Kuna watu wanaishi vizuri sana, tembea uone

Kuwa na bafu ya milioni 50 au zaidi ujue net worth yako ni zaidi ya 1B, tatizo ukifika hizo level huwezi enjoy tena 75'' tv yenye 8K na juice ya tende, watakao enjoy ni ndugu na watoto.

Haya maisha huwa tunafikiri ukifika level fulani utapata furaha lakini si kweli, utafika hadi hatua ya kumiliki private jet, lakini utaona nikiwa raisi nitafurahi zaidi.
 
Pesa yangu ni ya halali Mkuu na pia nawafahamu wengi wenye pesa ambayo ni halali kupitia jasho lao na wanazo za kutosha tu kujirusha watakavyo.



Hakuna hela ya halali,magumashi lazima yawepo la sivyo utaishia kuwa lofa tu
 
Wenye pesa halali wapo. Kama hutaki kuamini hilo ni tatizo lako. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.

Mkuu utake usitake ya halali hapo labda ni %60, magumashi sio lazima ukabe au uibe,hata kwenye kukwepa kodi na mengineyo ni magumashi hayo,mwenye pesa za halali %100 hajazaliwa bado
 
Aisee....maana yangu anazuga tu hapa ila anaweza kuwa ana ghorofa.
Tunachangia kulingana na hoja na si kwa mawazo yetu, yeye amesema analala na kuku uvunguni, jamii forum mimi naijua sana tangu 2008 niko hapa japo nabadili badili ID.

Ndo maana mimi kwenye ule uzi wake nikamwambia kama kweli analala na kuku wakiwa uvunguni basi hapaswi hata kumiliki smart phone. Angechagua moja kufunga kuku wakiwa nje ya nyumba kwa kutoa elfu 50 na kununua mabati chakavu akajenga banda la kuku
 
Mwenyezi Mungu awaongozee kama maisha yao mazuri ni ya halali. Hawajamuibia mtu, kumpora au kumdhulumu yoyote yule bali ni jasho lao halali ndio limewawezesha waishi maisha hayo...
Dalili za mtu mwoga. Tafuta hela achana na habari unazowaza.
 
Back
Top Bottom