Kuna watu soon watajutia nafasi adimu walizorubuniwa na kupoteza

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Kipenga Cha uchaguzi kitakapoanza na kuhitimishwa Kuna baadhi ya watu watajutia nafasi zao walizorubuniwa na kupoteza. Tukumbuke wanasiasa wengi hususan toka chama kikuu Cha upinzani Chadema walijiengua na kujiunga CCM wakidai kuunga juhudi. Jambo Hili lilitafasiriwa kuwa Ni rushwa kwa maana wapo walioamini wamenunuliwa.

Kwa Nini nasema watajutia, Hawa watu wakipita katika mazingira magumu mno ambapo baadhi ya mashabiki wao walikumbana na masahibu mbalimbali zikiwemo kuwekwa ndani, kuumizwa kwa kutiwa vilema hata baadhi kupotezewa jamaa zao. Hapa nakuambia iko kisasi kwa sababu tumekupigania dhidi ya tuliyeamini Ni adui yetu halafu wewe unatugeuka na kuanza kutunanga kisa umepata. Wakati wa kuunga juhudi hawakujali kufanya mikutano na sisi Bali walichojali ni kutinga PC na adui zetu na kutupa majezi yetu Kisha kuporomosha matusi dhidi yetu.

Mbaya kuliko Hawa magwiji walirudishwa kwa mlango wa hila kuwatumia wakurugenzi ambao wslihskikisha hawapati wapinzani na hata huko chamani kule wslikotoka michskato ya kuwatafuta wagombea haukufanywa. Hizi zote zitatia chuki dhidi yao hivyo wajiandae kisaikolojia kuwa hawana Chao kupitia kura ya wananchi. Wameendelea chuki dhidi ya vyao vyao kule walikotoka hata kusahau uwakilishi wao na kujikita kuchamba upinzani bila kujenga hoja kwenye mijadala ya kitaifa. Mara utawasikia rais ameletwa na mungu kana kwamba wananchi hawajui andiko kuwa kiongozi anatokana na Mungu.

Narudia Tena Hawa watu watapata shida kujinadi kwa wananchi. Wanajua Ni jinsi gani jeshi la polisi na wakurugenzi wslivyowasaidia kurudi bungeni na dhahiri wanaelewa credibility yao kisiasa ilivyopungua. Mikutano yao majimboni hawafanyi Tena Bali wao Ni PC
 
Wamepeleka kijiko puani badala ya mdomoni tutasikia chafya zao nchi nzima.
 
Back
Top Bottom