Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Watu hawana dogo!
Jana THRDC wametoa tuzo kutambua mchango wa wanaharakati wanaotetea haki za binadamu kupitia platforms mbalimbali.
Miongoni mwa waliopokea tuzo hiyo ni Mwanaharakati Maria Sarungi ambaye alitambuliwa kwa kupaza sauti kupitia mtandao wa Twitter.
Tuzo haina shida. Wapo walioona nembo ya tuzo ambayo ni Mkuki na Ngao haikupendeza kwa mwanamke hasa kwa kuzingatia mila na desturi za kiafrika.
"Hii tuzo iliyotolewa kwa akina Maria ni ya ajabu! Mtu kupewa Mkuki na Ngao ni ishara ya mwanaume wa kiafrica anayeenda vitani. Kwa asili yetu, mwanamke wa kiafrica hapewi mkuki na ngao" ameandika mdau mmoja kwenye mitandao ya kijamii akiambatanisha na picha ya Maria akiwa amesimama na tuzo hiyo kama inavyoonekana kwenye Uzi huu.
Mwingine akaongeza;
"Waandaaji wanatoa tuzo bila kuzingatia Maadili ya Kitanzania. Tafsiri ya Mkuki/Ngao/Panga/Upinde inakinzana na fikra za tuzo kwa mwanamke. Ni bora wangempa hiyo tuzo bila kukabidhiwa Mkuki au Ngao!"
Aidha, yupo aliyehoji kama ikitokea mwanaume kupewa tuzo ya chungu, mwiko na ufagio, itakuwa ni sahihi kupokea?
My take: Naona inafikirisha kweli. Je, kuna haja ya waandaaji wa tuzo kama hizi kuzingatia aina ya nembo kulingana na jinsia, tamaduni, mila na desturi?