Kunambi alalamika kwa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunambi alalamika kwa Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Jun 20, 2008.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kunambi alalamika kwa Kikwete

  Chief Kunambi amefanya kikao cha ndani na Kikwete nyumbani kwake Ubungo Msewe. Katika kikao hicho amemlalamikia Kikwete kuhusu kuwasau waasisi wa TANU na wapiga uhuru pamoja na wastaafu kwa ujumla. Lakini pia amemweleza Kikwete uchochezi unaofanywa na CHADEMA kwa wananchi wa eneo hilo hususani kuhusu mitambo ya Richmond ambayo haiko mbali sana na nyumbani kwake. Amemtaka Kikwete kuchukua hatua kuhusu wahusika wa Richmond kwa kuwa suala hilo limekuwa kero kwa wanachama wa CCM kila wanapopita. “Tukivaa mavazi ya chama, tukipita mitaani tunaitwa Richmond”, alisema Chifu Kunambi. Kitongoji cha Msewe ni moja ya vitongoji vyenye upinzani mkali ambapo katika uchaguzi wa 2005 kura nyingi zilikwenda kwa CHADEMA. Wadadisi wa mambo wanasema haya ni matokeo ya uchochezi unaondelea kupitia nyaraka ambazo zinasambazwa mitaani hali ambayo kama haitazibitiwa mapema inaweza kuchochea wananchi kufanya hujuma katika mitambo hiyo ya umeme.

  PM
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Anakumbushia Pension yake huyo labda wamemsahau sana si vibaya kubwaka kidogo.....
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  na yatendeke kama ulivyonena......
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  TATIZO LA HAWA WANAOITWA WASISI NI HILI, HAWATAKI KUTAMBUA KUWA MUDA WAO UMEISHA

  ukienda zimbabwe ni hawa hawa hawtaki mabadiliko kwa kisingizio cha kuasisi

  ukienda zanzibar ndo hawa hawa, tunayaenzi mapinduzi matukufu

  sasa, kama afrika itakumbatia hawa watu hatutaenda mbele. ni vema kuwapuuza wao na mvi zao, hawana jipyaa

  shaban robert "zamani elimu haikuwepo, mvi zilitumika kuhesabu wenye busara, lakini siku hizi elimu imekuwepo, si swala la kuhesabu busara ya mtu kwa mvi zake
   
 5. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  natamani ningekuwa na uwezo nikawatia vijana hamasa, wakachukua mabomu ya petroli wakaanza na IPTL, hiyo mitambo ya richmond, na ningekuwa na uwezo zaidi wa kisayansi nikazima minara yote ya vodacom, na caspian.
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Duh!
  Tuhuma za ufisadi zishaanza kuitwa UCHOCHEZI?
  Kaazi kweli kweli.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Joto Masaka wanalionja wenzio huko mtaani...Na wewe unadai PENSION...Ama kweli siku ya kufa nyani...
  Sasa na wewe hilo JOTO wezio wanalolipata huko mtaani we hulipati hapa JF?
  Unatakiwa ujue kuwa si lazima watu kutoka nje wafanye mambo flani flani ama walie ndio ujue machungu ya Mtanzania.
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Iwa wanasema tuwe tunasikiliza ushauri wa wazee lakini sometime iwa unakuwa pumba tu haufai.Sasa huyu mzee alikuwa anakumbushia pension yake.Sasa kama wanachama wa CCM wamelala kwa nn wasikejeliwe?Ukiangalia wamemchagua Keenja huyo lakini toka awe Mbunge hata sura yake hajawahi kuipeleka kwa wananchi angalau kuzuga tu.Miundo mbinu mibovu kupindukia jimbo la Ubungo.
  Wanahaki kuwazomea kama Mbunge walio mchagua analala hata bungeni kwa nini wasiwakejeli?
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wapiganaji wa ANC waliitwa "terrorist" na makaburu, Waafrika waliwaona "heroes"

  Nani mchochezi na nani ni muhamasishaji wa jamii? Inategemea na nani unamuuliza swali.

  As that artical poet Macka B would have it,

  "Who are the terrorists? Who are the heroes? x 2
  Double Standards
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Huko Arusha walivamia ofisi za CCM na kukomba mamilioni kibao!
  Sasa mzee wa watu anaona haya mambo licha ya kwamba walipigana kwa ajili ya nchi yao lakini Mafao ya hawapewi...Sasa wananchi wanataka kuwavamia wakidhani na wao ni wanamtandao mafisadi...Unajua kwasababu mwenyekiti wao ameshasema hakuna fisadi ndani ya chama...Then wananchi watatumia ile falsafa ya...WALK LIKE A DUCK,TALK LIKE A DUCK..HELL YEAH THATS A GADDAMN DUCK!
  SHOOT IT!
  NO MORE INDIGNITIES AND AN UNNECCESSARY SUFFERINGS FROM THE PEOPLE...Who are actually blessed with abundants of Natural wealth from God!

  Mungu huchukia kama watu wanakufa huku wao ni matajiri!
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  unaposhindwa kuonyesha uwezo wako wa kuongoza nchi kwa wananchi wako, matokeo yake ndo kama haya.
  kila mwenye uwezo wa kukutisha anakutisha, mpaka vizee vitandani na watoto barabarani.

  kikwete act up now, or else utatukanwa mpaka na watoto wadogo
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  Jun 21, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  rais wetu kwa kutembelea wagonjwa ,wazee na wastaafu ..namsifu..

  laiti kama angeweza kuwapa wastaafu wote pension kwa wakati..wakiwamo wale wa afrika mashariki wanaoshinda geti la ikulu kila siku...ningempa kudos zaidi.....nafikiri mzee kunambi kama ametumia busara atakuwa ameomba mafao kwa wastaafu wote kwa ujumla ..maana hata wale wazee wa relwe na bandari wanalingana naye........

  pia ingekuwa ziara za rais hospitali zinaleta dawa na vifaa....na kuondoa adha kwa maskini ningefurahi zaidi..

  kinachoonekana wazi kwa rais wetu ni kuwa anapenda raia zake ..ila hana uwezo wala namna ya kutuvusha...sasa unajua kutupenda peke yake haitoshi..kama hana njia!!..wanasema "if wishes were horses beggars could ride..."

  pia niwakumbushe usemi wa mzee mwinyi...."MASKINI HAWAPENDI WANAWE...."...akimaanisha kuwa mzazi maskini anampenda mwanawe lakini asilani ataonekana hampendi..kwa sababu hawezi kumvika nguo nzuri,zawadi nono.,chakula kinono..outing za hapa na pale...kama mtoto wa familia ya kitajiri ambaye ndio ataonekana anapendeka kwa sababu ya fahari hizo...lakini rohoni maskini anaweza kuwa aaanampenda mwanawe kuliko jirani yake tajiri.....
   
 13. M

  Masatu JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu yarabi nafsi hapo Mzee Kunambi kivyake hao wastaafu wa community watajiju!
   
Loading...