Kuna watu makatili kweli kweli, achoma paka moto akiwa hai

Gily Gru

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
7,800
20,749
Nimefuga kuku sana wa kienyeji mbegu za hapa hapa nchini, mbegu ya malawi (wale weusi tiiii) na mbegu ya Kuroiler. Kwa kweli inauma sana pale kuku anapokufa mda mwingine unakosa hadi raha. Kuna kuku kishingo kila nikiingia kwenye malazi ya kuku huwa alikuwa ananifata nyuma nyuma nikstokea kumpenda sana yule kuku.

Siku mojan nimedamka mapema kwenda kulisha kuku nikakuta kuku wangu kishingo kadanja nilikosa raha siku nzima. Baba yangu mdogo mfugaji naye alikuja nisabahi home ile kunikuta na simanzi akanitusi acha ufala wewe akisema “mimi nafuga ngombe na mbuzi na wanakufa, wewe kafa kuku unatia huruma, angekufa ngombe wa million 3 si ungekufa?” Hahah!

Nimeandika haya nikimfikiria huyu mchaga ana roho ya namna gani kuchoma paka moto. Mie kama kuna paka anakula mifugo ningemuwekea sumu kwenye samaki. Lakini huyu jamaa ana roho ya namna gani. Mimi ni mchaga wa Mkuu Rombo lakini aisee kuna wachaga wana roho ngumu sana. Nawataadharisha wale wenye wenza wa kichaga chungeni sana kuweni makini mnooo.

Tahadhari, video ya kutisha.

Huyu taahira ni wa kupiga shaba kabisa, unatesaje kiasi hicho kiumbe kisicho na utashi wa kujua chochote zaidi ya inner instincts zinazomwambia njaa inauma, kula hicho, huyo mnyama haelewi chochote. Hii roho ilianza kwa wale mbwa waliochoma vifaranga Arusha, tabiaia kama za majibwa yani. Namlaani huyu mchagga kwa kitendo alichokifanya kwa nguvu zangu zote, mshxenzi mkubwa huyo, apigwe shaba kabisa
 
Huyu taahira ni wa kupiga shaba kabisa, unatesaje kiasi hicho kiumbe kisicho na utashi wa kujua chochote zaidi ya inner instincts zinazomwambia njaa inauma, kula hicho, huyo mnyama haelewi chochote. Hii roho ilianza kwa wale mbwa waliochoma vifaranga Arusha, tabiaia kama za majibwa yani. Namlaani huyu mchagga kwa kitendo alichokifanya kwa nguvu zangu zote, mshxenzi mkubwa huyo, apogwe shaba kabisa
Simtetei huyu mchaga kweli kafanya kitendo cha kikatili
Je wanao ua ng'ombe na mbuzi nao pia sio makatili?

Wale wanaokula nyama yetu pendwa ya kitimoto, wanamuua vibaya mno hakuna mnyama anauliwa mbaya kama kitimoto nao sio wakatili?

Tena hata wewe ushawahi ua mbu ambae haelewi chochote na anafata instincts zake

Kumpiga shaba hapo sishauri. Kwa wenzetu kuna haki za wanyama. Tanzania sijajua zimekaaje, ila tunatakiwa sana kuboresha haki za wanyama. Ukigonga mnyama wa mbugani unashtakiwa, ila matukio ya kikatili yanaendelea sana huku duniani. Ndo mana nashauri binadamu tuwe VEGANS, kama mimi naheshimu pia haki za wanyama...
 
Kuchoma moto?!!!! Hapana aiseee, hii haikubaliki, ningemjua huyo jamaa ningemwinda kama digidigi
 
Sasa unakuja utotoni mwako ulikua unaua ovyo mijusi. Unashika mjusi, unamkatakata nawembeeeee

Kwann usiwe na roho katili ukubwan?
Nilikuwa napenda kuwakata mijusi mkia nikiwa wadogo
Tulikuwa tunaaminishwa ukiwa unaua mijusi utakuja kutetemeka ukubwani

Ila roho hiyo mimi binafsi sina. Unaweza kukuta jamaa alilelewa na parokia
 
Kumbe paka hana roho 7😅😅
Ukimpa paka pilau akala ananyonyoka manyoa yote
Akiingia kwenye shimo anashindwa kutoka
Ila atakaa mpaka akonde na atatoka hata kama week mbili
Paka kweli ana roho ngumu, ila roho ya paka kuwa saba, sijui hilo
 
Ni njaa tu mkuu,miaka fulani nikiwa kijana nilifuga paka.
Akawa mkubwa haswa na kanenepa sana kwa ajili ya lishe.
Yule paka aligeuka sana badae ikawa kero.
Kwanza hakai ndani, ye ni kupigwa miti tu nje huko.
Ikawa kero.
Siku kafungua friji kala samaki woote.
(Sijui alihonga)
Hapo sina plan ingine ya msosi.
E bana siku hiyo nikapanga mauaji.
Karudi jioni hivi zile hasira nimemkuta jikoni nikafunga mlango nikarudi na gongo.
Kama la kuchezea golf
Hiyo mechi humo ndani
Ilikua balaa.
Nilimkosakosa na ye alinikosa kunitoboa macho mpaka nikafungua mlango mwenyewe akakimbia kutoka hakurudi tena.
Sijawahi kupenda paka tena
 
Nilivyosoma juu juu mwanzo nikajua ulimpa kipigo paka mpaka akafungua mlango
Kumbe wewe ndo ulifungua mlango
Inasadikika paka ndio mnyama msafi na mstaarabu sana. Ukimfuga na kumfundisha vyema anafugika kuliko wanyama wengine wote. Mwanyama huko nje wanakuwa trained. Hata ukitupa chakula chini haokoti, na wala hawanyi hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom