Kuna watetezi wa CCM lakini "Mafao ya viongozi wastaafu yashtua"! Tujaribu kwa upande mwingine! Sio dhambi

Uko na akili nyingi sana ndugu yangu. Eti mtu anamlingalisha Rais mstaafu na mwalimu au muuguzi ! Rais ni cheo cha juu kabisa katika nchi. Mimi naona hayo mafao hayatoshi kabisa.
Mbona mambo ya kawaida unataka rais akistaafu aishi kama RAIA wa kawaida

In reality mi naona rais astaafu anapumzika tu .

Hafu MTU kama rais usifananishe Na daktari sijui nurse au mwalimu yule ni kiongozi wa juu kabisa katika taifa kuwatunza top 3 wetu wakistaafu sio sababu ya umaskini wetu hizo ni argument za kitoto.

Lazima tuwatunze hawa watu wamebwba siri zote za nchi wanajua nchi nje ndani unataka wakaishi kiufukara baada ya kustaafu washawishike kufanya mambo ya ajabu.

Tena nadhani
Pia top wa majeshi nchini inabidi waweker pia kwenye hizi privileges incase nao hawana

Watu kama CDF, Na top team yake yote yani luteni general wake Na ma major heneral.

IGP, DG wa TISS
Pia mwanasheria mkuu Na jaji mkuu pamoja Na speakers wote.

They know too much lazima tuwacontrol baada ya kustaafu Na kuwatunza hadi wanapokufa ni jukumu LA taifa.
 
Sababu za kuing'oa CCM hazijatosha kabisa. Labda miaka 25 mbele
Ndio maana tuna kila sababu ya kuing'oa CCM ili tuufukie kabisa huu mfumo kandamizi hadi kwenye mafao! Lazima tubadili katiba kuuondoa huo mfumo wa kugawana rasilimali zetu watu wachache wakati hata wanapokuwa madarakani mishahara na malupulupu yao ni kufuru tupu! Wanajua kabisa kuwa wanawanyonya wengine lakini kwakuwa wamenogewa hawataki kubadilika! Dawa pekee kuking'oa hiki chama tupate mfumo mpya kabisa! Ni Nyerere tu ndio alistahili hayo mafao hawa wengine wote wamefanya hadi biashara wakiwa Ikulu!
 
Jana Pascal mayala alileta post ya kumwombea lisu uteuzi wa ubunge.hivi kwa akili ya kisomi isiyokuwa na msukumo wa kujipendekeza,mayalla anauwezo wa kujilinganisha na Lisu!.jamaa nilikuwa namheshimu sana lakini alipofikia inadhihirisha kazi anayoifanya haimlipi.

Ccm hakuna Uwezo wa kuisogeza tz mbele kimaendeleo,Bali kuisogeza mbele tz katika umaskini uliokithiri.
Hatuhitaji watawala,bali viongozi.

NEC,POLICE,MAHAKAMA wawe makini mwaka huu,maana wapo wachache kuliko wapiga kura.

Tanzania ni kubwa kuliko wao.tz haipiti ila wao watapita.
Mr amigo.
 
Mbona hueleweki, tuambie nia ya uzi wako ni nini ili tujue, vinginevyo tunaona kama unapiga kampeni uchwara ambayo ni kama kelele za mpangaji ambazo hazimnyimi usingizi mwenye nyumba
Jana Pascal mayala alileta post ya kumwombea lisu uteuzi wa ubunge.hivi kwa akili ya kisomi isiyokuwa na msukumo wa kujipendekeza,mayalla anauwezo wa kujilinganisha na Lisu!.jamaa nilikuwa namheshimu sana lakini alipofikia inadhihirisha kazi anayoifanya haimlipi.

Ccm hakuna Uwezo wa kuisogeza tz mbele kimaendeleo,Bali kuisogeza mbele tz katika umaskini uliokithiri.
Hatuhitaji watawala,bali viongozi.

NEC,POLICE,MAHAKAMA wawe makini mwaka huu,maana wapo wachache kuliko wapiga kura.

Tanzania ni kubwa kuliko wao.tz haipiti ila wao watapita.
Mr amigo.
 
Tena hayo mafao hayatoshi yanatakiwa yaboreshwe zaidi.
Ndiyo maana hata Yesu na mtume Mhamad walipingwa pamoja na mafundisho mazuri yote waliyotoa kwa wanadamu. Hata Mungu akija leo duniani kujidhihirisha mbele ya wanadamu, atapingwa tu. Utashangaa unayeweka comment kama hii, maisha yako ni ya kuungaunga tu lakini badala yake unasema "hayo mafao hayatoshi yanatakiwa yaboreshwe zaidi"

Uzuzu kama huu unafurahiwa sana na hao wanao kula asali na maziwa, wakiona wapiga kura wao wanayafurahia maisha yao ya mlo mmoja na kuwatakia wao wakubwa waboreshewe zaidi.
 
Hawa mahayawani tar 28 Lazima waondoke tunakoelekea watatutia Vidole matakoni.
 
Mbona hueleweki, tuambie nia ya uzi wako ni nini ili tujue, vinginevyo tunaona kama unapiga kampeni uchwara ambayo ni kama kelele za mpangaji ambazo hazimnyimi usingizi mwenye nyumba
Sipigi kampeni wala nini,ila nakataa uongo na unafiki.kwenye ukweli hawasemi.
Au kwa vile nimeitaja ccm!,kiufupi ndugu,ccm haiwezi kukwepa rawama kwa watanzania waliowengi kwa hatua hii.maana tangu Uhuru mpaka leo.watajipambanua VP!.
 
Nawaza
Vipi Mwalimu akistaafu
Vipi Daktari akistaafu
Vipi Nesi akistaafu
Vipi mfanya kazi yoyote wa uma akistaafu.

....je wao malipo yako saawa na hawa wakubwa?

Nasema hii sio serikali ya watu wa chini.

Nchi ya watumwa na watwana ila haisemwi wazi wazi
 
Ndiyo maana hata Yesu na mtume Mhamad walipingwa pamoja na mafundisho mazuri yote waliyotoa kwa wanadamu. Hata Mungu akija leo duniani kujidhihirisha mbele ya wanadamu, atapingwa tu. Utashangaa unayeweka comment kama hii, maisha yako ni ya kuungaunga tu lakini badala yake unasema "hayo mafao hayatoshi yanatakiwa yaboreshwe zaidi"

Uzuzu kama huu unafurahiwa sana na hao wanao kula asali na maziwa, wakiona wapiga kura wao wanayafurahia maisha yao ya mlo mmoja na kuwatakia wao wakubwa waboreshewe zaidi.
Mimi niliyekomenti nina akili timamu na elimu ya kutosha tu na maisha yangu siyo ya kuungaunga kama unavyojidanganya, nasema tena hayo mafao kwa viongozi wetu wastaafu bado ni madogo yaboreshwe tena. Huwezi kunipangia cha kuposti hapa wakati bando ni langu
 
Lawama kwa lipi kwa mfano hebu nisaidie ndugu yangu
Sipigi kampeni wala nini,ila nakataa uongo na unafiki.kwenye ukweli hawasemi.
Au kwa vile nimeitaja ccm!,kiufupi ndugu,ccm haiwezi kukwepa rawama kwa watanzania waliowengi kwa hatua hii.maana tangu Uhuru mpaka leo.watajipambanua VP!.
 
Lawama kwa lipi kwa mfano hebu nisaidie ndugu yangu
Kwanza siasa weka kando japo sina uhakika kama u mwanasiasa.

Demokrasia imeminywa sana,hakuna nchi iliyoweza kupata maendeleo pasipokuwa na demokrasia ndugu.sio kwamba raid hatumpendi ra hasha bali kuna mambo anafanya si kama taasisi bali MTU binafsi.sasa hiyo haina ustawi.kumbuka tz INA wakazi zaidi ya milioni 50.
So,kitendo kilichofanywa na katibu vs polepole hakuna afya kwa mstakabali wa demokrasia.
Vyombo vya habari havina sauti,nikweli au sio kweli ndugu.nieleze ukweli.siasa weka pembeni.
 
WAKATI Watanzania kwa mamilioni wakiendelea kukosa huduma mbalimbali muhimu ikiwamo afya na njaa kutawala katika maeneo mengi nchini, imebainika kuwa viongozi wastaafu wanarundikiwa mafao.

Ukubwa wa mafao hayo na posho kwa marais, makamu wa rais na mawaziri wakuu wastaafu unatajwa kuwa huenda ndiyo chanzo cha uongozi kupiganiwa kwa udi na uvumba na kwa gharama yoyote, kutokana na kuwa vyeo hivyo huwanufaisha katika maisha yao yote na baada ya wao kufariki wategemezi wao huendelea kunufaika.

Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1999, ambayo ilirekebishwa mwaka 2005, inaeleza kuwa Rais Mstaafu anapomaliza kipindi chake cha uongozi, hupata mafao ya mkupuo.

Ingawa kiwango cha mshahara wa Rais wa Tanzania ni siri, sheria hiyo inaeleza kuwa mafao yao hukokotolewa kwa kuzingatia mshahara wa juu aliowahi kupata miezi aliyofanya kazi.

Kiwango cha mafao hayo hukokotolewa kwa kutumia kanuni za kiwango cha asilimia itakayopangwa na mamlaka husika.

Mbali ya mafao yake ya kazi, Rais Mstaafu hulipwa posho ya kila mwezi kiasi cha asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani. Kiasi hicho ni sawa na Sh80 kwa kila Sh100 anayopata Rais aliye madarakani.

Licha ya posho hiyo, Rais hupewa ulinzi, msaidizi, katibu muhtasi, mhudumu wa ofisi, mpishi, dobi, mtumishi wa ndani, mtunza bustani, madereva wawili na gharama za mazishi atakapofariki.

Mafao mengine

Pamoja na malipo ya mkupuo anayopata Rais Mstaafu, pia anapewa pasi ya kusafiria ya hadhi ya kidiplomasia, yeye pamoja na mke au mume wake.

Rais pamoja na mke wake, pia hulipwa gharama za matibabu ndani au nje ya nchi.

Baada ya kustaafu rais pia hulipiwa matengenezo ya magari mawili yenye uzito usiopungua tani tatu, ambayo hutolewa na Serikali, ambayo pia hubadilishwa kila baada ya miaka mitano.

Kama hiyo haitoshi, Rais pia hujengewa nyumba mpya, ambayo ni lazima iwe na vyumba angalau vinne, viwili kati ya hivyo ni lazima viwe na huduma zote ndani (self-contained).

Aidha, nyumba hiyo ni lazima iwe na ofisi iliyokamilika na nyumba kwa ajili ya mfanyakazi wake.

Rais huyo mstaafu vilevile atagharimiwa gharama za mazishi pindi atakapofariki

Makamu wa rais na mawaziri

Mafao hayo ya viongozi wa umma yanampa nafasi Waziri Mkuu mstaafu na makamu wa rais fursa kama anazopata Rais, isipokuwa wao hawajengewi nyumba, pia wanapata gari moja tu.

Makamu wa rais na waziri mkuu wastaafu wanapewa fedha za kulipa mishahara ya watumishi, mpishi, dobi, mfanyakazi wa ndani, mtunza bustani na dereva.

Sheria hiyo inawakinga pia wategemezi wa viongozi wastaafu, hasa viongozi hao wanapofariki.

Kinga ya wategemezi wa viongozi hao iliundwa katika marekebisho ya Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Siasa ya Mwaka 1999, ambayo ilitiwa saini na Rais mstaafu Benjamin Mkapa Juni 2005. Marekebisho yaliyotiwa saini na Rais Mkapa ni pamoja na kuwalipa mafao wajane na wagane wa viongozi wa juu wa kitaifa akiwamo rais, makamu wa rais na waziri mkuu.

Rais mstaafu akifariki dunia, mke au mume wake hupewa nyumba, posho kiasi cha asilimia 40 ya mshahara wa rais aliye madarakani.

Aidha, mjane au mgane huyo hutengewa fedha za matibabu ndani ya nchi na matengenezo ya gari analopewa na Serikali.

Pia hulipiwa mshahara wa kima cha chini kwa dereva na mtumishi wa ndani pamoja na hupewa usafiri wa kwenda mahali atakapoishi maisha yake yaliyosalia.

Mabadiliko hayo yalilenga pia kuhakikisha kuwa iwapo kiongozi husika alikuwa analipwa pensheni kwa ajira ya awali, malipo yake yataendelea kutumiwa na mjane.

Aidha katika kikao cha Bunge la Bajeti mwaka uliopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kuwa Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya matibabu ya wastaafu wanaopaswa kutunzwa na Serikali.

Mawaziri wakuu waliostaafu na kunufaika na mafao hayo ni sita akiwamo, Joseph Warioba, Samuel Malecela, Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

Marais wastaafu, wanaonufaika na mafao hayo kwa sasa ni Benjamin Mkapa aliyeiongoza Tanzania kwa miaka kumi, kati ya mwaka 1995 na 2005 na Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza kati ya mwaka 1986 hadi 1995.

Akizungumzia unono wa mafao hayo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy alisema: “Huo ni mzigo, kwa Serikali” Alisema ni vyema kama hilo jambo likapelekwa bungeni ili lijadiliwe kwa kina.

Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Rose Kamili, alisema kuwa ni wakati wa wabunge kujenga hoja ili sheria hiyo ibadilishwe, kwani wapo wastaafu, ambao hawalipwi na wana madai ya muda mrefu.

“Mbona marais wakiwa madarakani tayari wanakuwa na fedha za kutosha, wanakuwa na mali na wameshawekeza kwa kiasi kikubwa, iweje wapate mafao makubwa kiasi hiki?” alisema akihoji.

Alisema kwamba mafao hayo pamoja na yale ya wanajeshi, Jaji Mkuu na IGP ni makubwa yakilinganishwa na uchumi wa taifa.

Source: Mwananchi.
Acha tu, inauma sana sana, na bado wanataka tujipange kwenye jua kali, mvua, vumbi na matope tuwashangilie wakiwa ndani ya ma-vx! Wakujilaumu ni sisi kwa kutokufanya lolote kwa kutumia kura zetu walahi, wajinga ni sisi na ni wapumbavu kabisa
...
 
Mimi niliyekomenti nina akili timamu na elimu ya kutosha tu na maisha yangu siyo ya kuungaunga kama unavyojidanganya, nasema tena hayo mafao kwa viongozi wetu wastaafu bado ni madogo yaboreshwe tena. Huwezi kunipangia cha kuposti hapa wakati bando ni langu
Hongera mkuu, uko sawa kabisa.
 
Tukiwachekea watatufanya wajinga hawa watu
Tukicheka na KIMA, tutavuna mabua. Bado hatujachelewa sana tangu 1961 mpaka sasa tumeshajua mbivu na mbichi. Mabadiliko aliyokuwa analilia JPM tumeyaona. Ilikuwa kuturudisha 1980, na kumbe ccm ni ileile, hakuna kipya.
 
Afu chakusikitisha zaidi unamkuta muhusika toka katika mahindi uliyotaja hapo juu te na akiwa kijijini amebandika mabango ya Ccm mpaka chooni kwake. Anakwambia yy ni Ccm kindakindaki. Ujinga mzigo
 
Back
Top Bottom