Kuna watu hawazipendi kabisa dhana hizi "Demokrasia" na "Haki"

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Watu wasiopenda demokrasia na haki ,huwashabikia na kuwatukuza sana watu wanaokandamiza haki na demokrasia.

Kitu kimoja nataka kuwaambia watu wa aina hii ni kuwa; haki na demokrasia ndio ubinadamu wenyewe. Kwa asili binadamu aliubwa kama nafsi iliyo huru yenye utashi kamili. Ni nafsi inayojua mema na mabaya na hivi vyote vimeandikwa katika mioyo yao.

Kuna watu wanafikiri demokrasia ni dhana inayohusu mambo ya siasa pekee yake! Huku ni kupungukiwa maarifa, demokrasia unagusa nyanja zote za maisha, kama uchumi, utamaduni na maisha ya kila siku.

Kuikataa demokrasia ni kukataa ubinadamu. Haki ni kitu halisi, haki haipendi kupuuzwa, haki si tu kwamba ni takwa la kibinadamu, haki ni takwa la Mungu mwenyewe. Haki isipotetewa hujitetea yenyewe.
 
Back
Top Bottom