Kuna wanaopanga maandamano ya nchi nzima kushinikiza kusiwe na uchaguzi 2020 na Magufuli aendelee kuwa Rais

kajima

JF-Expert Member
Dec 5, 2009
1,263
1,500

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
1,938
2,000
Kwanza nakushukuru kwa kuniheshimu kutumia verified name. Licha ya kutumia verified name pia mimi ni mwana habari, jukumu kuu la waandishi wa habari ni tell nothing but the truth. Hivyo mimi ni mkweli daima na yote niandikayo humu ni kweli tupu.

Kuamini ni jambo moja na kuwa na hakika ni jambo jingine. Nakuomba mambo ya imani, tuyaache kwenye dini, hapa tuzungumzie vitu vyenye uhakika na sio masuala ya imani.
  1. Ina maana hujui nani kaamuru kuawa Ben Saanane?. Kwanza sina uhakika kama Ben Saanane ameuwawa, wewe ndio unanieleza sasa. Nijuavyo mimi ni Ben Saanane ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, mpaka sasa hakuna ajuaye kilichomkuta. Kumbe mwenzetu unajua kuwa kauwawa na una mjua hadi aliyeamuru Ben Saanane kuuwawa!. Una uhakika wa hili?.
  2. Hujui nani kaamuru Tundu Lissu ashambuliwe?. Pia simjui aliyeamuru Tundu Lissu ashambuliwe, kwenye hili la Tundu Lissu, mimi naungana na mamlaka rasmi kuwa Tundu Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, na nimeisha andika mabandiko mengi kuhusu shambulio la Tundu Lissu. Vipi wewe mwenzetu unamjua aliyeamrisha Tundu Lissu ashambuliwe, una uhakika?.
  3. Hujui nani alikuwa nyuma ya utekaji wa Mo Dewji ?. Hata aliye nyuma ya shambulio hili mimi simjui, wewe mwenzetu unamjua?. Una uhakika?.
P
Mkuu P stuxnet alishakukuambia anakuheshimu na kwamba ukweli wote unaufahamu hivyo basi alikuomba muishie hapo. Sasa mbona ww umeamua kuendeleza malumbano au ww humuheshimu mwenzie? Au kwakuwa ukweli unaufahamu ila unajaribu kujiweka kando kusubiri hisani fulani toka kwa Mkuu wa Kupanga na Kupangua?
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,701
2,000
Naunga mkono hoja, ila uchaguzi ambao usifanyike ni uchaguzi wa rais tuu, Magufuli aendelee. Lakini kwa wabunge na madiwani, uchaguzi uendelee tuu kama kawaida kama nilivyoshauri hapa
https://www.jamiiforums.com/threads...na-haja-kufanya-uchaguzi-wa-rais-2020.980346/
Na kwenye huo uchaguzi wa wabunge na madiwani, kwa heshima ya utendaji uliotukaka wa rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano, katika uchaguzi wa wabunge na madiwani, Watanzania katika umoja wetu tutapaza sauti zetu na kuongea kwa sauti moja kupitia sanduku la kura kuwa tumemwelewa Magufuli na tunajua anataja kutupeleka wapi hivyo siku ya Uchaguzi Watanzania wote kazi ni moja tuu, "unachukua, unaweka, ..."
Malizia mwenyewe.
P
We Mayalla kwenye constitution Rais anapatikana vipi?hiyo gharama mnazozisema ndio amani yenyewe ya demokrasia

Mbona mahaba tamewajaa hadi mnataka kununua fundamentals za katiba ,This is a professional disgrace my dear
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,299
2,000
Katiba inatoa muongozo namna Rais, wabunge wanavyopatikana, kama itabaki hivyo then kufanya vinginevyo ni kukakaribisha kelele zisizo na msingi, gharama za chaguzi ni sehemu ya mfumo tulioamua kuuishi na unalindwa kikatiba.
Kuna makundi mawili hapa, the conservatives and the liberals.

Ma conservatives wanatumia kitu kinaitwa fast and hard rules, formular yao ni rules must be obeyed. Kama uchaguzi wa rais uko kwenye katiba na sheria, lazima ufanyike kwa mujibu wa katiba na sheria, nothing more, nothing less.
Huu ndio mtazamo wa ma conservatives, mambo yote yafanyike jinsi ile ile yanavyopaswa kufanyika.

Ma liberals wao wanasema lifanyike lile jambo tuu lenye manufaa kwa taifa. Uchaguzi is an expensive exercise na hakuna hata mara moja, Tanzania imeweza kufanya uchaguzi wake Mkuu kwa kujitegemea, hivyo uchaguzi ni gharama. Ikitokea mgombea fulani amepita bila kupingwa, gharama kubwa sana zinakuwa zimeepukwa. Trends za chaguzi zetu zote zinaonyesha hakuna hata mara moja imewahi kutokea a sitting president akashidwa, kwasababu
1. The playing field of the political landscape is not level, ni uwanja tenge. Mgombea mmoja anaingia kugombea na vingora, public resources, akiwa na vyombo vya dola mabegani mwake, kuanzia NEC, Polisi, Jeshi, Mahakama, na serikali nzima behind halafu anatoa kisu cha makali kuwili ili kigombewe huku yeye ameshika kwenye mpini!. Kama kuna yoyote anadhani anaweza kushindana na Magufuli hiyo 2020, with Magufuli's track record, this man needs his head seriously be examined!.
2. Japo tuko kwenye mfumo wa vyama vingi ikitegemewa vyama vyote vitakuwa sawa, it's not, CCM bado ni chama dola, chenye nguvu kumpita Goliati, chama kubwa toka chini kabisa kwenye mizizi hadi juu mbinguni , chama tajiri kwa loot ya Watanzania. Tajiri hawezi kushindana na masikini, masikini akashinda, ile story ya Daudi na Goliati, ni Mungu ndie alimpigania Daudi, labda na Tanzania Mungu ndie awapiganie opposition, tatizo linakuja ni opposition gani hiyo ikiyopo ya kupewa ikulu yetu?.
3. Tatu Tanzania mpaka sasa hapa tulipo, hatuna any serious and credible opposition ya kuichallenge CCM ambacho ni chama dola. Unashindana na chama dola ili kukipokonya hiyo dola, unategemea nini?.
4. Watanzania sio kama mbuzi, sisi ni kondoo, ukijumlisha na levels za ignorance ya walio wengi kufanya informed decision na levels za umasikini uliotopea wa kiwango cha t-shirt na kofia na mlo wa siku moja ni tosha kabisa kubadili matokeo.

Hivyo kwa upande wa urais, tunakwenda tuu kufanya igizo la uchaguzi wa rais. Sasa kwa umasikini wetu huu, is it worth it?. Ndio maana sisi ma liberals tunashauri let's have a room for maneuvering, akiwa mzuri na ame perform, apewe a walkover aendelee tuu bila kupoteza fedha kufanya maigizo.

P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,299
2,000
Mkuu P stuxnet alishakukuambia anakuheshimu na kwamba ukweli wote unaufahamu hivyo basi alikuomba muishie hapo. Sasa mbona ww umeamua kuendeleza malumbano au ww humuheshimu mwenzie? Au kwakuwa ukweli unaufahamu ila unajaribu kujiweka kando kusubiri hisani fulani toka kwa Mkuu wa Kupanga na Kupangua?
Duh...!. Haya bana, much respect.
P
 
Afya_tz

Member
Jul 30, 2019
55
250
Naunga mkono hoja, ila uchaguzi ambao usifanyike ni uchaguzi wa rais tuu, Magufuli aendelee. Lakini kwa wabunge na madiwani, uchaguzi uendelee tuu kama kawaida kama nilivyoshauri hapa
https://www.jamiiforums.com/threads...na-haja-kufanya-uchaguzi-wa-rais-2020.980346/
Na kwenye huo uchaguzi wa wabunge na madiwani, kwa heshima ya utendaji uliotukaka wa rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano, katika uchaguzi wa wabunge na madiwani, Watanzania katika umoja wetu tutapaza sauti zetu na kuongea kwa sauti moja kupitia sanduku la kura kuwa tumemwelewa Magufuli na tunajua anataja kutupeleka wapi hivyo siku ya Uchaguzi Watanzania wote kazi ni moja tuu, "unachukua, unaweka, ..."
Malizia mwenyewe.
P
Aisee kuna mambo yanaleta hasira hapa duniani
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,305

Siungi mkono hoja kwa sababu zifuatazo...

1. Uchaguzi haufanywi kwa mashinikizo wala maandamano... UPO KIKATIBA na maeleo yake yamenyooka kabisa... NITASHANGAA SANA KAMA POLISI WATARUHUSU MAANDAMANO YANAYOKWENDA KINYUME NA KATIBA....

2. Si kila mtanzania anamwelewa magufuli.... kuandamana kutaka kusifanyike uchaguzi, maana yake WASIOMWELEWA HAKI YAO YA KUPIGA KURA MNATAKA KUIPORA?

3. Kila chama kina mchakato wa kupata mgombea... na wengine huamua kushirikiana... HAKI YA CHAMA KUSIMAMISHA MGOMBEA MNATAKA KUIPORA?

4. Kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa... vile vile sanduku la kura ndi yo peke linalomwondoa mtu kwenye kinyang'anyilo... SASA HAKI YA MTU YA KUCHAGULIWA KUSHIKA NAFASI YA URAISI, MNATAKA KUIPORA?

Paskali... kwa hili mnaofikiri na kupenda litokee MNACHEMSHA... MNAIKANYAGA KATIBA
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,299
2,000
Siungi mkono hoja

Paskali... kwa hili mnaofikiri na kupenda litokee MNACHEMSHA... MNAIKANYAGA KATIBA
Kwa vile this is not the first kwa katiba kukanyagwa, then its not the last, katiba imekanyagwa sana tuu and nobody did anything, this time tuilanyage tuu for the goodness of this ro.ten and fuc.ken nation.
P
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,305
2,000
Kwa vile this is not the first kwa katiba kukanyagwa, then its not the last, katiba imekanyagwa sana tuu and nobody did anything, this time tuilanyage tuu for the goodness of this ro.ten and fuc.ken nation.
P
Kheee kiongozi ...!!! unhalalisha kosa kwa kosa? Yaani badala ya kuhangaika kurekebisha kosa unahalalisha... HILI SIKULITEGEMEA LITOKE KWAKO
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom