Kuna watu waliowahi kukataa uteuzi wa Rais?

Marehemu Jaji Mkude alikataa uteuzi wa kuwa Jaji wa mahakama kuu zaidi ya mara mbili, na sababu kuu ilikuwa afya ya wazazi wake ilihitaji uangalizi wake wa karibu sana, asingeweza kutimiza majukumu makubwa ya nafasi ya ujaji katika hali ile.
Duh, kwa hiyo huyu Jaji Mkude baadaye alikubali uteuzi! Je wakati anakataa ujaji alikuwa na shughuli gani?
 
Kabla ya uteuzi haujatangazwa, muhusika anapewa taarifa kwanza kukubali au akatae.
Kwa muktadha huu, lazima wengi watakuwa wamechomoa uteuzi kimyakimya.
 
Kabla ya uteuzi haujatangazwa, muhusika anapewa taarifa kwanza kukubali au akatae.
Kwa muktadha huu, lazima wengi watakuwa wamechomoa uteuzi kimyakimya.
Sio mara zote mteule anapewa taarifa, kuna teuzi nyingi tu ambazo mteule anasikia jina lake kwenye redio au televisheni.
 
Aiseee kwani teuzi hizi huwa nilazima?

Sio lazima lakini unamfikirisha sana kiongozi na kupoteza muda kuandaa then unakataa basi kataa kistarabu omba hata ushauri wa daktari usikatae tu, ukikataa tu na ikajulikana hivyo sio vizuri unaweka GAP
 
m
Salaam Wakubwa,

Kama tunavyosikia teuzi mbalimbali wakiwepo Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu wakuu,Wakuu wa mikoa na viongozi wengine wakiteuliwa na kushika nadhifa mbalimbli katika uongozi katika nchi yetu.

Naomba kuuliza,je kuna watu ambao katika awamu yoyote katika nchi yetu aliteuliwa na Rais kushika wadhifa Fulani katika nchi yetu lakini kwa sababu zake mwenyewe akaona siyo vema na kutokubali uteuzi huo?

Nawasilisha.

Mkuu umeadimika kama chozi la njiwa
 
Mwingine ni Tuntemeke Sanga yeye alikataa kuwa Waziri kwasababu aliona sio saizi yake, aliutaka Urais wa Nyerere!!
Ni kweli mkuu nae huyu kilichompata ni adhabu ya kutotoka wilaya kwake kwa miaka kadhaa.
 
Salaam Wakubwa,

Kama tunavyosikia teuzi mbalimbali wakiwepo Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu wakuu,Wakuu wa mikoa na viongozi wengine wakiteuliwa na kushika nadhifa mbalimbli katika uongozi katika nchi yetu.

Naomba kuuliza,je kuna watu ambao katika awamu yoyote katika nchi yetu aliteuliwa na Rais kushika wadhifa Fulani katika nchi yetu lakini kwa sababu zake mwenyewe akaona siyo vema na kutokubali uteuzi huo?

Nawasilisha.
Yupo mama Mwatawala aliyekua mhadhiri chuo kikuu Mzumbe alikataa uteuzi wa kua mjumbe wa human right commission of Tanzania alipoteuliwa na Mkapa
 
Mbatia pamoja a kuiponda serikali ya ccm chini ya jk, alikubali kuwa mbunge wa viti maalumu. Usicheze na nafasi za kiteuliwa 1/100 ndio wanakataa.
Mbatia hakuwa mbunge wa viti maalum mkuu bali mbunge wa kuteuliwa na Rais, ipo tofauti kati ya Wabunge hawa wawili.
 
Mbatia hakuwa mbunge wa viti maalum mkuu bali mbunge wa kuteuliwa na Rais, ipo tofauti kati ya Wabunge hawa wawili.
Wabunge wanaoteuliwa na raisi huwa na kazi maalumu (wanakuwa mawaziri most of the time), hawateuliwi tu bila sababu. Mbatia hakuwa na sababu maalumu kuteuliwa kuwa mbunge, hivyo hana tofauti na wale wa viti maalumu..teh!!
 
Back
Top Bottom