Kuna watu wanafikiri upinzani ndiyo kwisha habari yake wanasahau kufa ni sehemu ya kuanza upya.

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,541
3,449
Ili mbegu iote sharti ioze kwanza na kuharibika ili uhai uchipuke upya,ni jambo la ajabu sana hili kutafakari kwa kina.
Kwa wakulima hawawezi kustaajabu sana kwa sababu ya uzoefu wa jambo hilo ila kuna haja ya kujifikirisha zaidi juu ya mchakato unaofanyika.
Ukihusisha kuoza kwa mbegu na kuota kwenye maisha yetu ya kila siku unawez a ukauona uhusiano huo ukiwa dhahiri katika mambo mengi sana.
Kuna watu wana mtazamo kuwa upinzani Nchini unaelekea kufa kabisa lakini ninachokiona Mimi ni kuimarika zaidi kwa upinzani kuliko miaka mingi iliyopita.
Nina uhakika upinzani utakaozaliwa katika zama hizi utakuwa upinzani halisi uliotokana na misingi ya ndani kuliko ule wa 1995.
Hakuna namna yoyote ya kuzuia uoto wa asili porini,sharti uoto uote tu hata kama kutakuwa na ukame kiasi gani,mvua ikinyesha kila aina ya uoto itachipua.
Mbegu inayooza ili kuota haizailiwi peke yake ila huzaa matunda mengi na mbegu nyingine za aina yake nyingi mno kuliko yenyewe.
Hakuna Kanuni ya kutungwa na binadamu inayoweza kupingana na Kanuni za asili zinazoruhusu masuala kuendelea.
Upinzani haukuanzishwa na binadamu kwa faida yake ila upinzani ni mwigo wa binadamu kwenye mazingira yake.
Hata mawazo tu katika akili ya binadamu huwa na upinzani rejejea nadharia za Hobes,Hegel na Karl Marx unaweza ukaona nilichokiona.
Fuatilia nadharia ya Thesis-inavyozaa Antithesis-na hatimaye Synthesis unaweza ukahisi nimewaza nini hadi kuandika andiko hili.
 
Bwana Yesu alipingwa, Mtume Mohamed (swt) alipingwa,Budha alipingwa, Bahaullah alipingwa, Mizra Gullam alipingwa, Zorostrer alipingwa....wapinga Mungu wapo....Magufuli ni nani asipingwe atapingwa sana. Asipopingwa akiwa hai hata akiwa ametangulia mbele za haki atapingwa....Hata hitler ingawa amekufa lakini bado anapingwa
 
Back
Top Bottom