Kuna watu wananiandama; Je, ni kweli Benki wanahifadhi Nyaraka Muhimu kama, vyeti, mikataba, Hati n.k

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
750
3,140
Mada inajieleza, Nazungumzia nyaraka zenye kuonesha umiliki halali wa kitu, mali n.k.

Niliwahi sikia hii kitu lkn sababu muda huo sikua na uhitaji basi sikufuatilia kuhusu uhalisia wake,

Kwa sasa nina uhitaji sana wa kujua hili, maana kuna washenzi mijitu mizima baadala ya kupambana wapate vyao kihalali wananiandama sana.

Najua kuna njia ya kuhifadhi ndani mwenyewe lakini imefikia hatua ya kuvunjiwa nikiwa sipo.

Kubwa zaidi juzi wakati nipo safarini kumbe nilipanda na spy nashuka kwenda kula hotelini narudi mtu kapekua begi langu akapita na bahasha iliyokua ndani akidhani atapata anachotafuta akaambulia documents ambazo najua haziwezi hata kumsaidia.

Naomba mwenye kujua hili, je ni kweli hii huduma ipo bank? Km haipo je kuna sehemu nyingne salama?

Ningeweza kuhifadhi ndani kwangu ila mimi ni mtu wa mizunguko sana, kuzunguka navyo naona ni hatari zaidi.
 
Hapo kwenye kumvuruga kabla yake ndo kuna shida,labda toa somo jinsi ya kuwavuruga watesi wa mtu katika nyanja mbalimbali!
Mtu kabla hajakuvuruga mvuruge mara 2.....

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom