Kunahitajika kweli kufanya utafiti kuhusu pato dogo la Watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunahitajika kweli kufanya utafiti kuhusu pato dogo la Watanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, May 29, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,428
  Trophy Points: 280
  Wachumi washauriwa kutafiti kuhusu pato dogo Saturday, 28 May 2011 10:54

  Gedius Rwiza na Furaha Maugo
  Mwananchi
  MLEZI wa Taasisi ya Sera Afrika Mashariki (EPF), Dk Diodorus Kamala, amesema changamoto inayowakabili wachumi na watafiti, ni kuangalia tatizo la kutokuwapo kwa uwiano sawa kati ya ukuaji uchumi na pato la mwananchi.

  Dk Kamala alisema taarifa ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) ya Aprili mwaka huu, inaonyesha kuwa uchumi wa nchi za Tanzania, Uganda na Rwanda, unakua kwa kasi miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Alisema taarifa hiyo inaonyesha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2005/6. uchumi wa Uganda ulikua kwa asilimia 8.3 wakati wa Tanzania, ulikua kwa asilimia 6.9 na Rwanda kwa asilimia 7.9.

  Dk Kamala alisema hata hivyo katika kipindi hicho pato la wananchi katika nchi hizo lilikuwa bado la chini, ilhali Kenya ambayo uchumi wake haukui kwa kasi, pato la wananchi wake likiwa la juu.

  Alisema utafiti huo haukuhusisha nchi zenye idadi ya chini ya watu milioni tisa.Akizungumza kwenye majadiliano ya pamoja yaliyoandaliwa na Shirika la Policy Forum, Dk Kamala alisema tafiti zinapaswa kubaini chanzo cha Watanzania kuzidi kuwa maskini wakati uchumi unaonekana kukua kama Rwanda na Uganda, ambazo pato la raia wake ni la juu.


  "Unajua katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania inaonekana uchumi wake kuwa wa juu, lakini Watanzania vipato vipo chini, kuna kila sababu ya kufanya utafiti na kubaini chanzo cha tatizo hilo, ikiwamo ni pamoja na kupata funzo kutoka Rwanda kuhusu namna walivyowezesha uchumi wao kukua kwa haraka," alisema Dk Kamala.
  Alisema viongozi wa EAC wanapaswa kutenganisha siasa na shughuli za ujenzi wa uchumi, ili kuleta mabadiliko.

  Dk Kamala pia aliwataka viongozi EAC kuhakikisha kuwa wanatimiza makubaliano ya jumuiya hiyo, ikiwa ni pamoja na kusimamia suala la ushuru wa wa forodha.


  Aliwataka Watanzania kujenga imani kwa wanajumuiya na kwamba, baadhi ya watu walikuwa hawaoni umuhimu wa kuanzishwa kwake wakihofia rasilimali zao kukwapuliwa.Alisema mpango wa kufikia malengo ya jumuiya hiyo hauhitaji kwenda haraka na badala yake, unatakiwa kwenda hatua kwa hatua.

  Dk Kamala, ambaye alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano, alisema kama suala la uchumi halitaangaliwa kwa umakini matokeo yake, hata wawekezaji watakimbia na kwenda katika nchi zinazojali zaidi maendeleo ya kiuchumi .
  ~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**

  Chanzo cha Watanzania kuwa maskini ni Viongozi wabovu walio madarakani ambao ni mafisadi na wanaotumia ufisadi kujilimbikizia mali, kujilipa mishahara na marupurupu ya juu na kuwasahau wakulima na wafanyakazi, kusaini mikataba mibovu ya rasilimali zetu ambayo inawaneemesha wageni na mafisadi walio madarakani na kutokuwa na utawala wa sheria wa kuwashughulikia ipasavyo mafisadi mbali mbali waliojivisha ngozi ya uongozi ili kuendelea kujilimbikizia mali kwa njia za kifisadi ambao wanaendelea kufurahia utajiri wao uliopatikana kwa njia za haramu.


   
Loading...