"Kuna Watanzania wanaopenda tufanikiwe, na kuna Watanzania wanaotaka tufeli"-How is this possible?

Roman Israel Esq

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
2,026
3,280
Yamindinda said:
Tatizo unafiki na uzadiki umetujaa watanzania kwenye hili Saga kuna watanzania wanaopenda tufanikiwe na kuna watanzania wanaotaka tufeli

Kuna kauli nyingi sana zenye kufanana na hii kutoka kwa member anayeitwa yamindinda! Ambaye alikuwa akifurahia kuwa kampuni ya Barrick inapata matatizo na kwahiyo ni furaha kwetu!Kwamba kuna watazania wenzetu wanaotaka tufanikiwe, na kuna wale wanaotaka tusifanikiwe!

Hili la kushangaza sana, how is this even possible? Au labda hatujui wala kufahamu maana halisi ya mafanikio? Au pengine labda hatujui ni hatua gani zinazoonyesha kuwa sasa tunaelekea kwenye mafanikio? Au ni kwasababu kuna ambao wanaamini tumeingia chaka na kuna wanaoamini tuko sawa yani kwenye light traki?How is this even possible? Au ni namna zetu za tofauti za kutizama mambo na kuya analyse?
 
Wenzetu walioendelea kisayansi,kielimu ,kisiasa,Kijamii,kiuchumi na kiteknolojia wana mipango iliyopangwa kwa karne nyingi sana.
Kila kitu wanachokifanya kilipangwa kwa miaka mingi iliyopita. Na Yeyote aliyetawala akavuruga mipango yao walimkataa kwa nguvu zote.

Sisi mpaka sasa hata sheria tulizoweka wenyewe za kulinda haki,utu,na Uhuru wa watu wetu wenyewe bado ni shida kuzifuata na kuzilinda. Watawala wanakiuka sheria kwa makusudi na kutoa matamko badala ya sheria.
Sasa mafanikio ya matamko Mara nyingi sio endelevu.
Mafanikio yanapaswa yawe ni mwendelezo wa mipango na malengo ya miaka mingi.

Watanzania wengi sana wanapenda mafanikio yao binafsi.
Ndio maana mtu akipata madaraka anageuka na kuacha Yale aloyokuwa akiyapigania na kuilosoa serikali kuwa inakosea.
Mtu Huyo huyo anakua tayari hata kuona wakosoaji wakioshia Gerezani.
Wengi wanataka maendeleo yao wenyewe sio ya watu wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenifumbua macho yangu kwa namna ya tofauti. Thread hii ilikuwa ni swali fikirishi sana. Nashukuru sana kwa kunielewa mkuu na kuweka pointi zako za ukweli kabisa. Umejibu kwa namna ambayo umeonyesha upeo mkubwa.

Kuna kitu nimejifunza kutoka kwenye bandiko lako. Kwasababu nimekuwa nikjiuliza sana hilo swali. Yani kuna ambao wanaona kabisa kuwa tunafanikiwa na kuna ambao wanaona kuwa tumepotea. Kumbe ubinafsi wetu sisi watanzania pia ni sababu mojawapo kubwa!
 
Back
Top Bottom