Kuna watu waliwekeza sana kwenye malumbano ya CCM na CHADEMA ili kujinufasha

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
6,000
4,586
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kama kuna uwezekano wa CCM kukaa meza moja na CDM kutafuta usuluhishi, kwanza lazima utambuwe kosa liko wapi ndio upange nini kinachotakiwa kujadiliwa.

Tukirudi kwenye kichwa cha habari, chembe chembe zilizojionyesha jana za kupeaa mikono kati ya viongozi wa CDM na Rais Magufuli, zimeleta hamasa kwa upande mmoja na huzunu kwa kwa upande mwingine. Na ni dalili tosha kwamba mahafahali wawili wakigombana, kuna watu wengine wanatumia huo mwanaya kujengea himaya yao. Uwezekano wa kuharibika yale yote walio jipangia na kutararia ni mkubwa sana na watatumia kila mbunu kukwita wewe mjinga na hujuwi unalolifanya. Mwl. Nyerere alituhasa, kadri tunavyojitahidi kwenda mbele tutasikia kelele nyingi sana zikituzomea ...wajinga hao…..

Chadema ilipofikia sasa, haina uwezo wa kukimbizana na Magufuli na kufanikiwa kumpita. Ajenda nyingi walizokuwa wanazipigania na ambazo ndio ilikuwa misingi yao ya kutaka kuingia madarakani, Rais Magufuli amezibeba zote. Chadema walitaka mabadiliko ya sera (policy change) ili kumlinda na kumjengea mazingira mazuri mfanyabiashara mkubwa na mdogo. Yote hayo Rais magufuili anayapitia kwa kasi ya ajabu. Leo hii unweza kufunguwa biashara au kujenga kiwanda bila bugudha ya rushwa au usumbufu wa kuchelewesha vibali.

Nchi zinazofuata mfumo wa vyama vingi na wana demokrasia iliyokomaa, vyama vinashirikiana kwa karibu sana hasa kwenye mambo ya kitaifa. Kwa lugha ya kiingereza wanasema Cross-Party Agreement au Cross Party politics. Huwezi kujiita wewe ni mwanademokrasia kama unashindwa hata kukaa meza moja na mwanasiasa mwenzako kuamua jambo linalohusu nchi.

Sitaki kufukuwa makaburi na kuangalia nini kilitokea katika kipindi cha miaka minne iliyopita, lakini nikiagalia wale wote waliokuwa wanafoka na kutoa maneno ya matusi na kumkejeli Rais Magufuli mpaka wemgine wanaenda nje ya nchi na kutoa taarifa za uwongo, picha ya jana Mwanza itakuwa imewaumuza sana, tena kupita kiasi.
 
Tumwache Magufuli atumikie Watanzania

Tuwaache Wapinzani wapige kelele watachoka tu
Ili mradi Rais anatekeleza kila ilani ya chama cha siasa
Huko kwenye kazi JPM hana mpizani, tatizo kuna watu wanaona treni inayoyoma wanakimbila kudandia na wengine wanawatukana wenzao wadadiaji, kama picha la kihindi.
 
Magufuli hakuombwa apatane na vyama vya upinzani, tumechoka na upotoshaji wenu.

Jee hapo kamuomba au kamkumbusha wajibu wake kikatiba?
Ameliweka jambo hilo kwa sababu maridhiano ya kitaifa na hayo wala hayahitaji kukaa vikao bali ni serikali kutoingilia Uhuru wa vyama kufanya siasa, kutobambikia watu kesi kwa sababu sio wanaccm na kiujumla kuheshimu sheria na katiba tuu.
Sasa nani anasema wanahitaji kukaa meza moja? Ameambiwa mbele ya mashahidi wa ndani nà nje, asipokubaliana kikiwaka anabeba lawama zote personally
 
Neno Maridhiano linatofauti kubwa na neno Taratibu au Kanuni, unachosema wewe ni kufuata kanuni lakini maridhano lazima pande mbili zonano pingana kukaa chini na kukubaliana taratibu ambazo zinawapendea wote.
 
..kuna watu pia waliwekeza ktk UKATILI na DHULUMA dhidi ya viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.

..kwa maoni yangu hao wamepigwa na taharuki hawajui nini kitatokea baada ya kauli za Mzee Mbowe na Prof.Lipumba.
Na hao pia wamo, wadau wote walio furahia na kuchochea malumbano ya kisiasa wanateseka huko waliko.
 
Na hao pia wamo, wadau wote walio furahia na kuchochea malimbano ya kisiasa wanateseka huko waliko.

..kuna watu wameua, wameteka, wametesa, wametia vilema, wamedhulumu, viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani.

..kwa maoni yangu hao ndiyo wanaweza kuwa KIKWAZO kwa hicho kinachoitwa " maridhiano. "

..na mwanasiasa au kiongozi akionja siasa za kikatili kama hizi za kwetu Tz anakuwa mateka ni vigumu kuachana nazo.
 
Ni jambo njema kukaa meza moja na kuongea ili kumpunguzia Magufuli haya makelele anayopigiwa kila siku, yanamfanya asikwende kwa kasi aliyodhamiria.
Mzee wa watu anafanya makubwa, nchi inakwenda kwa kasi, aachiwe atimize na kulivusha taifa.
 
Magufuli mwenyewe hajiamini na kazi zake,ndio maana anaogopa uchaguzi uhuru,na ameminya demokrasia kwa vyama vya upinzani,demokrasia ambayo ingemfanya ajitathimini kiutendaji,ila wenye akili wameamua kutafuta malidhiano naye,pamoja na kwamba wao ndio wanaoumizwa na utawala wa Magufuli,kwa kuwa malidhiano yalishawahi kuleta amani kuliko ubabe na utendaji wa mtu.

Mfano ni Kenya ambako walioibiwa ushindi ndio waliotafuta amani kwa kukaa meza moja na wezi,na sasa nchi ya Kenya ni shwari,wala huwezi ukasikia polisi na wananchi wakikimbizani mitaani, huku wezi na walioibiwa ushindi wakiendelea kunywa juisi pamoja.
 
Tukundane, Hapa umeongea kisiasa zaidi kuliko kiuhalisia. Hakuna mwanasiasa anyeogopa uchaguzi kama ajenda za kushindana zipo. Na kwahivi sasa sioni mpinzani akija anajenda yoyote itakayoshidwa kijibiwa na CCM au Magufuli mwenye.
 
Mleta uzi kuna ukweli hasa kwa hao waliotegemea CDM kufa. Lakini uko upande mmoja zaidi kana kwamba hauoni kwamba kuna ukiukwaji wa haki hasa katika muundo anaoufurahia wa kuondoa haki ya kuchagua na kuchaguliwa na pia hajaombwa amekumbushwa.

CCM mnajiona mko sawa sana, haya madaraja ya mikopo ambayo hailipiki hayata wasaidia kitu ktk kuinua uchumi na pia pakiharibika hapa. Kama una akili timamu Mbowe alimkumbusha Mheshimiwa jambo la muhimu mno.
Kumuua mtu ati alikukosoa na ukajipa uharali wa kitendo cha kuua nakunyanyasa hauwezi kuwa na uwezo wa kuwanyanysa milele.

Uchumi mnazani una boreka amani mnazani inaboreka kwa sababu baba zenu wanayo nafasi ya kuonea watu kwa sasa. Kwa sababu baba zenu wanao uwezo wa kupata kwa upendeleo kila jambo lina wakati.

Kujenga daraja la mkopo ubungo haliwezi kunisaidia mimi niliyeko Tunduru. Kugawagawa vipesa haviwezi kusaidia.
Kutenda haki ndiyo njia pekee inayoweza kusaidia kila jamii na kuleta utengamano. Ndege zenu hazisaidii kukua kwa uchumi bali miundo mbinu ya kuwasaidia wakulima waweze kuvuna. Njia ya muongo ni fupi unakopa unasema hukopi tusubiri
 
Tukundane, Hapa umeongea kisiasa zaidi kuliko kiuhakisia. Hakuna mwanasiasa anyeogopa uchaguzi kama ajenda za kushindana zipo. Na kwahivi sasa sioni mpinzani akija anajenda yoyote itakayoshidwa kijibiwa na CCM au Magufuli mwenye.

Mkuu ndio ninasikia kwako, kwenye nchi masikini ajenda kwa wananchi zinakosekana? Ajenda zipo nyingi sana ni suala la kuweka mtu sahihi kunadi ajenda hizo.
 
..kuna watu pia waliwekeza ktk UKATILI na DHULUMA dhidi ya viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.

..kwa maoni yangu hao wamepigwa na taharuki hawajui nini kitatokea baada ya kauli za Mzee Mbowe na Prof.Lipumba.
Polisi, tiss,mahakama NEC na bunge, baada ya hotuba ya jemadari mbowe ambayo raisi ameikuikubali, itabidi wasubiri maelekezo mapya ya utendaji wao,
 
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kama kuna uwezekano wa CCM kukaa meza moja na CDM kutafuta usuluhishi, kwanza lazima utambuwe kosa liko wapi ndio upange nini kunachotakiwa kujadiliwa.

Tukirudi kwenye kichwa cha habari, chembe chembe zilizojionyesha jana za kupeaa mikono kati ya viongozi wa CDM na Rais Magufuli, zimeleta hamasa kwa upande mmoja na huzunu kwa kwa upande mwingine. Na ni dalili tosha kwamba mahafahali wawili wakigombana, kuna watu wengine wanatumia huo mwanaya kujengea himaya yao. Uwezekano wa kuharibika yale yote walio jipangia na kutararia ni mkubwa sana na watatumia kila mbunu kukwita wewe mjinga na hujuwi unalolifanya. Mwl. Nyerere alituhasa, kadri tunavyojitahidi kwenda mbele tutasikia kelele nyingi sana zikituzomea ...wajinga hao…..

Chadema ilipofikia sasa, haina uwezo wa kukimbizana na Magufuli na kufanikiwa kumpita. Ajenda nyingi walizokuwa wanazipigania na ambazo ndio ilikuwa misingi yao ya kutaka kuingia madarakani, Rais Magufuli amezibeba zote. Chadema walitaka mabadiliko ya sera (policy change) ili kumlinda na kumjengea mazingira mazuri mfanyabiashara mkubwa na mdogo. Yote hayo Rais magufuili anayapitia kwa kasi ya ajabu. Leo hii unweza kufunguwa biashara au kujenga kiwanda bila bugudha ya rushwa au usumbufu wa kuchelewesha vibali.

Nchi zinazofuata mfumo wa vyama vingi na wana demokrasia iliyokomaa, vyama vinashirikiana kwa karibu sana hasa kwenye mambo ya kitaifa. Kwa lugha ya kiingereza wanasema Cross-Party Agreement au Cross Party politics. Huwezi kujiita wewe ni mwanademokrasia kama unashindwa hata kukaa meza moja na mwanasiasa mwenzako kuamua jambo linalohusu nchi.

Sitaki kufukuwa makaburi na kuangalia nini kilitokea katika kipindi cha miaka minne iliyopita, lakini nikiagalia wale wote waliokuwa wanafoka na kutoa maneno ya matusi na kumkejeli Rais Magufuli mpaka wemgine wanaenda nje ya nchi na kutoa taarifa za uwongo, picha ya jana Mwanza itakuwa imewaumuza sana, tena kupita kiasi.
Pia Magufuli akiachana na siasa za ukandamizaji akakubali maridhiano,kuna wanafiki wengi wanaomzunguka watakosa kazi, huenda hata wewe ukafa njaa
 
Wanaopinga kauli thabiti ya maridbiano aliyoitoa mbowe wanahofu ya kupoteza kazi na ulaji,
kitengo kinachotumiwa kuteka, kutesa, kuua kutishia wafanyabiashara, kuzuia wapinzani wasifanye siasa kinapewa fungu kubwa,

hivyo basi magufuli kukubali maridbiano kuna watu watapoteza uhalali waa uwepo wao kwenye payroll
 
Back
Top Bottom