Kunakucha au Kumekucha ,hakuna tena kulala si shwari tena - Tume ya uchaguzi huru

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Sasa sio shwari tena,Tanzania inahitaji Tume huru ya uchaguzi ,CCM wakitaka au wasitake hii sio nchi yao na kama haitoshi watambue hawana hati miliki, Tume huru ya uchaguzi ni lazima kuliko kifo maana kifo kinaweza kuchelewa ,ila Tume huru inahitajika sasa na hakuna sababu ya kuchelewa na wakati huo huo msukumo wa Katiba mpya kwani WaZanzibari wamebanwa na katiba iliyopo hawafurukuti,muungano gani huu usikwisha makelele,hivi hatukusoma hatujui kujenga kitu kizuri ? Na kila upande ukafurahia ?

Vyama vya upinzani ndio sehemu ambako sauti zinahitajika na sio kusubiri kutangazwa tarehe za uchaguzi ndio na wao eti wanasema tume sio huru,ni ulimbukeni na kuwafanya wafuasi wao mazwazwa.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,730
2,000
Naunga mkono hoja. Bila Tume Huru ya uchaguzi, vyama vikuu vya siasa kama Chadema na vinginevyo, vitangaze mapema kususia uchaguzi mkuu ujao.
 

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
5,640
2,000
Ndani ya CCM wapo wanaopenda kuwepo kwa tume huru lakini waoga kujionyesha. Akitokea rais akasema utaona harakahara wakijitokeza na kusifia.
Hata viongozi wanapima upepo lakini tume huru ni mhimu kukiwa na kati .mpya pia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom