Kuna wanachama siwaamini ndani ya Chadema

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Wana JF mimi kuna wanachama wapya wa Chadema sina imani nao kabisa. I dont have any personal issues with them but I am uncomfortable with them. I dont real know what they have in their hearts. Ni bwana Mabere Marando na Shibuda. They are very good in politics game lakini sina uhakika kama kweli ni wapinzani. Naomba kama kuna mtu anaweza nitoa wasi wasi nao anieleze. Asanteni na kama kuna niliemkwaza anisamehe,
 
Kuna Thomasi Nyimbo...
Rose Kamili
Mashishanga
Tundu Lissu - Huyu kutwa kupayuka kwenye vyombo vya habari badala ya kutumia vikao vya chama.
List goes on....
 
Hivi hamuwezi kujadili haya mambo kwenye vikao vyenu vya shina ama matawi badala ya kuleta ukumbini. Mbona wengine siyo wanachama wala wapenzi wa CLUB BILLICANAS?
 
Kuna Thomasi Nyimbo...
Rose Kamili
Mashishanga
Tundu Lissu - Huyu kutwa kupayuka kwenye vyombo vya habari badala ya kutumia vikao vya chama.
List goes on....

Do U have a Hidden Agenda?????
 
Shetani One,
usiwe na wasiwasi, chama kina katiba yake. Katika katiba hiyo haki na wajibu wa kila mwanachama na kiongozi umefafanuliwa.
Hili la kuwa na wasiwasi etc usiliendekeze. Kwenye siasa tukiruhusu hisia kufanya maamuzi, hatuwezi kufika popote.
 
Katiba, kanuni na taratibu za chama zitachuja nani abaki kwenye chama na nani atoke. Mafuta na maji huwa havichanganyiki, siku si nyingi tutajua pumba na mchele ni upi, naamini CHADEMA ina mfumo imara wa ndani wenye uwezo wa kushughulikia hayo yote. Ondoa shaka kaka!

YouTube - MH. JOHN SHIBUDA AONGEA (MichuziBlog)
 
Mwanzishaji wa thread hii alikuwa na nia njema lakini wakina Sokomoko wanajaribu kudandia kwa lengo tofauti; ukweli Shibuda ni ccm damu damu, ameingia chadema baada ya ccm kumkatalia kugombea ubunge. Kama kungelikuwapo upenyo wa kukidhi haja yake hiyo bila ya kutoka ccm angelifanya hivyo. Katika hali hiyo siyo mtu wa kuamini moja kwa moja. Kuhusu Marando huyo kinachosababisha watu kumtilia shaka ni historia yake ya ushushushu. Na wengine wanakumbuka alivyowahi kuchaguliwa kuingia kwenye bunge la Afrika Mashariki kwa nguvu za ccm. Zaidi ya hapo mimi binafsi, huwa nashindwa kuelewa ni kwanini alifika mahali akaiachia nccr(M) kudidimia mikononi mwa Mbatia! Ukiyahunganisha yote hayo inakuwa wazi kwamba ni mtu wakufanya naye kazi huku ukiwa mwangalifu.
 
Kwa hilo la kuingia chadema baada ya kukosa ubunge, hana tofauti na Dr. Slaa.

Na hilo la ushushu wa Marando - unakumbuka Dr. Slaa alisema mashushu wanaripoti kwa chadema. Sasa utawaogopa vipi watu wanaoripoti kwako?
 
Wana JF mimi kuna wanachama wapya wa Chadema sina imani nao kabisa. I dont have any personal issues with them but I am uncomfortable with them. I dont real know what they have in their hearts. Ni bwana Mabere Marando na Shibuda. They are very good in politics game lakini sina uhakika kama kweli ni wapinzani. Naomba kama kuna mtu anaweza nitoa wasi wasi nao anieleze. Asanteni na kama kuna niliemkwaza anisamehe,
Si vyema kuwahukumu watu kabla ya kutenda kosa tena ni kinyume cha haki zote zinazofahamika duniani. Binafsi sioni sababu za kuwatilia shaka kwani chama kinaongozwa na kanuni na katiba itakayopambanua pumba na mchele. Kufanyia kazi usalama wa taifa si sababu tosha kwa Marando kuwa "stigmatized" na kumtazama Shibuda kama CCM damu nikum-stigmatize pia. Watu hugeuka kufuatana na mazingira yanavyojifungua. Hakuna aliyezaliwa CCM kama ilivyo kwa Chadema na vyama vingine ambapo wengi waliopo katika kambi ya upinzani leo ndiyo walewale waliokuwa makada wa CCM. Kina Maalim Seif, Lipumba na hata Rais wa mioyo yetu (Dr. Slaa) waliwahi kuwa makada wazuri wa TANU na CCM na sintashangaa siku moja kumwona hata JK akijiunga na upinzani kadiri mazingira yatakavyojifunua. Vile vile wengine wanaotajwa kwa niaya kuwafitinisha wana CHADEMA kwani hata mimi mwenyewe nilikuwa mshabiki na kada mzuri tu wa CCM nikiwa Jeshini hadi baada ya siasa za vyama vingi kuingia na kustaafu. Chadema tunapaswa kuvitumia vipaji na ujuzi wa waliokuwa makada wa CCM wanaouelewa vyema uimara na udhaifu wa CCM. Moja ya mbinu wanazotaka kutumia CCM kuimaliza Chadema ni kupandikiza hali ya kutiliana shaka na kusababisha vurugu ili kukiua au kukipunguza kabisa nguvu chama hiki pekee cha upinzani wa kweli. Nawasihi wana Chadema wa kweli tuachane na propaganda za wahuni na walaghai hao ili waambulie patupu.
Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ibariki nchi yetu; Mama yetu Tanzania.
 
Wana JF mimi kuna wanachama wapya wa Chadema sina imani nao kabisa. I dont have any personal issues with them but I am uncomfortable with them. I dont real know what they have in their hearts. Ni bwana Mabere Marando na Shibuda. They are very good in politics game lakini sina uhakika kama kweli ni wapinzani. Naomba kama kuna mtu anaweza nitoa wasi wasi nao anieleze. Asanteni na kama kuna niliemkwaza anisamehe,

Time will tell , but atleast give them the benefit of doubt!
 
Bwana Mchillo asante kwa maelezo na kama ukumbukavyo mimi nilitaka kutolewa wasiwasi tu kuhusu hawa ndugu. Basi ni wenzteu tuendelee kuishi nao kwa imani kuwa sote ni wamoja
 
Back
Top Bottom