Kuna yeyote anamfahamu huyu nabii David Stefano Mpanji wa Mbeya?

Afisa Mteule Drj 2

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
3,586
3,935
Huyu bwana nabii anaitwa david Stefano Mpanji ana unguruma sana huko Mbeya na anapigwa sana vita na watumishi wengi wa mungu huku na yeye akiwa ni mrusha madongo mzuri kwa wenzake.

Kanisa lake linaitwa GMCL pia ana radio ambayo pia inaitwa GMCL ambako huko ndio hubwabwaja sana na si kumhubiri kristo kama ambavyo tunategemea na hata lugha zake sio kama za kilokole kama tulivyozoea bali ni za kibabebabe.

Kanisa lake ni la miujiza miujiza ya ajabu ajabu pia yeye ni Muuza maji na mafuta kwa waumini wake ambapo uwa anasisitiza kuna uponyaji kwenye hayo maji na mafuta yake.

Kuna yeyote ana historia ya huyu bwana au ana mfahamu vizuri. Ninajua JF ina watu wengi na inafika mbali mno najua hawakosekani watu wanaomfahamu Huyu jamaa.
 
Kitendo tu cha kufanya biashara ya maji na mafuta, hadi hapo kuna mashaka.

Uponyaji huwa hauuzwi kwa sababu tulipewa bure na Mungu mwenyewe
Ikiwa Mungu amemwelekeza mtu aponye kwa maji au mafuta, huyo huyo MUNGU lazma atoe njia ya kupatikana bure.

Ila Kama ulivyosema uliambiwa maji shilingi 100 ya uponyaji ujue wazi so MUNGU Yesu ni formula ya MUNGU mwingine
 
Kwa hitimisho nasema Mpanji ni mganga kama waganga wengine.
Au nasema uongo ndugu zangu
Anaweza akamwambia mtu "nawaona watu watatu wamekaa kwenye kifua chako" kwenye kubwabwaja Kwake story zake kuu ni wachawi, makaburi, maiti, majini, waganga wa kienyeji na mambo mengine ya giza giza hana kabisa msisitizo wa watu kumfuata kristo bali msisitizo wake ni watu kukombolewa na kukombolewa kwenyewe ndio huko sijui kuombewa na kutumia maji na mafuta.
 
Ikiwa Mungu amemwelekeza mtu aponye kwa maji au mafuta, huyo huyo MUNGU lazma atoe njia ya kupatikana bure.
Ila Kama ulivyosema uliambiwa maji shilingi 100 ya uponyaji ujue wazi so MUNGU Yesu ni formula ya MUNGU mwingine
Na kama nabii wahitaji watu waponywe kupitia maji au mafuta.

Unaelekeza tu watu waje na maji au mafuta toka majumbani mwao, then nabii uviwekee mikono watu warudi na vitu vyao hivyo makwao.

Zamani enzi za mikutano ya injili, wale wahubiri walikuwa wanawaelekeza watu waende na vitu kama nguo, leso, maji n.k toka makwao.

Vitu hivyo vilipoombewa na hata watu waliporudi navyo makwao vikatumika kuwawekea walio waginjwa na dhaifu nao wakapona na kupata afya.
 
Anaweza akamwambia mtu "nawaona watu watatu wamekaa kwenye kifua chako" kwenye kubwabwaja Kwake story zake kuu ni wachawi, makaburi, maiti, majini, waganga wa kienyeji na mambo mengine ya giza giza hana kabisa msisitizo wa watu kumfuata kristo bali msisitizo wake ni watu kukombolewa na kukombolewa kwenyewe ndio huko sijui kuombewa na kutumia maji na mafuta.
Anapo niacha mdomo wazi ni kua mda mwingine anaombea mtu hata akiwa mbali, ila tu upeleke picha ya mhusika.

Hapo Ndo natosha kabisa
 
Na kama nabii wahitaji watu waponywe kupitia maji au mafuta...

Unaelekeza tu watu waje na maji au mafuta toka majumbani mwao, then nabii uviwekee mikono watu warudi na vitu vyao hivyo makwao...

Zamani enzi za mikutano ya injili, wale wahubiri walikuwa wanawaelekeza watu waende na vitu kama nguo, leso, maji n.k toka makwao...

Vitu hivyo vilipoombewa na hata watu waliporudi navyo makwao vikatumika kuwawekea walio waginjwa na dhaifu nao wakapona na kupata afya...
Kuna mtu siku moja redioni alipiga simu kwenye kipindi kuuliza hilo jambo sina kumbukumbu huyu bwana nabii alijibu nini ila nakumbuka alitetea hayo maji yake. Huwa anayaita damu ya Yesu.
 
Anapo niacha mdomo wazi ni kua mda mwingine anaombea mtu hata akiwa mbali, ila tu upeleke picha ya mhusika.
Hapo Ndo natosha kabisa
Na si picha tu anapokeaga hata nguo nadhani za walio mmbali ziombewe mfano ndugu wanataka ndugu yao mlevi aombewe aache ulevi na huyo ndugu mlevi hataki kuja hapo kwa mpanji,wanachofanya ndugu zake wanaweza kuchukua nguo yake na kuipeleka Kwake mpanji aiombee.
 
kwa jinsi nilivyojifunza mambo ya kiroho ni magumu sana,wito hasa wa Mungu unategemea na uwezo wa mtu wa kuelewa au elimu yake,mfano Mtume Paulo alikuwa na elimu kubwa sana tofauti na wakina Petro ndio maana akapewa nafasi ya kuandika karibu vitabu nusu kwenye biblia
kwa mfano Gwajima ana wito lakini ni ngumu sana kuelewa kwa akili ya kawaida inabidi utulie sana
Mungu anampamtu wito halafu mtu anaufanyia kazi kutokana na uelewa wake,kuna kiburi na majivuno na ujinga hayo nimeyaona kwa watumishi wengi wa Mungu
kama mkristo inabidi utumie akili sana kumwelewa mtu mwenye wito
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom