Kuna wasiasa wa aina nyingi Tanzania, ebu tutazame aina kuu tatu

nelly nashon

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
242
521
KUNA WANASIASA WA AINA NYINGI SANA TANZANIA, KWANGU MIMI NAONA AINA KUU TATU

1) Wanasiasa ambao kazi yao kuu ni kuitetea serikali, yaani kuwatetea watawala.
Wanasiasa wa aina hii wao kazi yao kuu ni kuirinda serikali kwa kujenga hoja kwa wananchi kuonesha kuwa serikali iko makini na hakuna udhaifu katika utendaji. Kundi hili la wanasiasa wao wako tayari kufanya lolote kutunza heshima ya watawala hata kama wataonesha wazi madhaifu yao.
Kundi hili ni kubwa na linapendwa sana na watawala, serikali.

2) Wanasiasa ambao kazi yao kuu ni kutetea wananchi, yaani kuwatetea wanyonge.
Kundi hili ni dogo lakini linaushawishi mkubwa, wapo karibu na wananchi, huikosoa serikali wazi wazi pale inapokosea, huwatetea wananchi wanyonge kwa kuikumbusha serikali kuwahudumia wananchi.
Hawa wako tayari kufungwa, kupigwa virungu, kutaifishwa mali zao, kubezwa lakini hawasiti kupaza sauti zao kwa kuonesha wazi shida za wananchi na kuitaka serikali kuzitatua.
Kundi hili halipendwi na watawala.

3) Wanasiasa uchwara, bendera fuata upepo!!
Hawa kimsingi huwa hawajui ni kipi wanacho kisimamia na kukipigania, wao wapo tu kusubiri matukio ili wapate cha kuzungumza, na maranyingi siasa zao hazina mizizi kwani ni za msimu tu.
Hawa serikali mara nyingi huwatumia kama vibaraka kwani hawana forums ( jukwaa),

Kama nilivyo tangulia kusema, kuna aina nyingi hizi ni tatu tu kati ya nyingi. Unaweza jitathimini ujue wewe ni mwanasiasa wa namna gani!!!
 
Back
Top Bottom