Kuna watu wamefungwa na familia zao wasioe ama kuolewa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Hili jambo ni mpaka likukute ndiyo utaona madhila yake, la sivyo utaona ni story tu.

Kuna baadhi ya familia hutokea mtoto mmoja akainuliwa kuliko wengine, na yeye kwa kupenda ama kinyume chake, asifanye juhudi zozote kuwainua nduguze.

Huyu mzazi humuona kama ndio mkombozi na kichumio cha familia.

Wote tunatambua dhima, hamu na furaha ya kuwasaidia ndugu na wazazi mara upatapo kazi, biashara kustawi n.k na ukiwa bado single. Wengi huwaza nyumbani kwanza, wazazi na ndugu.
Hapa ni kwa vile bado huna kwako rasmi.

Wazazi wengi hulitambua hili na wachache hupenda kudiriki kusema: "Akipata kwake huyo hatatujali tena kama zamani", ama watasema "ameshapata kwake huyo huduma zimepungua na hatujali tena" Hii hofu wanayo wazazi wengi.

Ni ukweli usiopingika na jambo lisilozuilika tena unapompata wako wa kujenga kwenu nyie wawili sasa. Mambo hubadilika kwa kasi sana. Ukiamka badala ya kuwaza wazazi sasa, ama ndugu zako, cha kwanza utamuwaza mwandani wako. Ni wachache mno mno huweza kubalance hili.

Taratibu ukaribu huanza kupungua kati yako na familia yako ya wazazi na ndugu na ombwe kuanza kuonekana. Na kama ni familia iliyobweteka na haijitumi halafu wewe ndiyo kila kitu kwao, tatizo huwa kubwa maradufu.

Sasa basi baadhi ya wazazi, sometimes kwa msaada wa ndugu kwa kuogopa kukosa ukaribu walio uzoea, huamua kutumia nguvu za giza kukufunga ili usiweze kuoa wala kuolewa. Sana sana utaishia tu ku-date na watu kwa muda mfupi na mwishowe mahusiano kufa bila sababu zozote za msingi.

Unaweza kujikuta kabisa unatamani kuwa na familia yako baada ya kumpata mtu sahihi lakini the moment unawashirikisha wazazi na ndugu zako, matatizo huanzia hapo. Mwishowe wanaku-counsel kuwa huyo siyo mtu sahihi kwako nk nk. Unajikuta unampiga chini na mambo yako yanarudi kwenye mstari. Hapo lazima uwaamini ndugu zako.

Mzazi ni Mungu wako wa pili, usipomsikiliza yeye au akikunenea mabaya unaweza usifanikiwe maisha yako yote! Lakini je kama ukigundua ni kimeo? Je, utafanyaje ukigundua kuwa mzazi hataki uwe na mahusiano rasmi?

Ndiyo maana kuna baadhi huamua kwenda mbali na nyumbani na kufanya baadhi ya vitu kimyakimya bila kuwashirikisha wazazi na ndugu. Akishajiweka vizuri kabisa ndio hurejea akiwa tayari na kwake kulikosimama!!

Jr
 
Bado kazini, unarogwa usionekane, wife anakuroga usipate mchepuko, mchepuko unakuroga usione mwingine umsahau mkeo.

That's why life span yetu inadondoka kama nazi mnazini
Wazazi wa binti wanaloga uoe bint yao maisha yasonge. Wazazi wako wanakuloga usioe ila wazidi kufaidi maisha yako.

Kitaa unalogwa kisa umefanikiwa sana!¡/kwa hili lazima udate

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado kazini, unarogwa usionekane, wife anakuroga usipate mchepuko, mchepuko unakuroga usione mwingine umsahau mkeo.

That's why life span yetu inadondoka kama nazi mnazini

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazazi wa binti wanaloga uoe binti yao maisha yasonge. Wazazi wako wanakuloga usioe ila wazidi kufaidi maisha yako.

Kitaa unalogwa kisa umefanikiwa sana! Kwa hili lazima udate.
Kwa staili hii kwanini tusife mapema?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazazi wa binti wanaloga uoe binti yao maisha yasonge. Wazazi wako wanakuloga usioe ila wazidi kufaidi maisha yako.

Kitaa unalogwa kisa umefanikiwa sana! Kwa hili lazima udate.
Hii kali aisee 😂😂
 
Kuna bwana mmoja yupo vizuri kiuchumi ila tatizo hana mtoto, na ana mke inasemekana hayo ndo masharti...Kuna siku nimewahi kulala moja ya guest house yake anayomiliki niliota mindoto ya ajabu ajabu mara sijui kisima kinatoa moto..Haruhusu mwanaume na mwanamke kuingia mule pasipokuwa na cheti cha ndoa. (Nipo nje mada ila nipo kwenye right track...Mule mule ulozini).
 
Ukitaka kushangaa Ya MUSA sasa nipale ambapo

Familia hiyo hiyo -- ukute ina watoto wakike wakubwa ambao kutwa kucha wana waroga waume zao ili wapate chance ya kuwa miliki

Ila inapotokea Kaka yao akapata Mke/Mwanamke halafu huyo Mwanamke nayeye akamroga kaka yao ili ammiliki --- Basi hao ma-dada (ma Wifi ) na Mama mkwe huwa wana kuwa wakali dhidi ya Huyo mwanamke Kama vile Wao ni pili pili kichaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom