Kuna wizi umetokea, ni mwanasiasa yupi wa kuaminiwa?

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,074
2,000
Huku mtaani kuna wizi umetokea, mbiu imepigwa na mwizi alikuwa anakimbia, watu wenye ghadhabu walitoka nje lakini hawakumfukuza wala kumzuia mwizi aliyekuwa anapita katikati yao.

Mwizi ameacha kukimbia, ameamua kutembea huku akigawa bakshishi vitu alivyoiba kwa wapita njia na wanaoshangaa.

Ajabu, wanaotuhabarisha juu ya tukio hilo wameacha kuliita tukio hilo wizi – wanatuambia eti, HAKUNA MKATE MGUMU KWA CHAI! Habari hii imechangamsha baraza zote leo - jamii ya ajabu!
 

rsvp

JF-Expert Member
Dec 13, 2012
720
500
Aisee!!!,

Yaani ,kila mtu yupo kimyaaa!,utafikiri hakuna kitu kilichotokea.

Yaani,kila mtu yupo kimyaa,nani aseme ukweli,kila mtu anaamini wenye maamuzi wanajua!

Yaani, kila mtu yupo kimyaa,watu wakiwa wawili wanaongea,akiongezeka mtu wa tatu kila mtu anakuwa kimyaa!
 

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,789
2,000
this time, tuna gawa mbao, (kama noma na iwe noma kwani nini), hatuiachii mashua izame ki kukuu huku tuna iangaliaa tuu…….
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom