Kuna watu wanalia wengine kufurahi lakini ujue Mungu ndie mpangaji wa yote haya

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Kila kitu huwa kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake :

Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa,
Wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna kilichopandwa,

Wakati wa kuua na wakati wa kuponya

Wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga

Wakati wa kulia na wakati wa kucheka

Wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza

Wakati wa kutupa mawe na wakati wa kuyakusanya

Wakati wa kukumbatia na wakati wa kuacha kukumbatia

Wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza

Wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa

Wakati wa kurarua na wakati wa kushona

Wakati wa kukaa kimya na wakati wa kuongea

Wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia

Wakati wa vita na wakati wa amani

Usije ukafikiri kinachokutokea ni kwa bahati mbaya iwe furaha iwe huzuni yote ni mipango ya Mungu

Furaha yako inaweza kugeuka kuwa huzuni na huzuni yako kuwa furaha

Yote ni Mungu anakupangia

Muhimu ni kuendelea kuomba kwa alie juu juu kabisa
 
Ndio ni mpango wa mungu
Sio yote mungu ukupangia bali yeye mjuaji na mweza wa yote uamuzi mzina ni wewe kuamua mambo mengi mfano kuendlea kuteseka na magojwa na nguvu za giza hama kuliitia jina lake, wakati mwine Mungu hukuacha ulie tu au uteswe na wachawi kwani haujataka kumwita hama kufuata njia zake Mungu hakuumuumbia shida hizi mwanadan bali ni mpango w mwanadamu mwenyewe
 
Sasa uwe unabisha kwa hoja
Binadamu hana uwezo wa kujiamulia na hapa ndipo Mungu anapotuletea magonjwa huzuni na kadhalika
 
Ni ukweli kabisa
ahaaa! sasa kama amekupangia basi ni moja kati ya mungu ambae hawatendei haki watu wake! inamaana kuna watu amewapangia kwenda motoni na wengine peponi maana si unaishi kwa kupangiwa na yeye.. sasa kama anawapangia kwanini mnamghasighasi shetani wkt mungu wenu ndo amewapangia toka mwanzo wako mpk mwisho wako..?
 
Sasa uwe unabisha kwa hoja
Binadamu hana uwezo wa kujiamulia na hapa ndipo Mungu anapotuletea magonjwa huzuni na kadhalika
Hata kusema binadamu hana uwezo wa kujiamlia unajipinga mwenyewe kwani umejiamlia tu kusema binadam hana huwezo wa kujiamlia na wakati leo watu wanajimlia tu kujibagua wenyewe mfano mzuri ni yule anaeona rangi nyeusi ni udhaifu amekosewa kuumbwa hivyo yeye si lolote na ajichumbue tu na mikorogo hapa kajiamlia, watu hawajimrii kulewa, kuroga kumtegemeza mganga unataka yesu awalinde wakati wamejimlia njia zao wenyewe kwa upendo wa Mungu huwaacha na maamuzi yao na njia zao kwani wameamua kumfuata baba wa uwongo
 
ahaaa! sasa kama amekupangia basi ni moja kati ya mungu ambae hawatendei haki watu wake! inamaana kuna watu amewapangia kwenda motoni na wengine peponi maana si unaishi kwa kupangiwa na yeye.. sasa kama anawapangia kwanini mnamghasighasi shetani wkt mungu wenu ndo amewapangia toka mwanzo wako mpk mwisho wako..?
Ili swali lako linamdai vyeti ,,, halelujah!!!
 
ahaaa! sasa kama amekupangia basi ni moja kati ya mungu ambae hawatendei haki watu wake! inamaana kuna watu amewapangia kwenda motoni na wengine peponi maana si unaishi kwa kupangiwa na yeye.. sasa kama anawapangia kwanini mnamghasighasi shetani wkt mungu wenu ndo amewapangia toka mwanzo wako mpk mwisho wako..?
Shetani huyo huyo ametoka kwa Mungu so ni mpango wa Mungu pia
 
Hata kusema binadamu hana uwezo wa kujiamlia unajipinga mwenyewe kwani umejiamlia tu kusema binadam hana huwezo wa kujiamlia na wakati leo watu wanajimlia tu kujibagua wenyewe mfano mzuri ni yule anaeona rangi nyeusi ni udhaifu amekosewa kuumbwa hivyo yeye si lolote na ajichumbue tu na mikorogo hapa kajiamlia, watu hawajimrii kulewa, kuroga kumtegemeza mganga unataka yesu awalinde wakati wamejimlia njia zao wenyewe kwa upendo wa Mungu huwaacha na maamuzi yao na njia zao kwani wameamua kumfuata baba wa uwongo
Ndio maana kuna adhabu Mungu ameziweka huko ni kumkufuru mungu
 
there is natural power that oparete within an individual and free will that make decision
 
Kama Mungu ameumba kila kitu kilichopo kinachoonekana na kisichoonekana unawezaje kusema Mungu Hapangi lolote kwa binadamu
 
Back
Top Bottom