Kuna watu makatili kweli kweli, achoma paka moto akiwa hai

Niligombana na baba yangu alitaka kuwa mbwa wetu kisa wanakula mayai kwanini iwe hivyo mnyama hajawahi kuwa na rasilimali yoyote,wao wanaishi kwa kututegemea sisi na hii ni kwa sababu tuliwakalibisha nyumbani
 
Tatizo wengi mnaangalia mlipoangukia na siyo mlipojikwaa. Hawa paka wengi wameamua kuishi maisha ya wizi kwa sababu wametelekezwa. Mtu anafuga paka, anaacha wanazaana hovyo hawapi huduma,halafu anategemea watakula nini? Asilimia kubwa ya paka wezi chanzo ni binadamu.

paka ni kama kuku wa mayai,yaani kadri mazingira yalivyo bora anazidi kuzaa.
 
Unaongea hayajakukuta. Fikiria na hali ngumu hii umekopa hela sehemu ukaamua kiingiza vifaranga vyako vya kuku wa broila ili baada ya mwezi wakupe faida na upunguze deni na ukizingatia bei ya vifaranga iko juu halafu unatoka zako mizunguko unakuta paka kama huyo kala vifaranga wako.

Usilaumu tu kwa kila unachoona vaa uhusika wa huyo mchaga. Haya Mapaka yasiofungwa yanasumbua sana.

Kwamm niliyewahi kupatwa na usumbufu wa Mapaka haya nampongeza jamaa alichokifanya
Wewe na paka akili zenu zinafanana.

Kama huwezi kuelewa kwamba paka hana utashi, basi kwa hakika wewe na yeye tofauti yenu ni kiwiliwili tu.
 
We jamaa bwana huruma yako haina logic

Kwani unapowafuga hao kuku wanakua kama sehemu ya familia au ni kwa ajili ya biashara.

Mbona ukiwauza na kupata pesa husikitiki.

Usitupige kamba mkuu.
 
Huyu taahira ni wa kupiga shaba kabisa, unatesaje kiasi hicho kiumbe kisicho na utashi wa kujua chochote zaidi ya inner instincts zinazomwambia njaa inauma, kula hicho, huyo mnyama haelewi chochote. Hii roho ilianza kwa wale mbwa waliochoma vifaranga Arusha, tabiaia kama za majibwa yani. Namlaani huyu mchagga kwa kitendo alichokifanya kwa nguvu zangu zote, mshxenzi mkubwa huyo, apigwe shaba kabisa
Hujawahi kupata hasara wewe
 
paka ni kati ya wanyama jeuri sana asee.. anaweza akafanya kitu, anajua kabisa sio sahihi kukifanya, huku anakuangalia usoni kama kusema: "yeah, nasukuma glasi ianguke ivunjike na huna la kunifanya." mbwa ndo kidogo unaweza kum-train akaeleweka, ila paka! hapana.
Yule alifanya makusudi ka fungua friji kaangusha sufuria zima mchuzi wote na samaki kibao chini katafuna,mi narudi na njaa zangu kwanza kachafua jiko msosi kamaliza dah nilikasirika haswa.
 
Ni njaa tu mkuu,miaka fulani nikiwa kijana nilifuga paka.
Akawa mkubwa haswa na kanenepa sana kwa ajili ya lishe.
Yule paka aligeuka sana badae ikawa kero.
Kwanza hakai ndani, ye ni kupigwa miti tu nje huko.
Ikawa kero.
Siku kafungua friji kala samaki woote.
(Sijui alihonga)
Hapo sina plan ingine ya msosi.
E bana siku hiyo nikapanga mauaji.
Karudi jioni hivi zile hasira nimemkuta jikoni nikafunga mlango nikarudi na gongo.
Kama la kuchezea golf
Hiyo mechi humo ndani
Ilikua balaa.
Nilimkosakosa na ye alinikosa kunitoboa macho mpaka nikafungua mlango mwenyewe akakimbia kutoka hakurudi tena.
Sijawahi kupenda paka tena
Napenda wanyama ila paka aisee sipendi. Mbwa hata umpige vipi, hawezi kukugeuka zaidi ya kukimbia ili hasira ipungue. Ila paka anakugeuka kabisa ili mpambane.
 
Paka ni km binadamu mkuu wana roho ngumu sana na kila kitu wanajua.
X wangu alikua na paka wawili mama na mwanae wa kiume.
Ajabu nikiwepo pale mama yuko benet mda wote ataniganda hana vurugu.
Huyu mtoto sasa na lilikua limevimba kweli paka paka haswa.
Naingia nikale mbususu litafungua mlango linajilaza katikati.
Kumtoa hapo mtakesha.
Nikana isiwe tabu nikajikata.
 
hawa wadudu hamuwajui nyinyi,usione hawaishi na msela ukadhani ni bahati mbaya.wanajua.

enzi hizo niko kijijini huko,imechinjwa kuku ikaungwa rost imeliwa robo mchana,inatakiwa iliwe na usiku na kesho yake maana tulibaki watoto 3 tu,wazazi waliondoka mchana huo kwenda seminar mjini.

huwa kuna meza kubwa sana iko nyuma ya nyumba,hiyo tunaweka vyombo na vifaa vingine vya chakula na hata mboga sometime,siku hiyo kwa kuogopa paka hatukuweka sehemu nyingine yoyote isipokuwa sufuria husika iliwekwa juu ya hiyo meza,kisha ikafunikiwa ndoo kubwa juu ya ndoo ikawekwa tofali ya block.

tukaenda kisimani kuchota maji.
wakati tunarudi tunashangaa kwa mbaaali kuna kama kuku wanakimbizana kunyang'anyana vitu,kumbe wamegawana nyama ya kuku aliyechinjwa,kuku nao tulikuwa nao kama 130 hivi wa kienyeji,kucheki ndoo juu ya meza iko chini,tukajua hapa tayari tumeshapigwa.

kufika pale paka tuliyekuwa tunamfuga,analamba mchuzi chini na wanaye kujipongeza kwa kazi aliyoifanya huku matumbo yanakaribia kugusa chini,kwa hasira nilipiga mmoja shuti hakuinuka na roho zake 7.
wengine walitawanyika mbiooo.
Ahaaaa mbavu zangu
 
Nimefuga kuku sana wa kienyeji mbegu za hapa hapa nchini, mbegu ya malawi (wale weusi tiiii) na mbegu ya Kuroiler. Kwa kweli inauma sana pale kuku anapokufa mda mwingine unakosa hadi raha. Kuna kuku kishingo kila nikiingia kwenye malazi ya kuku huwa alikuwa ananifata nyuma nyuma nikstokea kumpenda sana yule kuku. Siku mojan nimedamka mapema kwenda kulisha kuku nikakuta kuku wangu kishingo kadanja nilikosa raha siku nzima. Baba yangu mdogo mfugaji nae alikuja nisabahi home ile kunikuta na simanzi akanitusi acha ufala wewe akisema “mimi nafuga ngombe na mbuzi na wanakufa, wewe kafa kuku unatia huruma, angekufa ngombe wa million 3 si ungekufa??” hahah

Nimeandika haya nikimfikiria huyu mchaga ana roho ya namna gani kuchoma paka moto. Mie kama kuna paka anakula mifugo ningemuwekea sumu kwenye samaki. Lakini huyu jamaa ana roho ya namna gani. Mimi ni mchaga wa mkuu Rombo lakini aisee kuna wachaga wana roho ngumu sana. Nawataadharisha wale wenye wenza wa kichaga chungeni sana kuweni makini mnooo...

View attachment 2004793
OhOhOh; mkuu, paka ni wa kwake au ni paka wa jirani au mwenye paka huyo hafahamiki au ni paka shume/wa porini?
Aisee Mangi; Kama ni paka wa kwako au jirani hujatenda vema. Je, umewakinga kuku wako kwa uzio/wavu ili paka, kicheche, Kenge , nyoka wasiweze kuingia? Maskini paka alikuwa hajui kwamba alikuwa anawinda na kula kisichoruhusiwa.
Kuna njia za kumfundisha paka au mbwa asiwinde au kula mifugo ya hapo nyumbani.Mara nyingi kutumia ile mitego ya chuma ya kubamiza (Maarufu kama mitego ya panya). Haitamwua lakini cha moto atakiona kwani atabamizwa pua au atanaswa mguu na hawezi kujitoa mwenyewe.
 
Nakumbuka kipindi nikiwa nmeua form4 nilianza ufugaji wa kanga(ndege) nikichukua mayai ya kanga natamishia kuku nilibahatika kupata vifaranga 54 ila bahati mbaya paka walifanya lile banda ndio shishi food namuunga mkono mdau alichofanya!
 
Nakumbuka kipindi nikiwa nmeua form4 nilianza ufugaji wa kanga(ndege) nikichukua mayai ya kanga natamishia kuku nilibahatika kupata vifaranga 54 ila bahati mbaya paka walifanya lile banda ndio shishi food namuunga mkono mdau alichofanya!
Kumbe mpo wengi wa aina hiyo aisee?! Mdau mmoja hapo juu aliuliza : Kwa kumwua huyo paka mla vifaranga kwa mateso makali vile, je, vifaranga au hasara imerudi? Hajapata jawabu. Nina hamu ya kumsikia Mangi amejibu vipi hilo swali. 🤣 🤣
 
Ukatili wake uko wapi hapo?


Nakumbuka miaka ile natoka shule saa 8, nakutana na paka anajifuta mashavu. Yan kala kipolo changu

Wanasema paka usimpige huku umefunga mlango.
Lakini mimi nilifunga mlango na madirisha. Ndani ya dakika 10 tulikaa meza ya maradhiano mwenyewe nilifungua mlango

Ila yule paka hakuwai kuonekana tena pale kijijini. Nilimpa heavy heavy kiasi cha kwamba akaanza kuwa chui
Nikaona tusifike huku sasa
Tangu siku hiyo mimi na paka hatupendani
 
OhOhOh; mkuu, paka ni wa kwake au ni paka wa jirani au mwenye paka huyo hafahamiki au ni paka shume/wa porini?
Aisee Mangi; Kama ni paka wa kwako au jirani hujatenda vema. Je, umewakinga kuku wako kwa uzio/wavu ili paka, kicheche, Kenge , nyoka wasiweze kuingia? Maskini paka alikuwa hajui kwamba alikuwa anawinda na kula kisichoruhusiwa.
Kuna njia za kumfundisha paka au mbwa asiwinde au kula mifugo ya hapo nyumbani.Mara nyingi kutumia ile mitego ya chuma ya kubamiza (Maarufu kama mitego ya panya). Haitamwua lakini cha moto atakiona kwani atabamizwa pua au atanaswa mguu na hawezi kujitoa mwenyewe.
Huyu niliipat tu whatsap sio paka wangu wala paka wa jirani. Huyu mangi kamuua paka vibaya sana angeweza hata kwenda kumbwaga mbali na anapoishi. Mie nafuga ila kwa sasa sina mifugo wengi niko Manzese sasa na nimejenga vyema kwa hiyo sina usumbufu wa wanyama hao uliowataja na naishi ndani ya fence inasaidia.

Hiyo mitego nilishawahi iona Rombo, aisee ule mtego ambao upo kama mkasi mbwa akiweka mguu mpaka unakatika. Hata ule mtego sio poa cha msingi watu wazingatie kuna baadhi ya dawa zinafukuza wanyama kwa kuwa wanyama wanakuwa hawapendi harufu yake. Hata baadhi ya miti inafukuza ukipanda kwako. Ndo maana wamasai hawapati kuliwa mifugo yao ovyo, wanyama hawasgei kabisa kwenye mifugo yao. .
 
Back
Top Bottom