Kunani EU? Ursula alipuka "EU lazima 'ichukue hatua' dhidi ya kuumizwa na Marekani"

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,601
6,014
TARATIBU EU DAWA INAANZA KUINGIA.

IKUMBUKWE JANA RAIS WA BARAZA LA ULAYA ALITAPIKA NYONGO PIA: Rais wa Baraza la Ulaya naye atapika nyongo: "EU inateseka zaidi na mzozo wa Ukraine kuliko USA"

Soma:
Mpango wa uwekezaji wa Joe Biden unaweza kutishia viwanda vya umoja huo, Rais wa Jumuiya ya Ulaya amesema

Rais wa Jumuiya ya Ulaya Ursula von der Leyen alionya Jumapili kwamba ili kuweza kushindana na mradi wa 'green energy' unaofadhiliwa na serikali ya Marekani, EU lazima "ichukue hatua" na kuongeza msaada wa serikali kwa makampuni yake yenyewe.

Mradi huo uliotiwa saini kuwa sheria na Rais Joe Biden mnamo Agosti, iliyoitwa Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei (IRA) ni - licha ya jina lake - kifurushi cha matumizi cha dola bilioni 738 ambacho kimetengwa na USA na dola bilioni 391 kwa miradi ya sekta ya nishati ya kijani na mazingira rafiki ya hali ya hewa, ikijumuisha dola bilioni 270 za motisha ya ushuru. Hapo awali ikisifiwa na waliberali wa pande zote mbili za Atlantiki, von der Leyen sasa anaona kitendo hicho kuwa tishio kwa tasnia ya Uropa.

IRA inatoa mapumziko ya kodi kwa watumiaji wanaonunua bidhaa za Marekani, na watengenezaji wanaozalisha bidhaa hizi nchini Marekani, hili linaweza "kusababisha ushindani usio wa haki, pia unaweza kufunga masoko, na hivyo kugawanya mifumo muhimu ya ugavi," aliuambia mkutano wa wanafunzi katika chuo kikuu katika Mji wa Ubelgiji wa Bruges.

Kwa motisha hizi kwa upande mmoja wa Marekani, na mapambano ya EU dhidi ya vikwazo mifumo ya ugavi na pia kupanda kwa gharama za nishati kunakochochewa kwa kiasi kikubwa na mzozo wa Ukraine kwa upande mwingine, IRA inaweza kuliweka bara la Ulaya katika hasara, aliendelea.

Ushindani kati ya Marekani na EU "lazima uheshimu uwanja sawa," alisema. "Lazima tuchukue hatua kusawazisha uwanja, ambapo IRA na hatua zingine husababisha uharibifu kwetu."

Kwa maana hiyo, von der Leyen alisema kwamba EU lazima iongeze misaada ya serikali kwa viwanda vyake, na kuwekeza katika nishati mbadala, huku akiishawishi Marekani "kushughulikia baadhi ya vipengele vya IRA vinavyoiumiza zaidi ulaya" .

Mapema Jumapili, mkuu wa kamati ya biashara ya Bunge la Ulaya, Bernd Lange, alisema kuwa kuishinikiza Marekani kuandika upya kitendo hicho ni kupoteza muda
, na kwamba EU inapaswa kuwasilisha malalamiko yake kwa Shirika la Biashara Duniani badala yake.
 
Kikubwa tuendelee kuwaombea warusi ,ule mkong'oto anaotembzewa huko front line ni WA kikatili kwa kweli 🥱🥱
 
🇫🇮 PM,Europe inaihitaji zaidi USA kuliko otherway round, but anyway Tanzania yangu nayo ina mambo mengi ,mpaka wangu na Mozambique 🇲🇿 unahitaji more attention kuliko haya ya Ukraine 🇺🇦 na wavamizi Russia 🇷🇺.
 
Hili ndilo vugu vugu la kweli kuelekea katika ile vita kuu ya 3 ya Dunia
 
Ninachowapendea hawa Europe na USA kwenye interest zao wakisuguana wanatiana adabu kama wakati wa Trump na zile tariffs zake kwa bidhaa za Ulaya...lakini akitokea adui kama Russia wanaungana tena huko wanakua wamoja japo Wana misuguano Yao.
 
Ulaya nao wahuni sema walitulizwa kwa muda na muingereza na best yake marekani......kuna mataifa kama ufaransa na ujerumani hawa jamaa ndo wanajiona kama vidume wa ulaya......shida ya ubepari ukishakanyaga maslahi yangu hatuna urafiki jamaa wameshaona mmarekani pamoja na muingereza wanawachezea changamsha bwege.

Marekani anafaidika sana na hii hali ya sasa hapo ulaya kapata soko la lazima la gesi na nishati nyingine tena anawauzia kwa bei kubwa....anaeumia upande wa nishati ni mjerumani sababu kwa ulaya ndo ana uchumi mkubwa wa viwanda huyu dawa ikiingia vizuri lazima atikise kiberiti,,,halafu kwa sasa mmarekani anataka kutoa incentive kubwa kwa viwanda nchini kwake.

Ulaya wanahofia jamaa anavuta viwanda vyao vingi nchini kwake kama vile alivyocheza mchina kwa ulaya na marekani mwanzoni wakati anakua, baadae wao watakua ni wateja na soko la kudumu la marekani, huku mfaransa nae hali ni hivyo hivyo ndani kwake kuna hali mbaya ukiongezea mrusi huku yalipokua makoloni ya ufaransa kwa africa anamtibulia ugali wake

Ufaransa part ya utajiri wake mkubwa anaupata kupitia makoloni yake ya zamani kwa kuweka vibaraka na kukwapua mali, sasa huku mrusi kwa kutumia wagner anamvuruga (hii wagner ndo anayoitumia africa, hapo syria na hata ukraine...aliusoma mchezo wa Blackwater ya marekani nae ka apply), hali ikiwa mbaya sana watakulana nyama wenyewe kwa wenyewe hao wamagharibi
 
Uchambuzi mzuri. Swali la msingi nini kauli kama sio msimamo wa sisi Waafrika. Usije kutumia ule msemo "wapiganapo tembo au hata kama wachezapo zinazoumia ...."
 
Uchambuzi mzuri. Swali la msingi nini kauli kama sio msimamo wa sisi Waafrika. Usije kutumia ule msemo "wapiganapo tembo au hata kama wachezapo zinazoumia ...."
Waafrika tunatililika, sie kwa waliotutawala naona tulichojifunza na kukomalia ni dini tu maana hata waarabu na nchi nyingine za asia zilitawaliwa ila walipo na sie tulipo noma. Makanisa ulaya yanakufa afrika ndo yanastawi kama uyoga.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom