Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Kunambi alalamika kwa Kikwete
Chief Kunambi amefanya kikao cha ndani na Kikwete nyumbani kwake Ubungo Msewe. Katika kikao hicho amemlalamikia Kikwete kuhusu kuwasau waasisi wa TANU na wapiga uhuru pamoja na wastaafu kwa ujumla. Lakini pia amemweleza Kikwete uchochezi unaofanywa na CHADEMA kwa wananchi wa eneo hilo hususani kuhusu mitambo ya Richmond ambayo haiko mbali sana na nyumbani kwake. Amemtaka Kikwete kuchukua hatua kuhusu wahusika wa Richmond kwa kuwa suala hilo limekuwa kero kwa wanachama wa CCM kila wanapopita. Tukivaa mavazi ya chama, tukipita mitaani tunaitwa Richmond, alisema Chifu Kunambi. Kitongoji cha Msewe ni moja ya vitongoji vyenye upinzani mkali ambapo katika uchaguzi wa 2005 kura nyingi zilikwenda kwa CHADEMA. Wadadisi wa mambo wanasema haya ni matokeo ya uchochezi unaondelea kupitia nyaraka ambazo zinasambazwa mitaani hali ambayo kama haitazibitiwa mapema inaweza kuchochea wananchi kufanya hujuma katika mitambo hiyo ya umeme.
PM