Kuna waraka wa serikali kuzuia kuajiri watanzania walioko nje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna waraka wa serikali kuzuia kuajiri watanzania walioko nje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Feb 10, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Nilijibu thread inayaotaka watanzania tulioko nje turudi nyumbani. Nikaeleza kwamba niliwahi kuelezwa kwamba wakati Mary Nagu akiwa Wizara ya Utimishi, alipitisha waraka ulioagiza taasisi na mashirika ya serikali kutoajiri watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi, sababu zikiwa kwamba kuwaajiri wao ni kuwakatisha tamaa watanzania "wazalendo" waliobaki nchini kusaidia kujenga nchi yao katika mazingira magumu. Dhana hapa ilikuwa kwamba hawa walioko nje "waliikimbia au kuisaliti nchi yao". Hii pia ilichangiwa na dhana kwamba watanzania wanaofanyia kazi nje wanaonekana kuwa na "international experience" ambayo inafanya mara nyingi wawazidi wale waliopo nchini.

  Naona hili ni jambo muhimu linalopaswa kujadiliwa. Ikiwa kuna mwenye kuweza kutupatia huo waraka itasaidia sana. Kama huo waraka upo basi pia utakana unafiki wa viongozi wanaotuomba turudi nyumbani kusaidia kuijenga nchi ikiwa huku wakijua kuna amri imetoka kwamba tusipewe kazi. Na pia ni vizuri kusikia maoni ya wengine kuhusu watanzania tulioko nje kushindania kazi na wale walioko nchini.

  China wao waliona umuhimu wa kuwatumia wafanyakazi walioko nje. Basi walikuwa wakiwafuata wataalamu wa kichina waliobobea na wanaofanyia kazi nje, na kuwaomba warudi nyumbani kwa mshahara ule ule au zaidi ya wanaopata katika ajira zao nje ya China. Hii strategy imefanikiwa sana kuchangia maendeleo ya China! (Angalia kwa mfano, mtaalamu mmoja wa juu wa technolojia ya tiba ya nano technology ni mama mmoja mtanzania anafanya kazi South Africa!)
   
Loading...