyu Joel kwa kuwa namfahamu kiunandani sana. Nasikitika kusema tena kwamba wakazi wa mji huu wa Mtwara itakuwa imekula kwetu tena kwa muda wa miaka mitano ijayo, ile shilingi yetu tuliyoichezea tayari imeshatumbukia ******. Huyu Joel kitaaluma alisoma shule ya sekondari kibaha na ikumbukwe kwamba ndie aliongoza alikuwa Tanzania One (2002),akamalizia pale kibaha na baadae kujiunga na Bicom pale Mlimani University. Simpigii kampeni lakini kiukweli ni mtu makini mzawa wa pale mjini na ambae ana upeo mkubwa ukilinganishwa na wagombea wezake katika kile kinyang’anyiro,mi naamini licha ya zengwe lililofanywa tena na wazee wa pale mjini kitu kingine kilichomwangusha huyu bwana ni udini, huyu ni mkristu,Anglikana.
  Na hata katika kufanya kampeni ni huyu bwana ambae alifanya kampeni za kisasa zaidi kwa kufungua kipindi maalumu katika redio ya PeaceFm akiongea na wananchi wa mtwara mjini na hata wale ambao walikuwa wanakaa mbali kabisa vijijini ambao hawakuweza kwenda kwenye kampen zake. Ni huyu ambae leo hii anasikitishwa sana si tu kwenye kuenguliwa kwenye kura za maoni bali pia kumsikia mheshiwa Makamba alivyowapa ‘STOP’ wagombea wa CCM kushiriki Midahalo, huyu Joel kwenye kipindi chake redioni aliweza kukusanya maswali yote yaliyotoka kwa wananchi na kuyatolea ufafanuzi mzuri. Siwezi sema kwamba CCM haikuwa chaguo sahihi kwake la hasha,ila kwa mpambanaji kama huyu nadhani angeenda CHADEMA(mtazamo wangu) nadhani angeweka ngome imara sana ya chama kama ilivyotokea kwa mgombe flani (Mr. Osman),na hata angeweza kumuengua huyu Gabachori-chori Murji kwani hakuna mtu asiyejua kwamba huyu bwana hana tofauti na ROSTAM AZIZ na ikumbukwe kuwa katoa rushwa sana hadi kupata kiti hiki cha CCM, ni huyu ambae alishawahi kuwa mbunge wa NEWALA kama sio Tandahimba na leo hii alichowatendea wakazi wa pale, hakuna hata mtu mmoja anayetamani kumuuona na wala kusikia CCM kule, huyu bwana ana fedha chafu (hili ni jembe) na anaweza kufanya lolote la dhuruma na asinyooshwe kidole na mtu yeyote, na ndie mbunge tunayesubiri kuapishwa atuwakilishe mjengoni kwa miaka mingine mitano. Elimu yake sidhani kama kuna mtu anayeifahamu, na siwezi ogopa kamwe kusema kwamba huyu hata elimu ya darasa la saba hana asilani!!
  Upeo wa viongozi wanaopitishwa kugombea kwa jimbo la Mtwara mjini CCM kwa kweli ni mdogo na kwa dunia ya sasa sidhani kama hata wataweza kusimama na kutoa ushawishi wa aina yoyote ile mbele ya watu wasio wavivu kufikiri, na nasikitika ni jimbo ambalo lipo wazi sana kwa wapinzani kulichukua kutokana na umakini mdogo wa CCM kuchagua watu wake, haswahaswa upinzani ukiweza kudhibiti kura zinazoibwa na CCM,hasa ukizingatia ni jimbo pekee ambalo lina mafuta na gesi ya asili ardhini pake. Na hili ndilo jibu sahihi kwamba tangu Tanzania ianze hakuna hata mbunge mmoja aliyewahi kuwa Waziri akitokea katika jimbo la Mtwara mjini. Nakusihi tu ndugu Joel usikate tamaa, jaribu tena uchaguzi ujao huenda ukaonekana tena, manake na sisi tuliokuwa upinzani(CHADEMA) tuna michakato mingi ya kulichukua hili jimbo na tunatunga sheria na kuangalia vipaumbele vya watu wa mtwara . ni mm EKS

  :eyebrows:​
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kiifupi na Kihistoria mji wa Mtwara ni mji wa mwambao ambao upo kusini mwa Tanzania yetu ambao kipindi cha ukoloni ulikaliwa na waarabu toka mashariki ya kati, ni mji ambao unajulikana kihistoria zaidi kwa kuwa na ngome kubwa ya Waarabu pale Mikindani(Museums) . Hauna tofauti na ule mji wa bagamoyo kihistoria ila tofauti t uni kwamba yale majengo ya mikindani ambayo yalistahili kuwa makumbusho na ni vivutio kwetu si wenyewe na wageni, yamekwisha mno kiasi cha kwamba hayana tena thamani na mengi yameshabomoka kwani hayajawahi kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile kwa kipindi kirefu sana. Mji huu ambao kwa sasa unaitwa Mtwara-Mikindani, hapo mwanzo ulikuwa unaongozwa na kutawaliwa na waarabu ambao baadae walijichanganya na wenyeji na kuzaliana, ni mji ambao wakazi wake wengi ni waislam. Nimeanza hivyo kwakuwa huenda watu walio wengi wanausikia tu huu mji labda kwa umaarufu wake kwa kuwa na zao la korosho, na wengine hawaujui kama huu mkoa upo upande gani wa Tanzania(kusini ukiambatana na mipaka ya msumbiji na Malawi).

  Sasa ni hivi, kwa muda mrefu sana,tangu mimi nimezaliwa huu mji unapiga hatua polepole sana na kwakweli mwendo huu wa kobe sijui kama tutafika kule ambako watanzinia wengi watashawishika hata kuja mara moja kuuangalia. Uongozi na usimamizi mbovu wa viongozi ambao wapo kwenye mji huu kwa kweli unakatisha tamaa sana, na hapa ndipo mada yangu inapoanzia. Sina lengo la kuzungumzia udini katika inshu nzima ya uongozi katika jimbo hili la mtwara mjini la hasha ila itanilazimu niongelee swala hili kwani ndio ukweli uliopo na ndio vitu vinavyofanyika pale.
  Tangu kipindi kile cha miaka ya sabini ambapo kulikuwa na mfumo wa chama kimoja hadi hii leo wabunge waliongoza jimbo hili ni Waislamu, kumbukumbu zangu zinaniambia kwamba kipindi kile nilivyozallliwa kulikuwa na Mbunge toka CCM anaitwa Mzee Mkanyama, huyu bwana hata sielewi sasa hivi yupo wapi,baada ya hapo wabunge waliofuatia ninaowakumbuka ni Mpeme, Sinani na sasa ni Murji aliyepitshwa na CCM.

  Mchakato mzima wa kuwapata hawa mabwana kiukweli ni udini ulishamiri katika pande hizi. Ikumbukwe kwamba tangu mwaka 1995 pale Rais Mstaafu BENJAMIN WILLIAM MKAPA kutawazwa kuwa raisi, nlidhani ndicho kitakuwa kipindi kizuri kwa watu wa mtwara kuneemeka kupitia mbunge wake Mpeme kuleta maendeleo jimboni.
  Mchakaato wa kumpata huyu bwana ambae kiukweli elimu yake bila shaka ni chini ya darasa la saba, ulijaa udini sana, nasema hivi kwasababu mkapa alimpendekeza mtu mmoja Mr Kambona achaguliwe kupitia CCM,huyu bwana hakupewa hii nafasi na wazee wa kiislamu kwa ile sababu tu eti huyu bwana ni ‘’kafri’’ kwani ameishi sana Italia ambako akiwatumikia wakristu(alikuwa barozi wa Tanzania nchini Italy),kwahiyo hafai kuongoza mtwara eti tu kuna waislamu wengi, vp inaingia akilini kweli? Ndo hivyo wazee wakaamua na kusema kwamba hatuwezi kuongozwa na kafri. Taabu ilikuwa kwa wale wagombea wenzake waliopita kwenye kura za maoni!,walitishiwa kuuawa na Mpeme kwa mtu yeyote atakayepata ubunge mbali na yeye. Aliwafanyia vibweka wagombea wenzake mpaka akapata ubunge . cha ajabu miaka yote mitano hakuwahi kuzunguza lolote pale bungeni zaidi ya kulala tu. Mwaka wa 2000 uchaguzi mkuu,wale wazee wa kiislamu wakamchagua tena huyu bwana awe mgombea,akapata ubunge na hakuongea lolote bungeni hadi alipomaliza utukufu wake.

  Mwaka 2005 kwa mshangao wazee wa pale mjini wakamtipisha mtu mwenye uraia wa msumbiji ambae tena elimu yake nadhani kama sio chini la darasa la saba basi ni si zaidi ya form four,huyu ni Mr Sinani agombee kwa tiketi ya CCM kama mbunge, akapata ubunge, hakuongea lolote bungeni hadi miaka mitano ikapita. Funika kombe mwanaharamu apite, huyu bwana akagombea tena na akabwaga vibaya na mgombea mwenzake (mfanyabiashara maarufu wa kihindi na sio mwenye asili ya kihindi,hapana, ni mhindi) na hapa ndipo ninapoanza kusema haya.

  Katika kipindi cha kura za maoni, palikuwa na wagombea makini ambao sio maarufu sana kwa jamiikulinganisha na huyu Baniani, lakini ni watu makini na wenye ushawishi mkubwa sana, hawa ni Mr JOEL NNANAUKA na Mr. KASUGULU. Nitamuongelea kiundani huyu Joel kwa kuwa namfahamu kiunandani sana. Nasikitika kusema tena kwamba wakazi wa mji huu wa Mtwara itakuwa imekula kwetu tena kwa muda wa miaka mitano ijayo, ile shilingi yetu tuliyoichezea tayari imeshatumbukia ******. Huyu Joel kitaaluma alisoma shule ya sekondari kibaha na ikumbukwe kwamba ndie aliongoza alikuwa Tanzania One (2002),akamalizia pale kibaha na baadae kujiunga na Bicom pale Mlimani University. Simpigii kampeni lakini kiukweli ni mtu makini mzawa wa pale mjini na ambae ana upeo mkubwa ukilinganishwa na wagombea wezake katika kile kinyang’anyiro,mi naamini licha ya zengwe lililofanywa tena na wazee wa pale mjini kitu kingine kilichomwangusha huyu bwana ni udini, huyu ni mkristu,Anglikana.
  Na hata katika kufanya kampeni ni huyu bwana ambae alifanya kampeni za kisasa zaidi kwa kufungua kipindi maalumu katika redio ya PeaceFm akiongea na wananchi wa mtwara mjini na hata wale ambao walikuwa wanakaa mbali kabisa vijijini ambao hawakuweza kwenda kwenye kampen zake. Ni huyu ambae leo hii anasikitishwa sana si tu kwenye kuenguliwa kwenye kura za maoni bali pia kumsikia mheshiwa Makamba alivyowapa ‘STOP’ wagombea wa CCM kushiriki Midahalo, huyu Joel kwenye kipindi chake redioni aliweza kukusanya maswali yote yaliyotoka kwa wananchi na kuyatolea ufafanuzi mzuri. Siwezi sema kwamba CCM haikuwa chaguo sahihi kwake la hasha,ila kwa mpambanaji kama huyu nadhani angeenda CHADEMA(mtazamo wangu) nadhani angeweka ngome imara sana ya chama kama ilivyotokea kwa mgombe flani (Mr. Osman),na hata angeweza kumuengua huyu Gabachori-chori Murji kwani hakuna mtu asiyejua kwamba huyu bwana hana tofauti na ROSTAM AZIZ na ikumbukwe kuwa katoa rushwa sana hadi kupata kiti hiki cha CCM, ni huyu ambae alishawahi kuwa mbunge wa NEWALA kama sio Tandahimba na leo hii alichowatendea wakazi wa pale, hakuna hata mtu mmoja anayetamani kumuuona na wala kusikia CCM kule, huyu bwana ana fedha chafu (hili ni jembe) na anaweza kufanya lolote la dhuruma na asinyooshwe kidole na mtu yeyote, na ndie mbunge tunayesubiri kuapishwa atuwakilishe mjengoni kwa miaka mingine mitano. Elimu yake sidhani kama kuna mtu anayeifahamu, na siwezi ogopa kamwe kusema kwamba huyu hata elimu ya darasa la saba hana asilani!!

  Upeo wa viongozi wanaopitishwa kugombea kwa jimbo la Mtwara mjini CCM kwa kweli ni mdogo na kwa dunia ya sasa sidhani kama hata wataweza kusimama na kutoa ushawishi wa aina yoyote ile mbele ya watu wasio wavivu kufikiri, na nasikitika ni jimbo ambalo lipo wazi sana kwa wapinzani kulichukua kutokana na umakini mdogo wa CCM kuchagua watu wake, haswahaswa upinzani ukiweza kudhibiti kura zinazoibwa na CCM,hasa ukizingatia ni jimbo pekee ambalo lina mafuta na gesi ya asili ardhini pake. Na hili ndilo jibu sahihi kwamba tangu Tanzania ianze hakuna hata mbunge mmoja aliyewahi kuwa Waziri akitokea katika jimbo la Mtwara mjini. Nakusihi tu ndugu Joel usikate tamaa, jaribu tena uchaguzi ujao huenda ukaonekana tena, manake na sisi tuliokuwa upinzani(CHADEMA) tuna michakato mingi ya kulichukua hili jimbo na tunatunga sheria na kuangalia vipaumbele vya watu wa mtwara . ni mm EKS

  :eyebrows:​
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mzee najua una machungu sana.
  Mji wa Mtwara naujua. Shida ni dini tu pale. Na hiyo dini siku zote haijawahi kuleta maendeleo.
  Nchi yetu inapiga makitaimu kurudi nyuma kwa sababu ile ile ingawa watu hawatki kusema.
  Pole. Tafuteni namna ya kurudisha jimbo hilo kwa nguvu mikononi mwenu. Nyenzo mnazo na mwaweza kuzitumia tarehe 31.10
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ahaaaaa!!! Na ndo Mana Profesa Lipumba amejichimbia huko kwa wiki mbili sasa -- kuna watu wao CUF kule!!!!!
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Na hii mitano itapita maana pale mtwara ahadi ufanyiwa msikitini na ndio inakuwa mwisho. Wanasubiri ahadi nyingine tena miaka mitano ijayo. Wana kila opportunities lakini maskini wa kutupa. Shauri yao. Wasubiri yule mama anaevaa baibui kila siku waone kama atawasaidia labda.
  Kama mnabisha niliwahi kuweka picha hapa last year. Search uangalie.
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na hii ishu ya udini linapokuja suala la siasa za Mtwara. Na inasemekana yule mama waziri wa pale ikulu ndio anayeshikilia bango makafir wasigombee.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  (Hakuna haja sana ya kujadili mambo ya tofauti za kidini). But ni kweli Lipumba yuko huko kwa sababu ya uislamu tu na si kitu kingine.
   
 8. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  udini huwenda ukawa upo hapo mtwara mjini tu..lakini pia sio udini pekee unaozuia maendeleo...pia mtwara kuna majimbo ambayo yameongezwa na wakiristo miaka mingi sana lakini hakuna maendeleo yeyote...je huko nako tatizo ni nini?
  mfano ni masasi...mrope.
  newala....mkuchika
  nanyumbu...mkapa and family
  lulindi.....anna abdalla miaka kibao kabla hajampa nduguye kumchae
   
 9. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CHADEMA NI CHAMA CHA WAKIRISTO, hakuna lolote watakalo wafanyia Wa TZ zaidi ya udini, hakuna maendeleo mutakayo waletea wa TZ zaidi ya kutumia fedha za walipakodi kwa kununulia pombe na zawadi siku za krismas, mwaka mpya na pasaka! historia imejionyesha hivyo! tangu tumepata uhuru nchi hii imeongozwa kwa muda mrefu na wakiristo! mfano Julius Nyerere alitawala miaka 24 akiwa Rais na miaka 14 alitawala TZ nyuma ya pazia!, na Benjamin Mkapa alitawala miaka 10 kama rais na hakuna maendeleo yoyote tuliyopata ktk uongozi huo wa kikristo zaidi ya kuwa maskini zaidi, wajinga zaidi, wagonjwa zaidi, majambazi zaidi, nk.

  Sasa ole wetu wa TZ tutakuwa tumefanya kosa kubwa kuwarudisha Mapadre watuongoze tena! CHADEMA ni hatari, wana udini na wanachuki na dini zingine tusiwape kura hata moja na Padre wao tumtose kwa kuupoteza ubunge wa Karatu na ikulu ataisikia kwenye bomba! chama makini ni CUF na Rais anaefaa ni Profesa I. LIPUMBA!
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mtwara wanajua matatizo yao na solution zao, tatizo ni ushkaji tu!!! hawana haja ya kulalama wakati wanajua shida zao

  tuwaache mtwara waamue kusuka au kunyoa na wakibaki nyuma, then hawahitaji huruma yoyote
   
 11. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  dini gani hizo zitaje basi
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu wewe huelekei kuwa na visiasa kiduchu kama hivyo...unaaibisha heshima yako...Lol!
   
 13. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  We mkuu huyu SINANI si ni MWARABU kabisa au nakosea?namjua sana na hata watoto wake nawafahamu sana wanaishi kariakoo...ni mfanyabiashara pia lkn mhhhh hivi elimu yake ikoje vile maana watoto wake hata mmoja shule hana zaidi ya kuchezea magari,inasikitisha wakati mwingine watoto wake walikuwa wanatumia gari la ubunge na bender juu utadhani ndo SINANI...makubwa huko MTWARA.
   
 14. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Mwinyi mbona hujamtaja mzee au keyboard imeteleza?huyu hapa ndg yako Kikwete sasa ndo anamaliza nchi waziwazi,anasain mikataba akiwa chumbani kama mwinyi,anaifanya ikulu kama yake na familia yake,Mwinyi mlimpiga wenyewe juzi juzi hivi ilikuwaje vile?
   
 15. E

  Eddie JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sizinga mara ya mwisho kuagalia Baniani sio Muislamu sasa huo "udini" ( isomeke uislamu ) umetoka wapi? Mdau hapo juu ka orodhesha majimbo ya huko huko Mtwara ambayo miaka nenda miaka rudi wabunge wakristo tena wakapata na uwaziri akina Anna Abdallah, Mkuchika, nk je kuna maendeleo?

  Ni suala la demographic tu kwani mikoa kama Mbeya, Iringa nk kuna majimbo hayaja wahi tawaliwa na waislamu je ni udini?.

  Tafuta namna bora ya kum (ji) pigia debe Mr JOEL bila kupanda chuki za dini
   
 16. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,454
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Pammoja na matatizo yote upinzani kwa mikoa ya Mtwara ,Lindi,Ruvuma ni ngumu kwani wananchi hawaamini chama kingine ila Chi Chiem.Kupanga ni kuchagua
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ..... mbaazi kusingizia jua
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Sep 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ukitaka kuwajua vizuri Wadanganyika ni swala linapofikia hapa. Hii ni dalili tosha kabisa ya kuonyesha kwamba waliochanganyikiwa ni sisi tunaopenda sana kuhukumu watu wengine kwa sababu tu ya Udini. Ebu nambieni ni jimbo gani hapa Tanzania huchagua mtu asiyekuwa wa kabila lao? sidhani kama yapo mengi sana lakini mbvona hatusema Uchaguzi huu umejaa Ukabila. Nenda Mbeya ukiwa sii Mnyakyusa kama utashinda Uchaguzi, Nenda Kilimanjaro, Kigoma, Tabora na mikoa karibu yote ujaribu kugombea hali huna nasaba yako pale kama utachaguliwa. Je, kwa nini hii isiwe Ukabila ila pale tu tunapochagua sisi kuona.

  Wakuu zangu, Duniani kote uchaguzi wa mbunge hufuata Asilia ya mgombea hata kama ni mhamiaji anakubalika vipi na wananchi wao na yeye anatambua vipi mahitaji yao. Kabila na dini yake ni moja ya sababu ambazo hazitajwi lakini zinachukua nafasi kubwa sana ktk uteuzi wa mgombea. Leo hii mimi hapa hata nikiwa Marekani, UK, France na hata Ujarumani naweza kabisa kuukosa Ubunge kwa sababu sina ukaribu nao hata kama nimesoma hadi darini. Naweza kutochaguliwa kwa sababu ni mweusi, muislaam au hata sina uzoefu wa tamaduni zao kuwa sababu. Elimu ya mtu sio kigezo cha Ubunge bali ukaribu wa mhusika na wananchi wenyewe na jinsi gani wananchi wanampokea mgombea. Na wala kuwa kabila au dini moja haina maana mtu huyo ni mbora zaidi ya asiyekuwa. Lakini pamoja na yote ni vigumu sana kushinda Uchaguzi wowote ikiwa mgombea sio wa kabila au dini ya wananchi walio wengi.

  Kama katiba yetu inavyosema Nchi yetu haina dini isipokuwa wananchi wake ndio wenye dini. Basi na tuelewe kwamba hao wananchi wenye dini wanaweza fanya maamuzi ya kulinda utamaduni wao ikiwa ni pamoja na dini au Kabila hii inafanyika hata Marekani au Uingereza. Udini unapozungumziwa ni pale nchi au chama kinapofanya maamuzi yake kwa kufungamana na dini moja lakini wananchi wenye dini wanaweza kabisa ku practice maamuzi yao kwa kutazama dini au hata kabila la mgombea na isiwe Udini au Ukabila..Labda niwaguse nyie wenyewe.. mnapomchagua mtu wa kua (mke/mme) wa dini yao huwa mnafanya Udini?

  Kwa hiyo wananchi wa Mtwara wanayo haki ya kuchagua mgombea kwa jinsi wanavyotaka wao. Hao wagombea kama kweli walikuwa makini wasingejiunga na CCM. Hilo kwanza kwani binafsi naamini kuwa mpiganaji yeyote anayeweza kuelta maendeleo Mtwara ni yule atakayeweza kuona jinsi Mkoa huo ulivyoachwa na CCM kwa zaidi ya miaka 30. Mkoa umesahaulika kabisa na sidhani kama Mbunge mmoja anaweza peleka mabadiliko huko. Huyo Makamba na mwanaye hawa wote ni Papa, chakula chao ni samaki wadogo. Kinachofanyika ni kuendeleza kuwafum,ba macho wananchi wa Mtwara hali mkoa huo umesahaulika miaka nenda rudi.

  Wamepita wabunge wasomi wenye dini tofauti na makabila tofauti huko Mtwara lakini hakuna kati yao alofanya la maana chini ya utawala wa CCM. Hivyo sii dini wala kabila lao ndilo lenye kuwawezesha Mtwara isipokuwa ni uwakilishi mzima wa chama tawala CCM ndio umewasahau wana Mtwara. Mgombea yeyote makini asingejiunga na CCM bali angejiunga na CUF hata kama yeye ni Mkristu. Kuacha kujiunga na CUF kwa sababu ni chama cha Waislaam inamfanya mgombea mwenyewe kuwa mdini vile vile kwani CUF haiongozwi na Kuran bali katiba.
   
 19. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Udini? Ukabila?....na kweli mbona safari hii Wahindu na waarabu wengi wametumia mipesa mingi tu na kuomba uongozi kupitia CCM? nafikiri kuna mkakati maalumu wa kui-BINAFSISHA CCM nyie subirini tu
   
 20. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Jamani if I can ask, ni lini Kambona alikuwa Balozi huko Italy? Kwa ufahamu wangu Kambona alikuwa ni mfanyakazi wa ubalozi wa Italy lakini hakuwahi kuwa balozi.

  Tiba
   
Loading...