Kuna wanaume wanapitia 'mitihani' sana maishani. Ndo maana wanachelewa kuoa

Basi bwana,

Kuna friend of mine mmoja kanipa kisa chake nimeona Huruma sana.Ba Nikaona Si vibaya kushare nanyi ili kama bado kuna wanawake ama wasichana wa hivi waone Aibu kidogo.

Kuna kaka mmoja hapo zamani kidogo alipata mpenzi, akaamua kumuendeleza kimasomo ila hawakuwa wanaishi nyumba 1. Ni ile ya nenda rudi na kufanya usafi wa nyumba na kurudi. Msichana akamaliza shule na chuo.

Basi bwana, huku na huku jamaa huyu akaona si vibaya amvute nyumbani kwake rafiki wa kiume toka kijiji kimoja ili nae aje kutafuta ridhiki ukitegemea yeye alishavuka hatua moja na rafiki yake huyo hakuwa kwenye hali nzuri. Wakaanza kuishi wote, tukumbuke yule dada bado alikuwa anakuja na kurudi bado mipango ya kuishi pamoja haikuwa imekamilika.

Jamaa mwenye nyumba akapata safari ya kwenda India alipokaa kwa miezi 5. Huku nyuma mpenzi wake akawa anaendaa kufanya usafi kama kawaida. Wakaanza urafiki na shemeji mtu huku na huku wakapeana na mimba ndani ya nyumba ya jamaa.

Sasa jamaa aliporudi na baada ya wahusika kugundua what will come to happen in the near future, dada akaanza kupiga chenga, mara amesafiri mkoa Mara sijui yupo Tanga, Mbeya. Na huku akidai amepata mimba.

Bila kuelewa mchezo lakini akiwa na machale ya samaki aina ya kambale, akaamua kuwa mpole huku akipeleleza kwa makini. Na anaendelea kusema kuna kipindi kutokana na ubusy mchumba akiwa mkoa jamaa alikuwa anamwagiza jamaa atume pesa kwa njia ya Gari.

Wakati ule simu zipo ila bado huduma za pesa. Jamaa akawa anadai ni yeye anatuma. OK, siku zikaenda na miezi ikakatika watoto mapacha wakazaliwa. Huyu mchumba akawapa na majina ya wazazi wake yeye bila kujua sio damu yake. Lakini kuwa alikuwa hana uhakika na jambo alilokuwa anahisi akaamua kuwa mjinga na kuanza uchunguzi.

Basi, siku moja akaenda Voda akadai simu yake imeibiwa kwa maana ya kutaka kujua ukweli (simu aliyokuwa anatumia dada ilikuwa ya huyu mchumba na zamani simu zilikuwa hazisajiliwi)lengo la kwenda voda ni kuiblock line na kuifufua kwa no. Ile ile kwa maana kwamba simu zote sasa zitaanza kuingia kwake na kwa simu ya yule dada nikawa hakuna mawasiliano. Na ikumbukwe wakati huo dada alikuwa kwa wazazi kujitazamia uzazi.

Kama alivyokuwa anawaza au machale yalivyokuwa yanamcheza SMS zilianza kumiminika toka kwa rafiki ake akijua anawasiliana na 'mwizi mwenzake' akagundua kumbe hata majina aliyoenda kuwapa wale mapacha wa kike na wa kiume ya wazazi wake hawayatumii. Wamewaita wanayojua wao si ukweli wanaujua wao?

Baada ya kugundua ukweli miaka wa watu kwa hasira alienda kumchukua Baba mzazi wa dada na kumwambia twendeni nyumbani nikawaonyeshe mzazi halisi wa hawa mapacha na pia kuanzia leo 'sihusiki na matunzo yoyote' na kabla ya Hayo alishachukua na damu ya watoto kwa siri na kupima DNA na kweli damu haikuwa yake.

Kumbuka jamaa mwizi hakuwa amejua uchunguzi wa mhusika. Alijua bado siri yake ipo palepale na akiwa bado nyumba ya rafiki ake bado alishangaa ghafla baba wa binti na mchumba mtu wakiingia ndani na kukabidhiwa.

Cha kushangaza huyu kaka mwizi ndo aliyekuwa wa kwanza kuingia chumbani na kuchukua kisu na kumrushia mchumba. Lakini mwisho wa siku jamaa aliishia police kwa kutishia maisha.

Wadada jamani. Tukumbuke fadhira hata kwa siku moja. Ona mfano huo kaka wa watu mpaka leo hataki kuoa tena hasa akikumbuka.Utu ni muhimu.

Je kama ungekuwa ni wewe kaka umepatwa na kisa hicho ungefanyaje?

Sent from my Solar 5 using JamiiForums mobile app
Lazima utakuwa ni ww tu

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni story ya kutunga tu.mambo ya DNA tanzania yameanza kipindi hata mpesa ipo hewani!
Amini hivyo.Siwezi kukubishia Ni kawaida kuwa Na watu wabishi.Amini hivyo hivyo.Basi.

Sent from my Solar 5 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni story ya kutunga tu.mambo ya DNA tanzania yameanza kipindi hata mpesa ipo hewani!
Uliza kwanza.Kuna Mambo mengi yalikuwepo ila inactive. Mfano unaweza niambia dawa za Ukimwi za kuongeza uhai wa MTU kuishi zilianza lini TZ??zilikuwepo Muda ila kuanza rasmi kutumika mpaka Wewe kujua Ndo shida.Usibishe Kila kitu Ndugu Yangu.Angalia Mada unasema nini sio kutafuta tumakosa ambato Hata hatupo.But Ni kawaida penye watu wengi.

Sent from my Solar 5 using JamiiForums mobile app
 
Very sad, ila kwa upande wa kuchelewa kuoa nakuunga mkono. Ni kweli binadamu tuna mapito sana. Ila kwa wanaume mapito yetu ni mengi. Tuchelewe tu.
 
Very sad, ila kwa upande wa kuchelewa kuoa nakuunga mkono. Ni kweli binadamu tuna mapito sana. Ila kwa wanaume mapito yetu ni mengi. Tuchelewe tu.
Haaaa haaa Je wewe una experience? Umeongea kiudhuni sana

Post sent using JamiiForums mobile app
 
mbona mnamlaumu uyo dada tu uyo kaka nae alishindwaje kumueshimu aliyemtoa kijijini c angetumia hata condom
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom