Kuna wazungu, Waarabu, na wahindi ambao ni Watanzania

Kwangu mimi mtanzania pekee ambaye hana ngozi nyeusi ni Mabala wa Mabalaa mwandishi wa Raiamwema. Huyu ni mtanzania kwa lugha, harakati na uzalendo wake. Sio mniletee mhindi wa maghorofa ya posta mpya ambaye hata Kiswahili hajui mniambie ni mtanzania.

Richard Mabala:
Pic+mabala.jpg
Kabisa! Si mwoga na anawasilisha maoni yake bila woga.
 
Asante kwa kuongezea, twasubiri mambo ya Dual Nationality sasa, tuirudishe ile brain iliyotekwa nje..
Mkuu. Simfahamu hata Mtanzania mmoja aliokataa kuchukua uraia wa nje. Wazawa wote ninaowafahamu ndani na nje ya nchi wana uraia wa nchi nyingine.

Hata viongozi wa juu na watoto wao wengi tu wana uraia mwingine.

Watu wanaangalia maisha kujitoboa siyo mambo ya uzalendo. Huwezi kuwa mzalendo ukiwa na njaa nje.

Hizo sheria hazisumbui zaidi ya kutozwa viza kuja nyumbani. Hata wakibadili, sioni mabadiliko katika uchumi unaoendeshwa na serikali ya kibabe isiyoheshimu sheria.
 
Kuna dhana inazidi kujengwa na kubebewa bango kwamba watanzania ni wale tu wenye ngozi nyeusi peke yake na wale wenye ngozi nyeupe kama Wazungu, Waarabu na wahindi si watanzania. Inaonekana kwamba hawa "wana kwao" mara kadhaa inasemwa kwamba warudi kwao.

Kwa watu waliowahi kuishi maeneo ya mipakani mwa nchi yetu wanajua kwamba tunao "watanzania" ambao kiuhalisia si watanzania bali ni watu wanaotoka kwenye nchi jirani tulizopakana nazo. Lakini hao hawabaguliwi kama vile wanavyobaguliwa hawa wenye ngozi nyeupe.

Dhana ya kubagua ni hali inayotokana na watu dhaifu kwa kila kitu. Ni kweli kuna baadhi ambao ni wabaguzi toka kwa Wazungu, waarabu na wahindi lakini si halali kusema wote ni wabaguzi. Hata wasio wahindi wapo watu ambao tunawajua kwamba ni wabaguzi ama wa kidini au kikabila ama kikanda.

Kama tunao wamakonde toka Msumbiji na tunawaona ndugu zetu ni kwa nini watu ambao wapo hapa tangu miaka ya 1920 tunawaona si wenzetu? Kuna makabila hapa tanzania ni miaka ya hivi karibuni ndiyo walianza kuolewa na makabila mengine na bado tunawaona ni watanzania wenzetu, tatizo nini kwa hawa wengine?
Umenikumbusha tukio nililohadithia linalohusiana ukoo wa Abdulrasul [kwa watu wa tanga watauelewa] ambapo atuhumiwa kuwa yeye siyo mtanzania. Aliweza kuthibitisha kuwa siyo kwamba yeye ni mtanzania lakini hata baba wa babu yake ambaye alizaliwa tanga[wajerumani walikuwa wanaweka kumbukumbu za vizazi na vifo hasa mijini] na siyo hivyo tu maisha yao yalianzia bagamoyo ambapo babu ya babu yake alijenga msikiti ambao hadi kipindi hicho mabaki ya msikiti yalikuwepo na jina la aliyejenga lilikuwepo.
Ninasema hivi nikimaanisha kama watu kama hao ambao wanaushahidi wa zaidi ya miaka 150 tunawaita wageni wakati wengine wetu hatuweza hata kuthibitisha miaka 100 ya koo zetu kuwepo nchini ati ni 'wazalendo'
 
Abunwasi watu wetu tunadhani sisi tunaunganishwa na rangi zetu kuliko uasili wetu. Kuna wahindi hapa ukiwaambia warudi "kwao" wataishia uwanja wa ndege huko India. Sasa kuna watu wametoka nchi za jirani hata miaka hamsini hawana wao ndiyo wanajiona watanzania haswaa!
 
Kuna dhana inazidi kujengwa na kubebewa bango kwamba watanzania ni wale tu wenye ngozi nyeusi peke yake na wale wenye ngozi nyeupe kama Wazungu, Waarabu na wahindi si watanzania. Inaonekana kwamba hawa "wana kwao" mara kadhaa inasemwa kwamba warudi kwao.

Kwa watu waliowahi kuishi maeneo ya mipakani mwa nchi yetu wanajua kwamba tunao "watanzania" ambao kiuhalisia si watanzania bali ni watu wanaotoka kwenye nchi jirani tulizopakana nazo. Lakini hao hawabaguliwi kama vile wanavyobaguliwa hawa wenye ngozi nyeupe.

Dhana ya kubagua ni hali inayotokana na watu dhaifu kwa kila kitu. Ni kweli kuna baadhi ambao ni wabaguzi toka kwa Wazungu, waarabu na wahindi lakini si halali kusema wote ni wabaguzi. Hata wasio wahindi wapo watu ambao tunawajua kwamba ni wabaguzi ama wa kidini au kikabila ama kikanda.

Kama tunao wamakonde toka Msumbiji na tunawaona ndugu zetu ni kwa nini watu ambao wapo hapa tangu miaka ya 1920 tunawaona si wenzetu? Kuna makabila hapa tanzania ni miaka ya hivi karibuni ndiyo walianza kuolewa na makabila mengine na bado tunawaona ni watanzania wenzetu, tatizo nini kwa hawa wengine?
What is your point
 
What is your point
Pointi yangu kuwa kuna wananchi wengine ambao wana asili ya nje ya tanzania ni watanzania zaidi ya wengi wetu ambao hatuwezi kuthibitisha ukaazi wetu wa nchi kwa kipindi cha miaka hata 80 na bado tunajiita wazalendo kwa kigezo cha uafrika
 
Wako watu ni weusi,lakini ni machotara,wamechanganya damu,na wako wengi katika nyadhifa mbalimbali,kuwafahamu ni mpaka umjuwe ukoo wake,na wengine wana majina ya kiasili ya makabila ya Tanzania. Na wengi wao ni wwnye asili ya kiarabu.
Wakati mwingine watoto wa baba mmoja,mama mmoja,wakawa na rangi tofauti,mmoja akafuata rangi ya baba,mwingine ya mama.
Kwa hiyo unaweza ukambaguwa huyu mweupe,kumbe ana kaka au dada ni mweusi.Nimewahi kuhudhuria msiba,wa bibiwa mtu fulani mwenye wadhifa,akiwa yeye ni mweusi sana na jina la kikabila la kitanzania, nikashangaa kukuta ndugu zake,ambao pia ndio bibi yao,wakiwa wengi wao ni weupe,waarabu na wengine weusi kama yeye.
 
Mkuu. Simfahamu hata Mtanzania mmoja aliokataa kuchukua uraia wa nje. Wazawa wote ninaowafahamu ndani na nje ya nchi wana uraia wa nchi nyingine. Hata viongozi wa juu na watoto wao wengi tu wana uraia mwingine. Watu wanaangalia maisha kujitoboa siyo mambo ya uzalendo. Huwezi kuwa mzalendo ukiwa na njaa nje. Hizo sheria hazisumbui zaidi ya kutozwa viza kuja nyumbani. Hata wakibadili, sioni mabadiliko katika uchumi unaoendeshwa na serikali ya kibabe isiyoheshimu sheria.
Mhh..Strong words, anyway acha tuone kama tutafika hii safari mpya..
 
Swali ulidhakutana na mwanajeshi,polis au mgambo chotara,
Alishawahi kuwepo mkuu wa polisi kikosi cha usalama wa barabarani alikuwa anaitwa divas alikuwa goa....pia mkumbuke yule mwanajeshi maarufu Kwa jina la black mamba pia,
Hata wakina hanspope walikuwa jeshini pia

Ova
 
Ndugu yangu unajua hata HARBINDER SINGH SETH wa IPTL ni MHEHE wa IRINGA na ana Documents zote za URAIA ila usishangae maisha yake na familia yake yako AFRIKA KUSINI. Pesa anazochuma HATUNZII hapa

- Akili kichwani, Tanzania Shamba La MAVUNO.
Kuna mwananchi wa Tanzania na Raia wa tanzania lazma uelewe hili sio kila Raia wa Tanzania ni mwananchi wa Tanzania but wananchi wa Tanzania wote ni Raia wa Tanzania....Kama hujaelewa sema nirudie.
 
Pona kuna yule alikuwa askari Polisi akiitwa David Divaz!
MIMI mwenywe usione najiita mrangi lkn kiukweli mm syo ukabila la mrangi ila ukiniona physical utashangaa ila ndy hvyo,baba wa mababa zetu inasemekana walitokeaga hko ugiriki walikujaga kwenye kilimo cha mkonge
Ila mm kama nlifatiliaa historia Ya wazee wangu na nakja ielewa vzuri mpaka leo hii

Ova
 
Mleta uzi ni moja ya zao la roho za ubaguzi ndio maana anataka kutufikirisha masuala ya kibaguzi.
Definition ya mtanzania inaeleweka kwa attributes zake. Mtanzania mwenye uraia wa Kuzaliwa au kuandikishwa. Wote ni watanzania. Sasa kama unakatiza hadi kwenye rangi zao, makabila yao na asili zao, huu ni udhaifu dhahiri wa kibaguzi.
Tuna waingereza weusi ambao wako katika majeshi ya uingereza, tuna wamarekani weusi na wengine tumesoma nao sasa wamebadili uraia na wako kwenye jeshi la marekani na wanatambulika kama wamerakani.
Ni ngumu kumkuta mhindi, mzungu na mwarabu jeshini au polisi si kwa sababu ya kubaguliwa lakini wenzetu wanaangalia zaidi maslahi ya kiuchumi/fedha. Ni kiasi gani atalipwa na kuweza kuendesha maisha yake?
Hivyo, ubaguzi ni roho. Roho hiyo inaonekana kwa watu wote kwa viwango tofauti. Haijalishi wewe ni Mtanzania, M-USA, Muingereza, Mchina, Mwarabu au Mhindi. Roho ni roho tu. Hazina dini wala kabila wala Taifa. USA wanalalamikia ubaguzi, Saudia wanalalamikia ubaguzi, China vivyo, hivyo.
Hivyo, unayoyaona TZ yapo mahali pengine kwa viwango tofauti tofauti.
Somalia je, hali ya ubaguzi ikoje?
 
Swali;

Ulishswahi kuona ndoa ya Mtanzania mhindi na Mtanzania mkwere? au ndoa baina ya Mtanzania mwarabu na Mtanzania mmatengo?
 
Back
Top Bottom