Kuna watu hufa mara mbili

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,782
Unaweza kudhani ni stori za kijiweni au kufikirika lakini haya mambo yapo na uzoefu wangu wa kuhudumia wafu ulinifanya nikutane naye.

Kuna watu hufa mara mbili na mara nyingi ikiwa ni usiku, wahudumu wa mochwari wanalifahamu hili vema! Unaletewa mwili uuhifadhi kwenye jokofu lakini kwa wakati huo majokofu aidha yamejaa au kuna miili mingi inahitaji kuipanga vema kabla hujaiload kwenye jokofu.

Miili yote inayoletwa mochwari imeshathibitishwa na daktari kwa maandishi kuwa huyu ni marehemu/maiti hana uhai tena hapumui na ni mzoga lakini ukiwa kwenye harakati za kupanga hizo maiti ghafla mojawapo ya maiti inasimama wima na kutaka kupiga hatua huku macho bila kupepesa yakiwa yamemtoka pima! !! Huna jinsi unaisindikiza na teke irudi ilipokuwa na baada ya hapo hainyanyuki tena.

Mochwari kuna mengi ya ajabu ya kutisha na kustaajabisha na wahudumu wa huko wanaona mengi! Lakini kitu kisicho na majibu ni kwamba kwanini kuna maiti hua zinafufuka na kufa tena?

Bado kuna mengi hatuyajui.
 
Sijui kwa nini mwanadam ana tofauti na viumbe wengine kama wananyama na ndege.
Labda huko kuamka kifo chake hakikutoka kwa Mungu sa wale walio sababisha wanakosea step pengine.tusaidie ndugu yangu we mwenye kujua nasi macho yanguke
 
Sijui kwa nini mwanadam ana tofauti na viumbe wengine kama wananyama na ndege.
Labda huko kuamka kifo chake hakikutoka kwa Mungu sa wale walio sababisha wanakosea step pengine.tusaidie ndugu yangu we mwenye kujua nasi macho yanguke

Kuna jamaa aliajiriwa huko kukamshinda akakimbia! wale wahudumu wanaenda kwa wangaga ili wasivione!

Kuna vifo sio kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuna watu hufa kwa vinyongo na visasi na wengine hufa ghafla huku wakiwa kwenye jambo moja muhimu sana! Hivyo hata baada ya roho kuachana na mwili bado ile conscious mind haitaki kukubali ile hali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom