Kuna watu wanalia wengine kufurahi lakini ujue Mungu ndie mpangaji wa yote haya

Kashindwa kutetea hoja yake, kakazana ni mipango ya mungu, how? Jibu hana

Binafsi huwa najihoji kuwa na dini ila mambo mengi sana yanakosa majibu mubashara basi naamua kuacha.

Ukizingatia, haya majibuya huyu mleta Uzi ndiyo ayo hayo hutolewa humo kwenye dini zote yaani hayana uhalisia kabisa.
 
Na hizi dini ndo zinatupotosha. Mimi siamini kwenye dini ingawa huwa nashiriki mara chache kutokana na misukumo ya binadamu. Vitu vingi havina uhalisia
 
ume
Kila kitu huwa kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake :

Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa,
Wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna kilichopandwa,

Wakati wa kuua na wakati wa kuponya

Wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga

Wakati wa kulia na wakati wa kucheka

Wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza

Wakati wa kutupa mawe na wakati wa kuyakusanya

Wakati wa kukumbatia na wakati wa kuacha kukumbatia

Wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza

Wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa

Wakati wa kurarua na wakati wa kushona

Wakati wa kukaa kimya na wakati wa kuongea

Wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia

Wakati wa vita na wakati wa amani

Usije ukafikiri kinachokutokea ni kwa bahati mbaya iwe furaha iwe huzuni yote ni mipango ya Mungu

Furaha yako inaweza kugeuka kuwa huzuni na huzuni yako kuwa furaha

Yote ni Mungu anakupangia

Muhimu ni kuendelea kuomba kwa alie juu juu kabisa
nikumbuka maajabu ya suleimani kwenye muhubiri kitabu nakipenda sana kile
 
Na hizi dini ndo zinatupotosha. Mimi siamini kwenye dini ingawa huwa nashiriki mara chache kutokana na misukumo ya binadamu. Vitu vingi havina uhalisia

[HASHTAG]#Poise[/HASHTAG], naziona tu hata sielewi.
Maana naona zinaleta fujo tu hasa huko Africa.
 
Kama anapanga kila kitu kwa mwanadamu kwanini asitupangie mazuri kila mtu afurahi?
Unapangiwa mikosi kila siku, hata ujitahidi vipi hali ni ngumu tu. Huyu Mungu ana nia gani hasa? Kwanini anaangalia watu wakiteseka tena wengine ni innocest kabisa hajishughulishi kuweka mambo sawa?
utamlaumu bure huyo mungu wa kufikirika mkuu, mazuri na mabaya yote ni nature ya universe
kikubwa watu tutimize wajibu wetu na tupendane ili kuifanya dunia iwe sehemu salama kuishi, otherwise kila mtu apambane na hali yake!
 
Simlaumu. Namshangaa mtoa mada
 
utamlaumu bure huyo mungu wa kufikirika mkuu, mazuri na mabaya yote ni nature ya universe
kikubwa watu tutimize wajibu wetu na tupendane ili kuifanya dunia iwe sehemu salama kuishi, otherwise kila mtu apambane na hali yake!

Kweli, mkuu.
Nimewahi kwenda sehemu moja mtu akafika watu tumekaa akasalimu watu wa dini yake tu kwa kuwapa mkono kwa kuvuka wasio dini yake.
Yaani, Tanzania ii hii, siku hiyo nilitmani nimzabe vibao vya uso ila sheria ya nchi hairuhusu mtu kujichukulia sheria mikononi.

Ila dini na waumini wake, wanaudhi sana wakati mwingi ukiangalia vile wanatenda mambo ya kipuuzi.

Any way, ndiyo ujinga ambao wakoloni waliuleta ili tugawanyike na kuchukiana sisi kwa sisi.

Maana, kama Mimi [HASHTAG]#poise[/HASHTAG] sina dini sasa hapa nilipo wenye dini zote wananichukia.

Pia, wenye dini zao nao ila zimetofautiana majina nao wanachukiana kwa sababu ya majina ya hizo dini kutofautiana.

Mfano, waisalmu wanawachukia wakristo, sasa waislamu wasuni wanawachukia waislamu washia
Bado tena unakuta na kwa wakristo wale wa Roman Catholic wanachukiana na KKKT, Walokole. Yaani; dini ni uwanja wa fujo.

Yaani, dini ni ujinga juu ya upumbavu tuliolishwa.

Cc.[HASHTAG]#demi[/HASHTAG],
 
Kimoja tu jiulize we ulitokea wapi na nani alikuleta hapa duniani ukijua hilo vingine ni rahisi kuvielewa

Naona unaelekea kukataa haujui ulikotokea
Nimetoka tumboni kwa mwanamke ambae ni mama yangu.
 
Tunaomba utueleweshe Mimi [HASHTAG]#poise[/HASHTAG] na [HASHTAG]#demi[/HASHTAG] .
Sasa, Mungu alimletaje na kumuumba shetani ili atutese na Mungu huyo ana nguvu!?

Kwa nini tuwe na matatizo ambayo Mungu anaweza kuyasitisha tukaishi bila kuwa nayo!?
Huyu anayeitwa shetani alikuwa malaika wa cheo kikuu tu huko mbinguni

Tamaa ya kutaka na yeye afanane na alieumuumba ndio ilimponza kwa kuwa alitaka na ye aabudiwe ilitokea vita kuu huko aliko Mungu kati yake na malaika mwingine aitwae Mikaeli na huyu Mikaeli alishinda vita hiyo so ndio chanzo cha huyu lusifer na wenzake kutupwa duniani na kabla ya kuifikia dunia alipita sayari mbalimbali na huko alipingwa vibaya kiufupi walimkataa
Lakini sisi wa duniani tukaukubali uongo wake na hapo ndipo tulipojiletea matatizo wenyewe ufunuo12/7-9

So sio kweli eti Mungu alituletea matatizo bali matatizo haya tumeyakaribisha wenyewe
 
Kama Mungu, ana nguvu ni kwa nini basi asimzuilie au amfunge watu wasipate mateso !?

Kwa hiyo Mungu, anafurahia watu kuteseka!?

Je, kwa nini maombi na sala za watu zisiwe na nguvu ya kumuondoa shetani kabisa asije tena katika maisha ya wanadamu.

Any way , Mungu na shetani wote ni Sawa tu kwa sababu , kama watu wanateswa na shetani na Mungu anaangalia tu sasa hapo unawatofautishaje hao wawili kama wote mambo yao yote siyo Sawa!

Kwa nini , Mungu asiondoe tamaa ya dhambi kwa wanadamu ili wasimfuate au wasishawishiwe na shetani!?

Kama Mungu, anamzidi shetani kwa nini hadi wafuasi wa huyo Mungu wanapatwa na majanga ambayo wewe unasema yanaletwa na shetani , kwa nini Mungu asiwateteee!?

Naomba usome vizuri hayo maswali yangu na unijibu nielewe labda naweza nikajiunga na dini ila ukishindwa ndiyo basi tena.

Cc.[HASHTAG]#demi[/HASHTAG].
 
Kashindwa kutetea hoja yake, kakazana ni mipango ya mungu, how? Jibu hana
Hoja yangu iko wazi mbona
Kuwa na huzuni, furaha,maombolezo na kadhalika yote ni mpango wa Mungu
Sababu kuna siku Mungu ataiangamiza dunia kwa sababu ya ujuaji wetu sisi binadamu
Tumempa shetani madaraka makubwa na Mungu alieumba kila kitu tumemshusha

Sema yeye ni Mungu wa subira ukitaka kubadilika badilika kweli sio maigizo
 
Binafsi huwa najihoji kuwa na dini ila mambo mengi sana yanakosa majibu mubashara basi naamua kuacha.

Ukizingatia, haya majibuya huyu mleta Uzi ndiyo ayo hayo hutolewa humo kwenye dini zote yaani hayana uhalisia kabisa.
Kwa hiyo we huamini Mungu amekuumba
 
Na hizi dini ndo zinatupotosha. Mimi siamini kwenye dini ingawa huwa nashiriki mara chache kutokana na misukumo ya binadamu. Vitu vingi havina uhalisia
Sijaleta mada ya dini hapa nazungumzia Mungu alieumba mbingu na dunia wakati huo hata dini hazikuepo

Kama humuamini Mungu atakulazimisha umuamini
Huamini yupo atakuonyesha kwamba yupo
Maana hivi sasa binadamu tunajiamulia tu amri za Mungu hatuzifuati kabisa

Hatumwabudu Mungu bali tunamwabudu shetani kinyume kabisa na Mungu muumbaji

Tusizini tunazini

Ili mradi tu tuko sambamba na shetani
 
Kwa hiyo we huamini Mungu amekuumba

Mmmmmh. Kwanza , simjui sasa naanzaje kuamini hivyo kuwa kaniumba!?

Pia, najua uumbaji ni Baba na Mama ndiyo waumbaji.

Mfano, kwa nini baadhi ya watu wakose uzazi kama Mungu anaumba!?
 
Kweli, mkuu.
Nimewahi kwenda sehemu moja mtu akafika watu tumekaa akasalimu watu wa dini yake tu kwa kuwapa mkono kwa kuvuka wasio dini yake.
Yaani, Tanzania ii hii, siku hiyo nilitmani nimzabe vibao vya uso ila sheria ya nchi hairuhusu mtu kujichukulia sheria mikononi.

Ila dini na waumini wake, wanaudhi sana wakati mwingi ukiangalia vile wanatenda mambo ya kipuuzi.

Any way, ndiyo ujinga ambao wakoloni waliuleta ili tugawanyike na kuchukiana sisi kwa sisi.

Maana, kama Mimi [HASHTAG]#poise[/HASHTAG] sina dini sasa hapa nilipo wenye dini zote wananichukia.

Pia, wenye dini zao nao ila zimetofautiana majina nao wanachukiana kwa sababu ya majina ya hizo dini kutofautiana.

Mfano, waisalmu wanawachukia wakristo, sasa waislamu wasuni wanawachukia waislamu washia
Bado tena unakuta na kwa wakristo wale wa Roman Catholic wanachukiana na KKKT, Walokole. Yaani; dini ni uwanja wa fujo.

Yaani, dini ni ujinga juu ya upumbavu tuliolishwa.

Cc.[HASHTAG]#demi[/HASHTAG],
Popote uonapo fujo ni kazi ya shetani kwa sababu shetani alishaapa watu hawatamfuata Mungu muumbaji
 
Sijaleta mada ya dini hapa nazungumzia Mungu alieumba mbingu na dunia wakati huo hata dini hazikuepo

Kama humuamini Mungu atakulazimisha umuamini
Huamini yupo atakuonyesha kwamba yupo
Maana hivi sasa binadamu tunajiamulia tu amri za Mungu hatuzifuati kabisa

Hatumwabudu Mungu bali tunamwabudu shetani kinyume kabisa na Mungu muumbaji

Tusizini tunazini

Ili mradi tu tuko sambamba na shetani
Bila dini hizo sheria za Mungu ungezipata wapi? Mungu unayemjua wewe ndo huyo uliyefundishwa kanisani.
Mtoa mada unajichanganya, hueleweki hata chembe.
 
Kama Mungu, ana nguvu ni kwa nini basi asimzuilie au amfunge watu wasipate mateso !?

Kwa hiyo Mungu, anafurahia watu kuteseka!?

Je, kwa nini maombi na sala za watu zisiwe na nguvu ya kumuondoa shetani kabisa asije tena katika maisha ya wanadamu.

Any way , Mungu na shetani wote ni Sawa tu kwa sababu , kama watu wanateswa na shetani na Mungu anaangalia tu sasa hapo unawatofautishaje hao wawili kama wote mambo yao yote siyo Sawa!

Kwa nini , Mungu asiondoe tamaa ya dhambi kwa wanadamu ili wasimfuate au wasishawishiwe na shetani!?

Kama Mungu, anamzidi shetani kwa nini hadi wafuasi wa huyo Mungu wanapatwa na majanga ambayo wewe unasema yanaletwa na shetani , kwa nini Mungu asiwateteee!?

Naomba usome vizuri hayo maswali yangu na unijibu nielewe labda naweza nikajiunga na dini ila ukishindwa ndiyo basi tena.

Cc.[HASHTAG]#demi[/HASHTAG].
Amzuie wakati alipokuja tulimkubali wenyewe
Kwanza hatuonyeshi jitihada za kumkataa na wale wanaozionyesha shetani hawasogelei so onyesha kwanza kumkataa then Mungu atakusaidia kupambana naye vizuri maana ni kiumbe kisicho na nguvu mbele za Mungu

Mungu hawezi kumuondoa tu wakati asilimia 90 ya watu duniani wako na shetani na wanamwabudu iwe ni kwa kujua au kutokujua
 
Back
Top Bottom