Kuna wanachama wa Upinzani 400 gerezani halafu mnasema kuna utulivu?

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Nasikitishwa sana na wanaosema eti Tanzania kuna amani na utulivu wakati wanachama wa chama wa CHADEMA takribani 400 na zaidi wako gerezani kwa kesi mbali mbali za kubambikizia za mauaji na uhujumu uchumi, huo utulivu unatokana na nini? Haikutosha mmeamua kumtupia kesi ya Ugaidi mwenyekiti wao kabisa.

Haya mambo yana mwisho na wanayotekeleza haya makusudi walaaniwe na wafe vifo vibaya sana kwa jina la Yesu na tutaendelea kumlilia Mola wetu.

Haiwezekani kesi karibia zote zisizokuwa na ushahidi zinawalenga wanachama wa chama kimoja, hakuna huruma ili miradi tu kikundi fulani cha watu wachache kiendelee kula keki ya nchi wakati wengine wanaendelea kuteseka magerezani wakiacha familia zao zikiteseka. Tunamuomba Mungu wetu muumba wa mbingu na ardhi amalizane nao ili taifa lipate kupumua.

Huku ndio kuponyona majereha au kushindilia maumivu. Haya mambo kuna wakati jamii itachoka na haitavumilia ndipo tutakapoelewa.
 
Duuuh, mimi mwanaccm lakini kama haya ni kweli basi polisi wetu hawafanyi sawa sawa wanapaswa kupangwa upya. IGP yupo kwanini haya mambo yapo kiasi hiki?
 
Wewe, watoto wa Mbowe, Msigwa, Lema au Lissu mbona hawako magereza?

Kwahiyo wewe ni kamanda wa CHADEMA kuliko watoto wa MTEI ??
 
May be baada ya hao watu kutolewa uraiani na kuwekwa sehemu salama ndiyo utulivu umepatikana, May be wao ndiyo walisababisha kusiwepo na utulivu nchini.....
 
Mkuu..unamaanisha kati ya wafungwa na maabusu walioko gerezani hakuna wanachama wa ccm?..Mimi naona mtu kama amefanya kosa awekwe tu ndani haijalishi anatoka chama gani
 
Mkuu..unamaanisha kati ya wafungwa na maabusu walioko gerezani hakuna wanachama wa ccm?..Mimi naona mtu kama amefanya kosa awekwe tu ndani haijalishi anatoka chama gani
Mzigo wa mwenzako kwako ni ganda la usufi
 
Unaye mpenda hutaona makosa yake mpaka uone kwa macho,usituaminishe upumbavu wako tuubebe wote,ww katengeneze madirisha huko

By the way polisi ni hawa hawa na hata serikali ikishikwa na chadema na si hao ccm bado polisi ni hao hao wala hamtaenda kuchukua polisi Malawi wala Zambia,na yamkini mkawa ndo watu wabaya sana sana kwa kutumia hao polisi dhidi ya hao ccm kwa kulipa visasi
 
Mkuu..unamaanisha kati ya wafungwa na maabusu walioko gerezani hakuna wanachama wa ccm?..Mimi naona mtu kama amefanya kosa awekwe tu ndani haijalishi anatoka chama gani

..bila shaka kuna wana-ccm, act, cuf, udp,
wako mahabusu au magerezani kwa makosa mbalimbali.

..malalamiko ya Chadema ni kwamba wanachama wao zaidi ya 400 wamekamatwa kutokana na kutumia HAKI yao ya kushiriki ktk siasa, wakati wakitekeleza majukumu yao ktk chama.

..Katika hili labda tungejiuliza ni vikao au mikutano mingapi ya CCM imewahi kuzuiliwa au kuvurugwa na jeshi la Polisi. Halafu tulinganishe na yanayoendelea kwa vyama vya upinzani.

..Pia tuangalie ni wanachama wangapi wa CCM wamefikishwa mahakamani kwa makosa waliyoyafanya ktk majukumu au shughuli za kisiasa. Baada ya hapo tulinganishe na idadi iliyoko kwa vyama vya upinzani.

..Hata ktk masuala ya uchaguzi. Tujaribu kuchunguza ni wagombea wangapi wa CCM wamewahi kuenguliwa na Tume ya Uchaguzi na Wakurugenzi, halafu tulinganishe na idadi ya wagombea wa upinzani walioenguliwa.

Cc Tindo , Erythrocyte
 
Wewe, watoto wa Mbowe, Msigwa, Lema au Lissu mbona hawako magereza?

Kwahiyo wewe ni kamanda wa CHADEMA kuliko watoto wa MTEI ??

..mtoto wa Mtei aliwahi kuwekwa kizuizini kwa muda mrefu baada ya uchaguzi wa 2015 kwa sababu za kisiasa.
 
Back
Top Bottom